Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

40 kwa mwezi anko....
Gas kwa mwezi ni 50000
Maji 50000 (hapa nimepunguza)
Umeme 30000

Nyingine najaziaje
hapo unazungumzia familia zaidi ya watu sita lakini ya watu wawili na watoto wawili mtungi unapiga miezi miwili maji unalipa buku tano
umeme buku tano huyu kapanga chumba kimoja
 
Attachments

Mshahara wangu ni sh 220,498.16/= Ila Nina mke mmoja na watoto wawili wa kiume na hapa naandika hii comment nimetoka kununua kilo moja ya nyama kwa sh 5000/= ,nimejenga kajumba ka 2 rooms na sebule,sijawahi lala njaa.

Ukubwa wa mshahara sio kipimo Cha maendeleo Bali ni mipango tu mkuu,pambana utatoka
 
Mmh Hornet feb to june....au unapikia ile mitungi XXXL😁
Mi kila mwezi nanunua gas hiyo ni lazima,
hata mimi gas mkaa tupa kule japo huku mkaa ni bei rahisi ila kunawatu wakizoeshwa mkaa itasumbua kwa gharama natumia mtungi wa 15 mwezi mmoja na nusu kila kitu yakiwemo maji ya kuoga
 
310,000 mbona inatosha japo ni ngumu kufanya saving,kodi ya chumba na sebule medium quality 60000,umeme na maji 10000,chakula unasaga debe 2 za unga kila debe maximum 15000x2 ni 30000,maharage kilo 5x2000 ni 10000,mchele kilo 20x1200 ni 24000,mafuta Lita 5 ni 25000,mkaa nunua gunia moja 50000,gesi 25000 JUMLA NI 234000 hivyo ukiitoa kwenye 310000 itabaki 76000,suala la afya kata bima ya familia 54000 kwa mwaka,itabaki 22000 hii ya kubadilishia mboga kwa mwezi.Nauli kazini itabidi uwe mdau wa tz 11,suala la mavazi ni anasa,chai asubuhi ni anasa,king'amuzi ni anasa,bia ni anasa,kuhonga ni anasa, kutoa sadaka Mungu ndio anajua hali yako atakusamehe,YAANI KIFUPI UTAISHI KAMA SHETANI au nasema uongo ndugu zangu
 
hapo unazungumzia familia zaidi ya watu sita lakini ya watu wawili na watoto wawili mtungi unapiga miezi miwili maji unalipa buku tano
umeme buku tano huyu kapanga chumba kimoja
Khaaaaaaa anko maji buku tano mwezi? Labda zile nyumba za wapangaji wengi bill inagawanywa
 
nimerudi!
  1. cha kwanza mwenye kipato hicho anastahili kuwa na familia ndogo yenye mke na watoto wawili
  2. mara nyingi inatokea mama huwa ni wa nyumbani hivyo anaweza kufundishwa kufunga japo karanga na kutengeneza visheti
  3. ijulikane wazi chanzo cha mapato ni pamoja na mshahara si mshahara pekee fungua
 
Attachments

310,000 mbona inatosha japo ni ngumu kufanya saving,kodi ya chumba na sebule medium quality 60000,umeme na maji 10000,chakula unasaga debe 2 za unga kila debe maximum 15000x2 ni 30000,maharage kilo 5x2000 ni 10000,mchele kilo 20x1200 ni 24000,mafuta Lita 5 ni 25000,mkaa nunua gunia moja 50000,gesi 25000 JUMLA NI 234000 hivyo ukiitoa kwenye 310000 itabaki 76000,suala la afya kata bima ya familia 54000 kwa mwaka,itabaki 22000 hii ya kubadilishia mboga kwa mwezi.Nauli kazini itabidi uwe mdau wa tz 11,suala la mavazi ni anasa,chai asubuhi ni anasa,king'amuzi ni anasa,bia ni anasa,kuhonga ni anasa, kutoa sadaka Mungu ndio anajua hali yako atakusamehe,YAANI KIFUPI UTAISHI KAMA SHETANI au nasema uongo ndugu zangu
Bonge la ushauri
 
inawezekana ila nina watu nafahamu wanalipwa 180,000 kazini anaingia saa 1 asubuhi anatoka saa 12 jion
hapo anaweza kufanya chochote kweli?
kazi za viwandani
Kuna mzazi mmoja alikua analipwa mshahara 180,000 na inatosha majukumu ya kifamilia yote pamoja na kusomesha shule na chakula!
 
Khaaaaaaa anko maji buku tano mwezi? Labda zile nyumba za wapangaji wengi bill inagawanywa
kwangu natumia kiasi hicho ndo bili ninayolipa ila nimekuwa mpare kidogo
kwanza marufuku kutumia maji kabla hayajakingwa
vyombo havioshi na maji ya moja kwa moja bombani kwa kuwa kawaida yenu glass imetumika kwa kumpa mgeni mara moja lakini inaweza kuoshwa kwa glass tatu utaratibu huu wengi niliowafundisha wamepunguza gharama kwa zaidi ya 50% pia unapofungua maji fungua yatoke taratibu ili usiruhusu upepo uingie katika bill ya maji upo hapo
 
Back
Top Bottom