Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Sayansi na Teknolojia ni universal, ni uniform, kote duniani msingi ni ule ule.
Chanzo cha magonjwa mfano Malaria, Ukimwi, kipindupindu, ebola n.k ni kimoja duniani kote, causality yake ni ya aina moja na ni replicable.

Daktari au Injinia aliyesoma chuo bora anaweza kufanya kazi hiyo hiyo duniani kote. Uchawi tunaambiwa hata hauvuki maji.
 
Wenzetu waliwahi hadi kufanyia tafiti Remote viewing kwa zaidi ya miaka 20 kupitia jeshi lao na hiyo program waliita project stargate.
Kufanya utafiti wa kitu haimaanishi hicho kitu kipo, inamaanisha watu wanataka kujua ukweli wa jambo tu katika msingi wa kisayansi baada ya madai mbalimbali ya watu. Mfano kukiwa na kelele sana kuhusu rushwa au wizi wa pesa za umma, uchunguzi/utafiti utafanyika ili kubaini ukweli.

Jeshi la Marekani na Intelligence agencies wana projects au department za uchunguzi wa aliens, UFO, UAPs n.k

Again, Marekani mambo ya imani bado yana nafasi kiasi fulani tofauti na mataifa mengi ya Magharibi yalioendelea. US ndipo zilipoibuka dini unorthodox za Usabato(SDA), Jehovah Witness, Scientology- wanaoamini uwepo wa extraterrestrial civilizations na aliens pamoja na Mormons(LDS) ambao wanaamini Yesu alienda kuishi Marekani na Eden ilikuwa Marekani.

Kuna visa vya ajabu vya kila aina vya kidini/imani mfano Jonestown Massacre, Waco Massacre n.k

Mpaka mwaka 1878 kesi za uchawi zilikuwa zinapokelewa katika mahakama za Marekani wakati wazungu wa nchi nyingine walikuwa wameshaachana na huo ujinga kama miaka mia hivi nyuma.
 
Hakuna uchawi zaidi ya story za kusadikika zinazoaminiwa na watu wajinga wajinga. Ukitaka uthibitisho utapewa kila aina ya story except uthibitisho wenyewe.
 

Tatizo wote mnaopinga huwa mnatafuta nyufa za kutengeneza attacks.

Mnajaribu kuhalalisha kuwa "sijui ninachokiongelea"

Nimekaririshwa, nimeaminishwa na mimi nikaamini.

Ukiweza soma post zangu za nyuma

Actually nipo open minded. Naweza kuwa mkristu ila hainifanyi nisijue nguvu ya visomo na hata baadhi ya principles za uislamu. Na hata sababu ya kujiunga jf , ni kwa sababu nilivutiwa na ideas za atheist Kiranga

Pia naweza kuwa ni graduate lakini haimaanishi sijui vitu ambavyo kwa graduates ama wasomi wengi wanaviona kama vya kipuuzi kwenye jamii zao

Again, sijakuzwa sehemu moja,
Nimekuzwa kwa kuishi maeneo tifauti hii nchi kwa hiyo sikuwa programmed kufikiri navyofikiri. Kwa hiyo Nilichoamua kuamini ni kutokana na mambo nilioyaona na niliyoyathibitisha. Aidha kwa experience yangu binafsi ama ya watu wangu wa karibu.

Huwa nipo curious, na napotaka kujifunza, simfanyi mtu anaeniambia kitu ajihisi kuwa yeye ni mpumbavu. No

Nakaa chini na nijikuza au kujishusha kwa level itakayomfanya yeye kuwa comfortable..

Nikikuambia nishafuatilia hadi mizimu japo kwa sasa watu hawajali. Je, wewe umeshawahi fikiria hilo

Mimi nipo curious by nature, sio kwamba na_fake ili nionekane intelligent ama msomi. Na zamani nilikuwa Narendr kufuatilia history na nilikaa na wazee. Wanakusimulia vitu ambavyo hata havipo documented.

Na tabia ya kujifunza ni kuwa open kupokea unayoambiwa na kuyachuja ili uone ukweli na uongo ni upi .

Naamini katika spiritual world, naamini ipo, nimeshakutana nayo and unless uzame kwenye spiritual world kwa kufuata system na principles zake ambazo wewe huamini kama zipo. Huwezi kujua
 
😁😁
 
Some people they think they know But honestly they know Nothing

Kuna siku Moja nitakuja kudondosha Bonge la Uzi hapa JF nia na makusudio Nitataka watu wajifunze kupitia Mimi ili niweze kuwasaidia waache kuteseka siku hiyo Nitataka kabisa watu wakae na pen na karatasi kabisa kutake Notes

Sinto jali mishale nitakayo pigwa atakaye elewa na kuwa Tayari kujifunza ata jifunza ambaye hatokuwa Tayari shauri Zake abaki na ujinga wake
 
Ndio maana nasema ushahidi mnaodai nyie humu ni wa kisayansi na si vinginevyo ila mnanibishia.
 
Bila kuja na ushahidi wa kisayansi hakuna utakachoeleweka mkuu utapuuzwa kirahisi sana tu na kuonekana hauna elimu na kuamini sayansi.
 
Mkuu nadhani ni more about believes and rituals.
I think uchawi ni kitu ambacho kimekosa tafsiri sahihi so kwakuwa watu wameshindwa kuufanyia tafiti so ndio wakaupatia jina Hilo la uchawi

But apart from that uchawi Hauna nafasi kubwa sana katika jamii kama namna jamii ilivyo aminishwa , unakuta mtu akiumwa kichwa kidogo tu anahisi kuwa amerogwa

Wajua uchawi ni Aina ya agenda ambayo pia inatumika kipropaganda na Baadhi ya Makundi ya watu kwaajili ya watu hao kuwatawala watu wengine na kujitajirisha Kwa kupitia Watu hao , watu kama wachungaji waganga mashekhe and the likes ni wanufaika wakuu wa hizo propaganda ni kama namna ambavyo pia wanavyo nufaika Kwa kupitia propaganda za kidini,

Ila uchawi upo but Issue yake sio kubwa hivyo kama namna ambavyo inavyo aminishwa katika jamii

Sehemu kubwa iliyopo katika jamii ukiachana na matatizo yanayo changiwa na uhaba wa ufumbuzi wa kisayansi katika jamii husika na ukosefu wa kujitambua Kwa mtu mmoja Mmoja wanao Toka katika jamii hiyo husika

Pia matatizo mengine Yana sababishwa na Jamii kuwa Zina Asili ya mizimu na Majini , ( na hapo pia Kuna upigaji mkubwa sana wa pesa )

Kwasababu kile ambacho watu wame aminishwa kuhusu mizimu na Majini kipo tofauti kabisa na uhalisia wa viumbe hivyo jinsi ulivyo Watu wamedanganywa sana kuhusu hayo mambo Na kuaminishwa uongo kuhusu hivyo viumbe and kumbe the way ilivyo na vinavyo operate ni tofauti kabisa na watu walivyo Aminishwa

Na lengo kuu ni kuwaficha watu kuwanyima watu elimu ili baadhi ya watu Fulani wabaki kuwa ni wanufaika


Ipo siku Moja nitakuja kutoa hili darasa
 
Reactions: Lax
Bila kuja na ushahidi wa kisayansi hakuna utakachoeleweka mkuu utapuuzwa kirahisi sana tu na kuonekana hauna elimu na kuamini sayansi.
Katika maisha Wala tusijali kupuuzwa ,

Wajua ukiwa unaishi ndani ya ukweli na ukawa unaujua huo ukweli

Mtu mwingine akija kukubishia na kukupinga huwezi kukutetereka cause unajua kwamba ni ujinga tu ndio unao msumbua
 
Hakuna uchawi zaidi ya story za kusadikika zinazoaminiwa na watu wajinga wajinga. Ukitaka uthibitisho utapewa kila aina ya story except uthibitisho wenyewe.
Njoo inbox na majina yako 3 nitakuelezea kila jambo lako lililopita na lijalo
 
Kumbe yote hayo unayajua inaonekana umefanyia uchunguzi hayo mambo.

Ni ruksa kuuliza maswali kuhusu hiyo placebo effect ya kwa waganga ili kufahamu vizuri?
 
Naamini katika spiritual world, naamini ipo, nimeshakutana nayo and unless uzame kwenye spiritual world kwa kufuata system na principles zake ambazo wewe huamini kama zipo. Huwezi kujua
Mkuu kuamini tu sio ishu, mtu unaweza kuamini chochote, jambo la msingi je ni "fact".

Hitler na Nazi walikuwa wanaamini Aryan au Wajerumani ni master race, Wayahudi na Wakristo wengi wanaamini Wayahudi ni taifa teule(chosen people), Kuna wakati Wazungu na Waarabu walikuwa wanaamini sisi Waafrika sio binadamu kamili, Kuna kipindi watu walikuwa wanaamini jua linazunguka dunia hadi wakamuua Galileo aliposema Dunia ndio inazunguka jua, watu walikuwa wanaamini hewa chafu ya mvuke(miasma theory) ndio ilikuwa inasababisha magonjwa mbalimbali kama Malaria, homa, ukoma, kipindupindu n.k
 
Hili swala mi naamini lipo japo sijawai kulishuhudia.

Ila nahisi ni kua wachawi wa kweli ni wachache katika jamii, na kati yao kuna wanao utumia vibaya (kuroga na kuua watu bila hatia) na kuna wanao utumia vizuri kwa matumizi binafsi ikiwemo ulinzi wa mali na pengine kucheza faulo pia, nikimaanisha kuutumia katika mambo ya kiushindani.

Nahisi tu sina uhakika maana sifahamu. Karibu kunisahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…