Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Wakiguswa wao wanasema watu tukiguswa sisi wanasema waalifu au wezi wao wanajiita wafanyabiashara ila sisi wanatuita vibaka. Sisi kinachotugawa ni haya matatizo na shida tunazopitia ambazo enzi ya mwamba hazikuwepo na sio maswala ya watu walipororwa hela zao ambazo nao waliwapora masikini kupitia kukwepa kodi.
 
..Ni kweli alikuwa na uwezo wa kushinda.

..sasa kwanini alicheza RAFU za kiwango kile?

..kwanini walienguliwa wagombea wengi kuzidi kipindi chochote kile?
Yaliyo pita si ndwele, tugange yajayo.

Kwa sababu huyu mama ni mwema sana anapenda maridhiano amekuja na 4R. Ongezea na viongozi wa wajuu wa CCM wanakiri hadharani kupitia makamu mwenyekiti wa CCM na katibu wa UWT na kuna mawaziri kadhaa pia wamesikika wakitoa kauli hizi Nape na Makamba.

Haki itendeke haraka sana, mwambieni raisi aitishe uchaguzi mkuu haraka sana mwaka huu, kuondoa dhulma iliyofanyika 2020 si anataka maradhiano na ana amini haki aikutendeka maana hizo kauli zimeongelewa mara kadhaa mbele yake na Kinana, Nchimbi na Makamba; hata yeye mwenyewe anaamini hivyo ndio maana akaja na hizo 4R.

Kwa hivyo hakuna namna zaidi ya kuitisha uchaguzi mkuu mwingine haraka sana kuondoa dhulma ya 2020.

Kama wapo kwa dhulma na CCM uongozi wa juu wa CCM mwenyekiti, makamu na katibu na baadhi ya mawaziri wao wanakubali waitishe uchaguzi kuwapa wananchi haki.

Kunufaika na dhulma maana yake na wewe ni sehemu ya dhulma na uhalifu uliotendeka. Mama aitishe uchaguzi haraka sana hakuna namna nchi aiwezi ongozwa na raisi anaekiri yupo pale kutokana na dhulma.

Credit ya wazo kwa mchangiaji wa JF nimeokota kwenye mada nyingine
Kambi ya Fisi
 
Ukifa hauozi bwasheee.
Stieggler Ile pale 2225MW - tunaweza kusahau kabisa shida ya umeme tukitumia akili.
Tanzania ya viwanda na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda - Sasa hivi wote tumerudi kwenye uchuuzi.
Daraja la juu pale busisi - Mwanza.
Ujenzi wa reli ya kisasa Dar - Mwanza.
Kuifanya shillingi kuwa stable - Sasa hivi shillingi Kila siku inayumba.
Kuleta nidhamu ya utendaji serikali.
Kulifufua shirika la ndege lililokufa.
Kuboresha usafiri ziwa Victoria.
Kufanya watu waiogope na kuiheshimu dola.
Ujenzi wa miundombinu Kila Kona ya nchi.
Ujenzi wa masoko ya kisasa maeneo mbalimbali.
Ujenzi wa hospitali za rufaa Kila mkoa.
Kuboresha huduma za afya Kwa kununua vifaa vya kisasa (VP MRI nzima pale Muhimbili?).
Kujenga smelter ya Dhahabu pale Mwanza.
BOT kuanza kununua dhahabu na kuweka reserve ( Vipi ile reserve bado IPO?).
Kudhibiti utoroshwaji wa madini.
Kuruhusu wachimbaji wadogo wadogo kupewa maeneo na kuchimba ( Sasa magiants wameanza kuhodhi maeneo na kufanya udalali Kwa Wazungu na wachina).
Kudhibiti matumizi ya hovyo ya serikali ( watu wanapishana angani tu Sasa hivi, na mijengo wananunua).

HAYO YOTE NDANI YA MIAKA SITA.
HATUTAKI BLAH BLAH TUNATAKA MATOKEO CHANYA.
.......
 
Acha ujinga wewe ni Bora wachache wafe ili taifa lipone mfano huyo makamba wako anafaida gn kututoa kwenye kuunga umeme Kwa elfu ishirini na Saba mpaka laki tatu na nusu na manguzo wakarudisha zile Bei za enzi ya upigaji ya mkwere? Kuna faida gani yakuwa na watu kama Hawa wasiokuwa na huruma na maskini wa nchi hii? Hawa walitakiwa wapigwe risasi hadharani sijui kwanini magufuli aliwaacha Hawa mchwa wa hili taifa
Ooh ok. Kwani bado yupo kwenye hiyo wizara? Si alishaondolewa? Vipi bei ya kuunganisha umeme imeshuka?
 
Jiwe alikuwa mshenzi sana. Asante mhe. January Makamba kwa kulisema hili ili dunia ijue. Na January ndiyo mwanaccm pekee uliyebakia kuwa na akili.

Mhe. January Makamba naomba uende mbali zaidi, kwa kuitaka serikali kifuta kumbukumbu zote za serikali zinazomtambua jiwe kama mmoja wa watu waliowahi kuwa marais nchi hii.
Acha kumsingizia Makamba mambo makubwa. Makamba ana akili? Wewe unafikiri akili ni kama arsehole kila mtu analo? Mtu kilaza kabisa kama huyo unasema ana akili.... Wewe kwenu utakuaje?
 
..Januari anasema kuna viongozi walikuwa wanaidharau Wizara na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Raisi kiasi cha kufikia kutowasalimia.
Na hao ndiyo hawa wanaolalamika sasa.
Baada kuipuuza ofisi ya Makamo wa rais na Wizara zilizokuwa chini yake, wakajikuta kwenye taharuki isiyo kifani baada kipenzi chao kufariki Dunia.
Walisahau kwamba binadamu hufa.
 
Yaliyo pita si ndwele, tugange yajayo.

Kwa sababu huyu mama ni mwema sana anapenda maridhiano amekuja na 4R. Ongezea na viongozi wa wajuu wa CCM wanakiri hadharani kupitia makamu mwenyekiti wa CCM na katibu wa UWT na kuna mawaziri kadhaa pia wamesikika wakitoa kauli hizi Nape na Makamba.

Haki itendeke haraka sana, mwambieni raisi aitishe uchaguzi mkuu haraka sana mwaka huu, kuondoa dhulma iliyofanyika 2020 si anataka maradhiano na ana amini haki aikutendeka maana hizo kauli zimeongelewa mara kadhaa mbele yake na Kinana, Nchimbi na Makamba; hata yeye mwenyewe anaamini hivyo ndio maana akaja na hizo 4R.

Kwa hivyo hakuna namna zaidi ya kuitisha uchaguzi mkuu mwingine haraka sana kuondoa dhulma ya 2020.

Kama wapo kwa dhulma na CCM uongozi wa juu wa CCM mwenyekiti, makamu na katibu na baadhi ya mawaziri wao wanakubali waitishe uchaguzi kuwapa wananchi haki.

Kunufaika na dhulma maana yake na wewe ni sehemu ya dhulma na uhalifu uliotendeka. Mama aitishe uchaguzi haraka sana hakuna namna nchi aiwezi ongozwa na raisi anaekiri yupo pale kutokana na dhulma.

Credit ya wazo kwa mchangiaji wa JF nimeokota kwenye mada nyingine
Kambi ya Fisi

..waliodhulumiwa watambuliwe, waombwe radhi, na watendewe haki. Baada ya hayo kufanyika ndipo tutaweza kusema waliyopitia si ndwele...
 
Makamba amepewa shinikizo ili CCM kuendelea wanabidi waendekeze propaganda za magharibi.

Ni aibu.

Hii ni vita ya Kisakilojia tu, kwamba asitokee mwingine kuja kudai Rasilimali ni za Waafrika pekee. Kwmba MWafrika anajiweza kisiasa na kiuchumi.

Makamba ni mnafiki. Yeye alihusika 2000%

Kitaeleweka 2900's msisahau, mpitie hapa.
 
Mengi kati ya haya uliyoyaorodhesha hapa hata wakoloni waliyafanya na watu walidai uhuru.

Maendeleo ni maendeleo ya watu mkuu. Na demokrasia ni pale individual anapofeel yupo free and unharrassed kwenye nchi yake.
Watu wakiona hawako huru, na serikali haipo kwa ajili yao na haitokani na matakwa yao yaani wamepoteza yale mamlaka yanayowatambua kuwa wao ndo wenye nchi, hayo yoote uliyoyaandika hapo yanakua hayana maana kiongozi.

Utu ni kitu cha maana kuliko vitu.
Ma+vi
Ndio maana nasema sisi ngozi nyeusi tumelaaniwa
 
Back
Top Bottom