Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

MIMI ninaishi nao huo

Mke, mtoto na mimi tutakula 200,000 kwa mwezi

Mke na mtoto wana bima za afya kwa mwaka ambazo ninalipia 170000 (jumla kwa mwaka)

Mama kila mwezi ninamrushia 40,000

Pocket money yangu 30,000 kwa mwezi

Chumba nimepanga cha 35,000 ninatumia sola

Inayobaki ninasevu. Ila usiiige mkuu, ninaishi kiugumu sana hapo katikati lakini sijawahi kushindwa kabisa, sokoni nenda mwenyewe, na usipendelee kusafiri kwa daladala labda iwe lazima sana
 
Mmh Hornet feb to june....au unapikia ile mitungi XXXL😁
Mi kila mwezi nanunua gas hiyo ni lazima,
yaah natumia hiyo ya 46,000-50,000

niliwahi kununua gas tarehe mbili nov ikaisha tar 2 december
nililalamika nikamuhama na huyo muuzaji
kwangu inakaa mpaka miezi sita

vya kuchemsha vinaingia kwenye mult cooker vya kukaanga kwenye ges
 
inabidi utufundishe mbinu
 
Basi kipato kinawezekana kulingana na sehemu na sehemu, mi kwangu maji ya elf 5 ni ya siku tatu.
 
unasafiri kwa nini?
kuna fundi alikuja kwangu akaniambia anatembea mpaka Kawe kwa mguu

aisee ilibidi nimwongeze nauli japo sijui kama alipanda hiyo daladala
 
yaah natumia hiyo ya 46,000-50,000

niliwahi kununua gas tarehe mbili nov ikaisha tar 2 december
nililalamika nikamuhama na huyo muuzaji
kwangu inakaa mpaka miezi sita

vya kuchemsha vinaingia kwenye mult cooker vya kukaanga kwenye ges
Unapoenda kununua gas hakikisha unaipima uzito unapata kamili kulingana Na size ya mtungi wako
 
yaah natumia hiyo ya 46,000-50,000

niliwahi kununua gas tarehe mbili nov ikaisha tar 2 december
nililalamika nikamuhama na huyo muuzaji
kwangu inakaa mpaka miezi sita

vya kuchemsha vinaingia kwenye mult cooker vya kukaanga kwenye ges
Labda nami nijaribu kuswitch kwenye multcooker nimejaribu kupikia maharage dk 45 umeme hata unit 1 haikuisha
 
utakuwa msabato wewe hata soda hunywi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…