Je, Kuna sheikh yoyote mwenye masters au phd kama ilivyo kwa maaskofu wengi?

Status
Not open for further replies.
Saalam!

Mimi binafsi sijawahi husikia kuna sheihk mwenye bachelor degree, masters au hata phd kama ilivyo upande wa maaskofu wa madhehebu mbalimbali.

Sasa pengine mimi ndiye sijui au niko nyuma ya wakati kama ambavyo nafahamu ya kuwa sijawahi kumsikia wala kumwona sheikh msomi kwa kiwango hicho! Sasa , elimu zinazotolewa na dini ni kulingana na wito wa dini ya kiislamu, au ni utamaduni wao kwamba hakuna haja ya kuwa na elimu nje ya maswala ya dini.?

Nb , uzi huu ni kwa ajili ya kujifunza zaidi
Mohammed dewj, said Salim bakhresa, Ally Awadh
Shekhar Kanabar
Shubash Patel, Ghalib Said Mohammed,Salim Turkey,Fida Hussein Rashid,

Plus alhaji aliko dangote

Hawa wana mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Africa

Tuache chuki na unafiki
 
PhD ya UBWABWA na VIPAPATIO

WENGINE HUMU TUNAKUJA KUPUMZIKA UKICHUKULIA KILA KITU SERIOUSLY UTATESEKA SANA. LEO NIMEANUA NITUMIE HUU MUDA KUCHOKOZA WATU HUMU NDANI PIA KUNA MUDA NAKUA NIPO VERY SERIOUS.

KAMA UNA WASIWASI NA PHD ANZISHA THREAD NTAKUJA KUUDHIBITISHIA UMMA
NTAKUWEKEA DETAILS ZOTEEE

KWA SASA EMBU CHUKUA MAJI UNYWE KWA WINGI..😊😅
Sawa sawa sheikh
 
Saalam!

Mimi binafsi sijawahi husikia kuna sheihk mwenye bachelor degree, masters au hata phd kama ilivyo upande wa maaskofu wa madhehebu mbalimbali.

Sasa pengine mimi ndiye sijui au niko nyuma ya wakati kama ambavyo nafahamu ya kuwa sijawahi kumsikia wala kumwona sheikh msomi kwa kiwango hicho! Sasa , elimu zinazotolewa na dini ni kulingana na wito wa dini ya kiislamu, au ni utamaduni wao kwamba hakuna haja ya kuwa na elimu nje ya maswala ya dini.?

Nb , uzi huu ni kwa ajili ya kujifunza zaidi
Masheikh zetu Wana elimu ya Dini tu pekee. Wapo waliosoma kwenye darsa duara za Misikitini na hii ndio asili na bora zaidi na wapo ambao wamesoma kwa nidhamu ya vyeti kwa maana ya diploma, degree, master's na PhD lakini vyote ni vya dini.

Kwenye nukta yako ya msingi ni kuwa sio lazima kusoma hizo elimu nje ya dini, ikitokea mtu ana elimu hiyo sio mbaya, lakini hai athiri chochote.
 
Nakupinga! Tena kwa asilimia kubwa sana mkuu, huko uarabuni pia ni watu wavivu kupindukia UAE, Oman wamejaza wataalamu kutoka mataifa ya nje hasa India inahudumia sana ukanda huo

Dubai yale majengo yote unayoyaona yamjengwa na wakandarasi wa kigeni kwa 80% sio vibarua, kazi za ndani nk. kote wanafanya kazi wageni

Lkn elimu ni ugunduzi huwezi kusoma na usiitumie elimu yako kufanya kitu, sasa unaweza kutuambia ni bidhaa ipi waarabu wana shindana na wazungu, ikiwa hata hiyo elimu yao yenyewe wanaipata ulaya na USA
Wana mafuta na gesi
 
Masheikh zetu Wana elimu ya Dini tu pekee. Wapo waliosoma kwenye darsa duara za Misikitini na hii ndio asili na bora zaidi na wapo ambao wamesoma kwa nidhamu ya vyeti kwa maana ya diploma, degree, master's na PhD lakini vyote ni vya dini.

Kwenye nukta yako ya msingi ni kuwa sio lazima kusoma hizo elimu nje ya dini, ikitokea mtu ana elimu hiyo sio mbaya, lakini hai athiri chochote.
Wapo masheikh wasomi na madaktari na wengine walimu hapa hapa Tanzania.
 
Waarabu wana elimu tofauti kabisa ,wana vyeo vyao kwa vile hawavai suti ila ni wasomi ...Nima ndugu wanaishi huko umeongea uwongo mtupu ,nikachosababisba waarabu kama Saudi na Qatar kushirikiana na wazungu ni mikataba hata jeddah tower itajengwa na kampuni ya Trump.

Kama umeelewa nilichoandika basi unajua kama utabisha nitakufundishwa uchumi jinsi ulivyo ..Kwa nn hata majengo ya USA wanaweza kujenga kampuni za china ,na kule china wanaweza kujenga USA japo kwa sasa kuna mgogoro ambao unaona athari kwa pande zote.

Kupeana tender ni makubaliano ya sera ya uchumi wa dunia ,kwani kuna ulazima Iphone kwenda kufanyiwa assembling China? Soma uchumi utanielewa .
Tuachane na majengo basi turudi hata kwenye ugunduzi, ukiachana na namba (0123456789) mwarabu kagundua nn? Wana elimu gani hiyo ambayo haina tija kwao na kwa dunia?

Ww una ndugu mm nimefanya kazi UAE wale jamaa ni wavuvu kupindukia niamini mimi, hata ratiba zao ukienda town kuanzia saa 12-saa 4 asubuhi hata idadi ya watu ni ndogo sana kule panaanza kuchangamka kuanzia saa 1 usiku, saa 2 asubuh kuna watu bado wamelala

Unavyoiona Zanzibar ndio hivyo hivyo wanaishi Waarabu
 
Wenzetu walijikita zaidi kwenye neno na kueneza neno , ila upande wa pili show zote zinapigika neno linapigwa na elimu ya Dunia wamo tena sio shule ya mchezo mchezo mtu unakuta ni Padre huku ni mwanasheria au Daktari tena daktari bingwa 😂😂 vitabu vinachezewa kotekote yani !!
Kwa namna hii ndio maana dini yenu imekuwa dhaifu sana, na haieleweki.
 
Uislam haupimwi kwa elimu ya Dunia Bali kwa kufuata uislam kamili, maadili yake na kujua Allah kaamrisha na anakataza nini, Ujue kusoma Qur aan na Elimu ya Dini kiujumla, PhD ni si kipimo kuwa huyo mwislamu kasoma Dini, hiyo itabaki hivyo,pia Uislam si Jina Bali Kufuata kikamilifu Wala hakuna swali utaulizwa je ulikuwa na PhD? Hakuna, PhD Yako ukifa ndo mwisho wake bila kujali umefaidika nayo ama la hiyo inakuwa imeisha, Mwislamu ni kushikamana na Uislam wake Wala si kuwa na PhD FAHAMU HIVYO.
Huu nao ni uvivu wa kujielimisha, waarabu wenyewe walioleta dini ni wasomi wazuri tu, kwa nini tung'ang'ane na elimu ya dini pekee tukaacha elimu zinazobadili maisha yetu ya kimwili?
 
Wapo masheikh wasomi na madaktari na wengine walimu hapa hapa Tanzania.
Itakuwa huijui elimu ya dini vizuri. Ili uwe msomi wa dini inabidi uache kazi ufanye kazi na utumie muda mwingi sana kwenye elimu.

Wewe mfano tu kwa afrika Mashariki yetu hii hakuna Mwanachuoni, hili si jambo dogo.
 
Tuachane na majengo basi turudi hata kwenye ugunduzi, ukiachana na namba (0123456789) mwarabu kagundua nn? Wana elimu gani hiyo ambayo haina tija kwao na kwa dunia?

Ww una ndugu mm nimefanya kazi UAE wale jamaa ni wavuvu kupindukia niamini mimi, hata ratiba zao ukienda town kuanzia saa 12-saa 4 asubuhi hata idadi ya watu ni ndogo sana kule panaanza kuchangamka kuanzia saa 1 usiku, saa 2 asubuh kuna watu bado wamelala

Unavyoiona Zanzibar ndio hivyo hivyo wanaishi Waarabu
Wangekua wavivu wasingekua na maendeleo kuzid nyinyi maniga msio wavivu
 
Tuachane na majengo basi turudi hata kwenye ugunduzi, ukiachana na namba (0123456789) mwarabu kagundua nn? Wana elimu gani hiyo ambayo haina tija kwao na kwa dunia?

Ww una ndugu mm nimefanya kazi UAE wale jamaa ni wavuvu kupindukia niamini mimi, hata ratiba zao ukienda town kuanzia saa 12-saa 4 asubuhi hata idadi ya watu ni ndogo sana kule panaanza kuchangamka kuanzia saa 1 usiku, saa 2 asubuh kuna watu bado wamelala

Unavyoiona Zanzibar ndio hivyo hivyo wanaishi Waarabu
Mbona unachanganya mada!?
Kugundua ama uvumbuzi na usomi ni wapi na wapi!?
Mleta mada anasemea kuhusu LITERACY RATE SIO KUHUSU INVENTION AND INNOVATION.
Kuhusu LITERACY RATE waarabu wanasoma na wanapenda kusoma na Kuna hadi vyuo vipo rank ya Dunia uarabuni ikiwemo vyuo vya Saudi Arabia.
Unaonekana unaropoka huongei.
Mwaarabu kuwa mvivu haimaanishi sio msomi.
 
Tuachane na majengo basi turudi hata kwenye ugunduzi, ukiachana na namba (0123456789) mwarabu kagundua nn? Wana elimu gani hiyo ambayo haina tija kwao na kwa dunia?

Ww una ndugu mm nimefanya kazi UAE wale jamaa ni wavuvu kupindukia niamini mimi, hata ratiba zao ukienda town kuanzia saa 12-saa 4 asubuhi hata idadi ya watu ni ndogo sana kule panaanza kuchangamka kuanzia saa 1 usiku, saa 2 asubuh kuna watu bado wamelala

Unavyoiona Zanzibar ndio hivyo hivyo wanaishi Waarabu
Mwarabu amegundua ndege kabla ya kina weight brother,robot ,mambo ya navigation kwenda mbali kwa kutumia compass bearing ,ndio wafanyabiashara wakubwa hata kugundua mabara mengine ,mwarabu amegundua hesabu zinafanya kazi kwenye mifumo yote ya computer ... Mwarabu alikuwa mbele kwenye architectural.

Kihistoria wazungu ni washamba wa juzi tu ,kama unavyoona mikoa ya bara... Waarabu walishaendelea muda sana na wana historia kubwa .Hayo ni machache.
 
Itakuwa huijui elimu ya dini vizuri. Ili uwe msomi wa dini inabidi uache kazi ufanye kazi na utumie muda mwingi sana kwenye elimu.

Wewe mfano tu kwa afrika Mashariki yetu hii hakuna Mwanachuoni, hili si jambo dogo.
Una fikra finyu sana kijana kuhusu elimu ya dini mkuu.
Kuna uwezekano wa kusoma elimu ya dini na ya secular kwa wakati mmoja.
Huyo Ahmad Rusaganya amesoma tarekh,usual,balagha na korokoro zote huku akisoma na secular.
Alienda hadi Jordan kusoma kama ilikua hujui.
 
Huu nao ni uvivu wa kujielimisha, waarabu wenyewe walioleta dini ni wasomi wazuri tu, kwa nini tung'ang'ane na elimu ya dini pekee tukaacha elimu zinazobadili maisha yetu ya kimwili?
Inaonekana wewe unamfuata waarabu endelea kuwafuata imetatajwa Dini na PhD wewe huijui dini inavyoonekana kama huyo aliyeleta nada eti mashekh walingane kwa PhD na maaskofu, Wapi ukiona Haqi na Baatwil Vinalinganishwa?
 
Itakuwa huijui elimu ya dini vizuri. Ili uwe msomi wa dini inabidi uache kazi ufanye kazi na utumie muda mwingi sana kwenye elimu.

Wewe mfano tu kwa afrika Mashariki yetu hii hakuna Mwanachuoni, hili si jambo dogo.
Waeleweshe hawaelewi, wanataka kulinganisha na Baatwil, Dini ya Haqi na Dini ya Msosi wapi na wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom