Je, kuna faida gani ya kuwa na mikutano ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi?

Mswahili bila fimbo aendi, chama tawala bila amsha amsha hakiwezi leta maendeleo
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tatizo hata mkiletelewa mtu anataka mabadiliko na maendeleo mtamkataa tu watanzania uwezo wa kufikiri mdogo sana
 
Wewe ni mgumu kuelewa mikutano ya dini na siasa wapi na wapi

Tofauti yake ni nini boss, maana wote ni hadharani na kelele ni sawa. Isipokuwa kundi moja linahubiri imani na lingine sera. Approach zao ni sawa. Labda useme hofu yako ni kuwa wa dini hawagusi maslahi ya waliongia madarakani kwa wizi kura, hivyo unaowaona hawana madhara, ila mikutano ya siasa inagusa moja kwa moja maslahi ya majizi ya kura.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tatizo hata mkiletelewa mtu anataka mabadiliko na maendeleo mtamkataa tu watanzania uwezo wa kufikiri mdogo sana

Maendeleo yanaletwa na watu kupitia kodi zao, na sio mtu. Hakuna mtu anaweza kutoa mshahara wake kuleta maendeleo maana hautoshi. Ukisikia mtu anasema analeta maendeleo ujue huyo ni tapeli. Na mara nyingi mtu wa aina hiyo utakuta ni mwizi, na huwa na vikundi vya kikatili kuumiza watu wasiomsujudia.
 
hiyo mikutano haina faida yoyote ni bora aachwe aliyeshinda atekeleze Ilani yake

Kama angeshinda hadi leo matokeo ya uchaguzi wangeogopa kuyaweka kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kama sheria inavyotaka?
 
Kama angeshinda hadi leo matokeo ya uchaguzi wangeogopa kuyaweka kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kama sheria inavyotaka?
usome post ya mtoa maada alivyoanza kilaza wewe
 
Post ya mtoa mada iko na marking scheme nini, kiasi kwamba tutoe majibu yanayoendana na hisia zake?
kwa hiyo hapa unadhani umekuja kuexpress hisia zako au kichangia mada ?
 
Hoja yako umeijenga kwa namna ya kuonesha wapinzani ndio wanaofanya iyo mikutano wakati kiuhalisia kwa miaka 6 tumeshuhudia chama tawala pekee ndio wanaofanya iyo mikutano. Ilitakiwa uwaoneshee kidole chama tawala sio wapinzani, Inaonesha wewe kero yako sio mikutano kwa ujumla kero yako ni vyama pinzani kupewa iyo nafasi ya kufanya mikutano. Mimi naona cha muhimu kusiwe na ubaguzi kama kukatazwa ikatazwe kwa wote kama kuruhusiwa iruhusiwe kwa wote
 
kwa hiyo hapa unadhani umekuja kuexpress hisia zako au kichangia mada ?

Mada ina pande mbili, sio lazima tuwe na hitimisho moja, maana hii sio hesabu ukisema 2+2 jibu lake lazima liwe 4. Labda useme hii mada ndio uhalisia na sio hisia zake.
 
Reactions: RNA
Jibu rahisi sana ni hili" kwa nini unafanya ngono wakati mkeo ana mimba au umeshapata watoto".

Kwa ufupi siasa ni fani kama zilivyo fani nyinginezo, hivyo wanasiasa wanaishi kwa kufanya siasa ndio maana kuna waajiriwa kwenye ngazi zote za ofisi za vyama. Ukisema wasubiri uchaguzi tu maana yake ajira hazina maana.

Pili Tanzania tunafuata mfumo wa siasa za ushindani(vyama vingi). Kazi ya vyama pinzani ni kutoa sera mbadala wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Hivyo mikutano hiyo kazi yake ni kukosoa ama kutoa suluhisho mbadala wa yale yanayotekelezwa au yanayotarajiwa kutekelezwa. Lengo kuu ni kuwa na jamii bora zaidi.

Mfano: 2015 vyama vya upinzani vilikuwa na sera ya elimu bure... baadae ikachukuliwa na upande wa pili lakini utkelezaji wake hajkuwa mzuri mapungufu yamekuwa yakisemwa na upinzani leo tunaona serikali inarekebisha.

Je wapinzani wangekuwa wanakaa kimya elimu ingekuwa bure? Je ingekuwa walau imeboreka kama ilipo sasa?
Ndio maana kunahitajika sana mikutano ya siasa mara kwa mara.

Kupinga kwao kusikukere bali iwe ndio chachu ya kuleta maendeleo endelevu kwa wote.

Mbu asipokupigia huwezijua wanaingikia wapi.

"Wacha mvua inyeshe tujue panapovuja" tusiilaani mvua bali tuzibe matundu
 
kwamba wewe ni mchapakazi kuliko wote
 
Wanachama wapya utawapata wakati wa uchaguzi pekee..!!??
 
Jiulize swali hili kuna faida Gani cccm kubaki mamlakani

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Taifa linakuwa kama binadamu au mmea kwahiyo kila uchao kuna mambo mapya, unadhani kwanini CCM wanafanya hiyo mikutano si watulie tu wafanye kazi zao kama ni kutueleza wanachofanya vyombo vya habari vipo watatutangazia.
Hapo sasa !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…