Je, inawezekana Jakaya Kikwete ndiye Nyerere wa leo?

Acha dharau unawezaje kumfananisha Nyerere na kikwete

Nyerere alikuwa mbali Sana kuliko akina kikwete ,na maraisi wengine kiufupi sioni wa kufananisha na Nyerere
Tuache porojo twende na Facts

Mimi nasimama na Jakaya wewe simama na Nyerere halafu tuanze kutaja mafanikio na madhaifu ya kila mmoja
 
Msoga was one of the best Leader existed as Butiama was one best president existed in different era

Msoga = the extreme corruption
Butiama = the extreme dictator with fake Constitution.
 
kweli kabisaaaa. mimi nampenda sana kikwete na kusema ukweli kamzidi nyerere mara 70x70.
Kikwete kajenga secondari za kata nchi nzima na kuwaokoa vijana wengi kurudia rudia darasa la sana!
Kikwete kajenga high schools kila wilaya nchi nzima na kufanya elimu ya secondari na high school kuwa haki ya raia
Kikwete huyo huyo kajenga UDOM na kupeleka wanafunzi wengi chuo kikuu kupita nchi zote kusini mwa jangwa la sahala!
kikwete alifanyia kazi matatizo ya mwananchi mtanzania katika elimu hapo alikomboa wanyonge.
 

Huna unachoelewa, umekalilishwa vitu masijid/madirasa! Biafra alikowatetea walikuwa wanakaa wakristo? Wakati anavunja mahusiano na Israeli kwa sbb ya mateso ya Wapalestina, hao waparestina ni wakatoriki? Ufia dini ni uchizi uliopitiliza aisee
 
Wala hakuna kitu kama hicho. Jibu ni kuwa ndiye rais mstafu ambaye anaishi kwa sasa. Mwinyi ameshazeeka hawezi kushauri chochote
 
Hapana, haiwezwkani. Jakaya yupo juu sana ya Nyerere kiuongozi.

Magu ndiye unaweza kumfananisha na Nyerere, wote hao walikuwa hawaambiliki, wakurupukaji na walitumia nguvu nyingi kuliko akili katika uongozi.
Napenda kukupinga, huyo Jakaya ni mwanafunzi wa Nyerere aliyekuzwa nae kiuongozi. Nyerere alihakikisha anaacha kizazi cha viongozi wenye umri mdogo waje walifae taifa siku za baadae.

Na ndio hawa kina Jakaya, Lowassa, Mkuchika, Ole Sendeka, Lukuvi na wengine wa umri huo.
 
Hivi ulikuwa huelewi kuwa mwanafunzi siku zote huwa zaidi ya aliyemfundisha? Fikiri.
 
Ukiwapanga marais wanne bora kidemokrasia nchini
Namba 1 ni JKN
2. Mzee Ruksah
3. Ni JMK
4. Samia (huyu mpaka amalize kipindi chake akiendelea hiv, akawapuuza wahafidhina) kuna uwezekano akawa namba 2)
5. Mkapa
6. Hakuna
Mimi kwangu ni:
1.Mkapa Benjamin
2.Nyerere Julius
3.Kikwete Jakaya
4.Magufuri John
5.Ali Hassan Mwinyi
6.Samiah Suluhu.
 
Hata hivyo mwalimu ni binadamu kama wengine wala si haramu kumlinganisha na wengine kwani kipaji alichopewa yeye pia Mungu anaweza kumjaalia mtu mwingine kama alivyomjaalia yeye na hakumfanya kuwa binadamu wa kipekee ndiyo maana hata kwenye uongozi wake kuna makosa kadhaa aliyafanya na mengine ndiyo yamesababisha umasikini wetu hadi leo hii.
 
Huna unachoelewa, umekalilishwa vitu masijid/madirasa! Biafra alikowatetea walikuwa wanakaa wakristo? Wakati anavunja mahusiano na Israeli kwa sbb ya mateso ya Wapalestina, hao waparestina ni wakatoriki? Ufia dini ni uchizi uliopitiliza aisee
Kwa hiyo Nyerere kuimasikinisha nchi kwa kujiingiza ktk ma vita ya kusini mwa Africa yasiyokuwa na tija na ile ya Uganda kumtetea mkatoliki mwenzake Milton Obote wewe unaona ni sawa? Wewe kweli kilaza na umekunywa maji ya bendera.
 
Soma reference zenye akili kisha ndo uje kuandika. Wajerumani walipofika tanganyika walikuta wasomi wakiwa waislamu ambao waliandika kila kitu kwa hati ya kiarabu.
Taasisi ya EAST AFRICA MUSLIM WELFARE SOCIETY iliyojenga mashule kibao Tanganyika kwa ajili ya waislamu Nyerere aliipiga ban mwaka 1968.
Kama ni mtu wa usawa kwa nini hakupiga marufuku mashirika ya kikristo yaliyomiliki shule mbalimbali ili kufanya usawa?
Sasa nakusaidia. Kasome Kitabu cha Padre Dr John Sivalon na Kitabu cha Mohamed Said humo utapata kumjua Nyerere ni nani hasa na utaacha porojo zako ulizodesa kutoka magazeti ya uhuru na mzalendo. Utaelewa kwa nini wakati wa kuandika historia ya Tanganyika na uhuru wake walipewa hiyo kazi watu 2 :
1. Dr Wilbert Kleruu
2. Abdulwaheed Sykes
Baadaye Abdulwaheed akaondolewa na akaandika Dr Kleruu peke yake.
SOMA KIJANA ACHA POVU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…