Je, kuna faida gani ya kuwa na mikutano ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi?

Ila CCM ina vichwa jamani!! Hiki nacho ni kichwa cha CCM na kinaongoza vikao vya wilaya.
 
We unadhan kuna hasara gani watu kufanyia mikutano?

Kwann uwapangie watu namna na wakati wa kuongea?
 
Kwani walioibiwa kura wakifanya mikutano yao wanamzuia nini mwizi wa kura kufanya kazi zake?
 
VICHAA tu WANAJUA UMUHIMU wa hiyo MIKUTANO sasa wewe sijui tukuweke kwenye kundi gani
 
Hapa Tanzania kuna mambo mengi ya kizamani sana ambayo tunayafanya kwa kweli tunapaswa kubadilika.
 
Hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya mikutano
Kwa kifupi ni ujinga tu ndiyo unakusumbua kama siyo kuathirika na udikteta wa Magufuli wa kutaka kujimilikisha nchi na watu wake!
 
Kwa sababu ndio mwanzo wa kampeni za vyama Kwa ajiri ya chaguzi inayofuata...kimkakati zaidi...
 
Mikutano ikizuiwa MIKOPO INAPIGWA ban,

Acha iendelee maana mtoa PESA ndo huchagua WIMBO.
 
Hiyo mikutano itachochea utekelezaji wa ilani ya chama tawala kwani miamba itakapopita maeneo mbalimbali mojawapo ni kuwakumbusha wananchi wa eneo hilo kwamba hao sisiyemu waliahidi hiki au kile na kuwaambia waachane nao hali hiyo itawachochea sisiyemu kufanya utekelezaji ili waendelee kuaminiwa na wananchi wa eneo husika.Kubwa zaidi wabunge waliokuwa wanahamia Dar immediately baada ya kushinda si tu watapungua ila wataisha.Ukaribu kati ya wabunge na wapiga kura utaimarika sana.Kwa ufupi atakayefaidika na maamuzi ya mh Rais kuruhusu hii mikutano ni mwananchi ambaye ni mpiga kura.
 
Umelaximishwa kwenda kwenye mikutatano wewe chawa?
 
Umelaximishwa kwenda kwenye mikutatano wewe chawa?
Ungekuwa inafatilia hata threads zangu za nyuma ungejua mitazamo wangu.
Hata ningekuwa mwana ccm nisingekubali kuwa chawa asilani
 

Kungekuwa na uchaguzi wa kweli hoja yako wangalau ingekuwa na maana. Hii tabia ya chama kimoja kunajisi uchaguzi kisha tukae pembeni kusubiri kiharibu kitakavyo bila watu kusikia upande mwingine sio sawa. Vyama vingine vitakaa kimya, kisha ikifika uchaguzi mwingine hata kama wananchi hawaridhiki na hicho chama wanapora tena uchaguzi. Kwahiyo huko bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani kunakuwa kumejaa watu wasio na uhalali wa umma.

Hiyo mikutano ya vyama vya siasa itaonyesha kile ambacho hakipatikani huko bungeni, na kwenye mabaraza ya madiwani. Uzuri wa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa hushurutishwi kuisikiliza, wala kuhudhuria. Huenda ww ni mfaidika wa vyeo vya wizi wa kura, hivyo hutaki wananchi kusikia mambo mbadala kutoka kwa vyama vingine, maana unajua wananchi watapata ufahamu.
 
Wanaleta usumbufu kwa viongozi tu
Viongozi wasio na uwezo ndio wataona usumbufu, huenda ww ni kiongozi mwenye uwezo mdogo, hivyo unahofia hii changamoto. Nina hakika ww ulikuwa ni mmoja ya walioshauri kuzuia hiyo mikutano. Mbona kila siku tunaona mikutano ya hadhara viongozi wa dini, na hatuoni viongozi wa dini nyingine wakishindwa kufanya kazi zao kisa kuna mikutano ya hadhara ya kidini?
 

Huko Botswana na Zambia viongozi wanaingia madarakani ndio maana hawaogopi mikutano ya vyama vya siasa. Hapa chama kimekaa madarakani zaidi ya miaka 50 kwa shuruti, hivyo kikisikia tu mikutano ya vyama vingine kinajua wazi udhaifu wake utafanikwa. Bila kuitoa CCM madarakani tena kwa machafuko wataendelea kufanya mambo ya ajabu, huku wakigoma kuhojiwa popote.
 
Hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya mikutano
Hiyo mikutano sijui makongamano ya dini, wao hawana namna nyingine ya kupata waumini lazima mikutano ya hadhara? Au kwenye mikutano ya dini huna shida nayo maana haigusi maslahi ya walioko madarakani kwa wizi wa kura?
 
Hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya mikutano
Katika nchi zetu mikutano ndio njia Bora pekee inyompa fursa mwananchi kukutana na wanasiasa ana kwa ana iliaweze kuuliza ,kueleza ,kuhoji,na kupata elimu inayohusiana na sera za chama husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…