Je, kuna faida gani ya kuwa na mikutano ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi?

mimi ni Raia wa kawaida ambae sijaona umuhimu wa hiyo mikutano
 
Umenena vyema mkuu, hawa wanasiasa wanaturudisha nyuma
Wewe inaonekana hata ukilala njaa utasema ni wanasiasa wamesababisha ilhali ni uzembe wako.

Kwani Kuna mwanasiasa amewahi kukufunga kamba shingoni na kulazimisha kwenda kwenye mkutano wake?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hawezi kukuelewa, kumuelewesha chizi ni kujipa kazi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ila unaona umuhimu wa mikutano ya dini?
mikutano ya dini imengiaje ? wao hufanya mikutano kwa nia ya kutangaza habri za yesu au mtume
 
Faida ni kubwa sana kama mikutano hiyo italenga kuikumbusha serikali iliyoundwa na chama kilichoshinda uchaguzi kuhusu utekelezaji wa ahadi ilizoahidi kwa wananchi na kukikosoa pale kinapokwenda kinyume na maslahi mapana ya taifa na haki za raia. Lakini kama vyama vya siasa vitakuwa na agenda binafsi kwa maslahi yao binafsi na vyama vyao sioni umuhimu wa mikutano ya siasa baada ya uchaguzi.
 
Watanzania ni lazima tujiepushe na maswali ya kivivu maana yanaleta tabia za kivivu

Kuuliza “ kuna faida gani” ni misemo ya kivivu sana. Ni misemo ya kulalama na sio kujenga

Maswali ni kama

Je tufanye nini kusaida taifa?

Toa mbinu?

Yaani Watanzania kukutana na wananchi kujadili nchi yao unauliza kuna faida gani kweli? Hivi tuna watu wa type gani sikuhizi hapa?
 
Kwan katiba inasemaje? Na nn kinawakera kuwepo kwa mikutano ya kisiasa? Maana hawazuii utawala kufanya kaz zao! Kila mmoja atakula alikopeleka mboga!!
 
Je, kuna faida gani kutawadha baada ya kwenda haja kubwa?
 
Ni mjinga tu ndo anayeweza kuona mikutano ya hadhara inaweza kumzuia aliyeko madarakani ashindwe kutekeleza majukumu yake ...
 
mikutano ya dini imengiaje ? wao hufanya mikutano kwa nia ya kutangaza habri za yesu au mtume

Vyama vya siasa hufanya mikutano ya hadhara kwanza kwa mujibu wa katiba, pili ni kuhubiri sera za, na tatu mikutano ya hadhara ni fursa ya wao kuvutia wanachama wapya kupitia sera zao. Usipoelewa uliza.
 
Swali la kujiuliza, Kwa Nini kuwe na upinzani kama mnatekeleza majukumu yenu? nyie chama Cha mambuzi
 
Ni mjinga tu ndo anayeweza kuona mikutano ya hadhara inaweza kumzuia aliyeko madarakani ashindwe kutekeleza majukumu yake ...
hiyo mikutano haina faida yoyote ni bora aachwe aliyeshinda atekeleze Ilani yake
 
Vyama vya siasa hufanya mikutano ya hadhara kwanza kwa mujibu wa katiba, pili ni kuhubiri sera za, na tatu mikutano ya hadhara ni fursa ya wao kuvutia wanachama wapya kupitia sera zao. Usipoelewa uliza.
Wewe ni mgumu kuelewa mikutano ya dini na siasa wapi na wapi
 
Kwani mikutano ya siasa inazua vipi chama kilichopo madarakani kutekeleza sera zake
 
Mswahili bila fimbo aendi, chama tawala bila amsha amsha hakiwezi leta maendeleo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…