Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Kwa hiyo mchezaji aliyekaa U-20 yako kwa chini ya mwaka mmoja, tena program yako ya vijana isiyo na mbele wala nyuma na haujatoa mchezaji yoyote wa maana kutoka katika program hiyo kwa miaka 10, leo unamlipa milioni 15, na juzi juzi tu ulikuwa unamlipa milioni 2. Umesimama mbele ya majaji wa CAS, embu jitetee hiyo value ya Mzize ya bilioni 2 inatokea wapi? Kwa gharama zipi ulizoingia kwa mchezaji huyo?

Mkuu naona upo nyuma sana
Kadri muda unasogea value ya bidhaa inaongezeka kutokana na ufanisi wake

Sasa tuambie mzize wa yanga B na wa sasa wanaendana?? Ulitaka auzwe bei gani??
Klabu yenu ina miaka 100 na haijawahi kununua mchezaji kwa hata 800M, mnatajataja tu 2B mnadhani pesa ya madafu hiyo.

Mnatoa mifano ya mizigo sijui kutoa shambani hadi sokoni. Basi peleka sokoni nyanya zako halafu sema unauza kilo 100K, si mali yako bwana na una haki ya kujipangia bei? Hapo ndiyo maana ya mchezaji siyo mtumwa inapoingia.

Unaweza kusaini mkataba lakini baadae ukienda kulalamika mbele ya vyombo vya sheria na haki, mkataba ukaonekana siyo halali, sijui kama unajua hilo.
 
Mshahara na marupurupu ya Feisal pale Azam, gharama yake inaweza kukaribia Bilioni kwa mwaka. Nyie mnalinganisha na mchezaji mnayemlipa milioni 15 tena huo ni mkataba mpya, kabla ya hapo mlikuwa mnamlipa milioni 2.

Mnapenda kulinganisha na kuzitaja sana hizo timu za Ulaya sijui ni ushamba, kutojua au nini. Mnajua mishahara ya huko hata mchezaji akitoka tu timu ndogo au za vijana?
 
Sasa tunapata picha kamili

Nikataka kushangaa kumbe alileta ujanja tu?

Na huyu jemedari ndiyo sababu ya kuichukia yanga sana kwani alinyimwa nini?
Wakati wa uongozi wa msola,jemedari alikua mmojawapo wa walioomba nafasi ya ukatibu wa Yanga,na kwa 100%,jemedari ndio alikua anaenda kuwa katibu,jamaa ni meneja wa baadhi ya wachezaji,kama utakumbuka kakolanya akiwepo Yanga meneja wake alikua ni mmoja wa wajumbe wa kamati za simba,kuna derby ile Yanga chovu beno aling'ara mno,simba kwa kutumia mjumbe wake beno akaenda simba msimu uliofuata,jemedari kule simba alikua anawasimania john boco na manula na kipindi kile ndio walikua roho ya timu,kwa Yanga alikua anamsimamia gadiel michael,so simba ili kuzuia meneja wa wachezaji wao tegemeo asifanye kazi Yanga,wakatumia njia ya kumgombanisha na Yanga,simba kupitia makonda na haji manara wakamshawishi gadiel michael asaini simba akiwa kambini na taifa stars afcon iliyofanyika misri,kama utakumbuka kipindi cha magu, kibaya gadiel akijua kishasaini simba akawa anawazungusha viongozi wa Yanga ataenda kusaini hadi siku ya kufungwa dirisha ndio msola anagundua,hapo Yanga ikawa haina ujanja ikaenda kumuokota dogo mmoja mzanzibar marcelo maana hawakua na muda tena wa kupata beki wa kushoto mzuri,na kuanzia wakaachana jemedari maana haiwezekani mchezaji asaini meneja usijue,ndio toka hapo mzee wa nongwa akaingia kwenye mzozo na Yanga,jamaa majungu mno,alimpiga sana majungu saad kawemba pale azam,muulize oscar oscar alifukuzwa kazi azam media sababu ya nani
 
Kama hana hiyo thamani kwenye termination aununue huo mkataba kwa thamani aliyosaini kuwa anayo kisha aende kama mchezaji huru asisubiri kuuzwa. Halafu binafsi siipendi Yanga ila nimeongea tu mtazamo wangu.
 
Kama hana hiyo thamani kwenye termination aununue huo mkataba kwa thamani aliyosaini kuwa anayo kisha aende kama mchezaji huru asisubiri kuuzwa. Halafu binafsi siipendi Yanga ila nimeongea tu mtazamo wangu.
Yanga wanaweka hivyo vipengele kukomoa. Hawezi kuwa unamlipa mchezaji mshahara wa milioni 2 sijui 15 halafu kipengele cha kuvunja ni bilioni 2. Siyo mkataba wenye uhalisia maana uwekezaji wa klabu kwa mchezaji hauendani na kile wanachotaka kuvuna.

Hawaingii mikataba hiyo ya hovyo na wachezaji wa kigeni na wachezaji wazawa wanasaini kwa sababu ya njaa na ni kama hawategemei kuwa itatokea timu hapo kati ikawataka.

Wazawa wamezoea kutumikia mikataba hadi inaisha au wanaachwa na vilabu kabla mkataba haujaisha kwa hiyo hivyo vipengele wamekuwa hawavizingatii sana.
 
Reactions: Tsh
Hiyo mil 15 mshahara kwa mwaka total ni 180m ,tufanye marupurupu 100m kwa mwaka Fei anacholipwa hakizidi hata mil 300 kwa mwaka na bado Azam wanataka 2.5bil.

Mlikimbia hesabu ndio maana pamoja na mikataba mikubwa mliyo ingia bado Mo anawadai bil 87.
 
Hahaha, sasa na mchezaji alipaswa kujua thamani yake. Club yenyewe inawaza kuvuna pesa, ni jukumu la mchezaji kuhakikisha na yeye anavuna, asisubiri huruma. Alipoona hiyo clause ya B2 angesema anataka mshahara M50 badala ya M15 au aondoke huru.
 
Hiyo mil 15 mshahara kwa mwaka total ni 180m ,tufanye marupurupu 100m kwa mwaka Fei anacholipwa hakizidi hata mil 300 kwa mwaka na bado Azam wanataka 2.5bil.

Mlikimbia hesabu ndio maana pamoja na mikataba mikubwa mliyo ingia bado Mo anawadai bil 87.
Marupurupu gani hayo ambayo Mzize analipwa mil 100?

Unamuingiza Mo unadhani tunaongea Usimba na Uyanga hapa.
 
Wale wakina bangala na juma waliingizwa cha kike na uyo dalali, mchezaji bado ana mkataba wa mwaka Mmoja na klabu alafu anahojiwa anasema Nina 90% kuondoka na 10% kubaki wakati bado anao mkataba halali kilichowakuta mpaka sasa wanalo la kujifunza sababu ya kushikiwa masikio!
 
Umeandika kama wewe ndiyo Jasmine!! Kha! Povu kama lote.
 
Hahaha, sasa na mchezaji alipaswa kujua thamani yake. Club yenyewe inawaza kuvuna pesa, ni jukumu la mchezaji kuhakikisha na yeye anavuna, asisubiri huruma. Alipoona hiyo clause ya B2 angesema anataka mshahara M50 badala ya M15 au aondoke huru.
Ni wazi Mzize ana woga fulani. Kawasikiliza waswahili kama hawa waliopo kwenye uzi huu. Mswahili anaweza kutaka kukuzurumu au kukufichia fursa huku anakwambia "kumbuka kuna kesho". Ndiyo maana wanaleta vimaneno vya kinafki kama "tunaangalia maslahi yake asije kwenda kukosa nafasi ya kucheza"
 
Reactions: Tsh
Jasmine ameanza kumsimamia mzie hivi majuzi tu hapa kabla hajasaini mkataba mpya
Kwa kauli hii, unakiri kuwa Jasmine ndiye msimamizi wa Mzize kwa sasa.
NB: Nimeona hapo pengine unazungumzia mambo ya kutambuliwa na FIFA. Nadhani hujui tofauti ya wakala na meneja. FYI hata akina Jemedari Said Kazumari ni wasimamizi wa akina Manula, sio mawakala na wala hawahitaji kutambuliwa na FIFA
 
Ukitaka kuamini mashabiki wa Simba ni mambumbu kwelii pitia comments zao utaelewa .
 
Na unadhani kila mara kunapotokea mgogoro ni kwa maslahi ya Club basi? Ni vile tu mashabiki huwa hawavui vazi la ushabiki otherwise shabiki unaweza kuwa unafikiri unaipigania Club kumbe unapigania tumbo la mtu mwenye cheo fulani anayenufaika na uwepo wa mchezaji na wala sio Club.
 
Unaposema "wakala wa mchezaji anaangalia maslahi ya mchezaji kuanzia mshahara na marupurupu mengine" unataka kusema nini?
Clement Mzize alipelekwa Yanga na hilo tapeli lenu Jasmine? Au alianzia timu ya vijana, tena ni baada scout kumuona kwenye mashindano ya ndondo na ndipo akapelekwa U20 ya Yanga?

Sasa huyo Jasmine leo ndiyo anajifanya ana uchungu na Mzize ambaye hata alipotoka, hajui!! Acheni upotoshaji wenu hapa. Hatma ya Mzize kwenda kucheza nje iko mikononi mwake yeye mwenyewe, na timu yake ya Yanga! Na siyo huyo wakala mtafuta 10%.
 
Sijaona contract ya Mzize, vip ya Fei uliiona? Mpaka ya kafikia 1 bil.
Kama Feisal analipwa milioni 300 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka 3 ni milioni 900. Jumlisha na signing fee.

Mnajua value ya mauzo ya mchezaji inavyopatikana au mnadhani hii ni biashara ya machinga unajitajia tu bei unayojisikia?
 
Kama Feisal analipwa milioni 300 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka 3 ni milioni 900. Jumlisha na signing fee.

Mnajua value ya mauzo ya mchezaji inavyopatikana au mnadhani hii ni biashara ya machinga unajitajia tu bei unayojisikia?
Unaijua signing fee ya Mzize mkataba mpya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…