Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

uungwana ni maneno na matendo 🐒

ni umakini na ujasiri wa kiwango cha juu sana kwa taasisi na watu wake kujitathmini, kujisahihisha, kujirekebisha, kuziba nyufa, kuondoa kazoro na kuja na mawazo mapya, mipango mikakati mipya na kusonga mbele vizuri zaidi, kwa umahiri zaidi na kwa uhakika zaidi 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Tuepushe na Roho kujipa umuhimu zaidi ya wengine na kujihesabia haki 🐒
 
Naomba nisimuwekee maneno Makamba.

Maneno aliyoyazungumza ni tuhuma nzito kwa utawala wa Rais Magufuli.
Sasa kwani si Samia yupo? Majaliwa yupo? Mwigulu yupo? Aliyekufa ni mmoja tuu lakini wote wapo sasa hapa wana mdanganya nani? Na nyie mnajifariji kwa kupenda kusikia wanasema bila matendo? Hivi walio haribu uchaguzi si wapo? Nani kafa zaidi ya Magufuli?
Kwanini Sasa wasikubali Tume huru ya Uchaguzi kuvunja mzizi wa fitina?
 
1. Je, wanasiasa walifungwa?

2.Je, kuna walionyang'anywa fedha?

3. Je, kuna walioharibiwa biashara zao?

4. Je, shughuli za vyama vya siasa zilizuiliwa?

5. Je, uchaguzi haukuwa na makandokando?
Exactly!
Badala ya kumshambulia marope ni vzr kwanza kujibu hoja zake
 
Kwani hajulikani au wewe ndiye usiyemjua!!?
Kinachosubiriwa ni kuanza kutajana wao wenyewe.
 
So aliyosema Makamba ni uongo?
 
Ni uchaguzi wa mwaka gani uliwahi kuwaunganisha?

Uchaguzi wa 2015 ndiyo mgombea ubunge Alphonse Mawazo aliuwawa kama kibaka huko Geita!

Hakuna Tajiri amewahi kuharibiwa biashara kwa sababu ya siasa za uchaguzi kumzidi Mzee Tango kisa Mrema mwaka 1995.

Kama Makamba anamaanisha kweli si awashauri wenzie huko cabinet ipatikane katiba mpya na tume ya uchaguzi isiyojaa makada.
 
Hakuna kupumzika.
Yule lazima achomwe moto sn tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…