Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Kwahiyo kwa mfano kuamini Mungu ni kutarajia kwamba huyo Mungu atatokea in future ila sasa hayupo? Vp na mfano mtu kuamini karogwa hapo kipi hapo kinatarajiwa?

Maelezo yako kuhusu kujua kwa kudhani yanaonyesha ni sawa na kitu ambacho moja kwa moja si cha kweli.
 
Kwa hiyo Kwa wewe Sayansi haikosolewi!!?
 
Hoja yangu niliijenga kuzungumzia kupinga ujumla wa tafiti zote za Sayansi na ndio maana utaona huko awali nilitoa maelezo kuwa Sayansi inaruhusu kukosolewa.

Kupinga tafiti za kisayansi at single particular research sio sawa na kupinga Sayansi in general.
 
Nani wakuamua kuwa misingi ya uhakiki wa dini ni lazima ifuate vitu hivyo ulivyovitaja?
 
It makes senses,Ifike hatua watu wajikite kwenye kujua na kutafuta sababu(Rational Thinking) na kuachana na kuamini.

Imani zimekaa kama propaganda au manipulation flan ivi.
 
Aliyeweka kumjua si muhimu. Tunajadili hoja hatujadili mtu.

Wikipedia ina njia zake za ku verify taarifa na ndio maana kuna link za external sources ambazo unaweza kuzitumia kuhakiki taarifa kama legit.

Link hii hapa

Kuhusu Makavel kuwa na miungu mingi halafu wao wakiamini kwenye hiyo miungu yao hakuna Mungu muumba kwasababu waliamini Mungu mkuu ni yule ambaye ameumba mbingu na nchi ambaye sio miongoni mwa miungu yao.

Haina maana kwamba na dini zingine zenye kuamini Mungu zaidi ya mmoja nazo ziwe na mtizamo huo.

The fact kwamba kuna dini inaabudu miungu zaidi ya mmoja ambao hakuna Mungu muumba, haiwezi kuwa sheria ya kufanya dini zingine zinazoamini Mungu zaidi ya mmoja nazo zisiwe na Mungu anayehusika na uumbaji.
 
Kitu ambacho naweza kuwa na uhakika nacho mpaka sasa ni kuwa unajaribu kuibua mjadala katikati ya mjadala ili uonekane maswali yako hujajibiwa upate sababu ya kukwepa hoja ya kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Kwa kulijua hilo na kwa faida ya wasomaji nataka twende hivyo hivyo unavyotaka wewe kwasababu haitokuwa busara kukushinikiza ujibu hoja ambayo inaonekana kuwa ni kubwa kwako.

Kwa hiyo tutaenda kwa mfumo huo huo unaoutaka wewe.
 
Nimeyatoa kwenye tafsiri ya hili neno la Polytheism

Polytheism ni imani ya kuabudu miungu zaidi ya mmoja. Katika dini za kipolytheism, kuna miungu mingi, kila mmoja akiwa na majukumu na sifa zake maalum. Dini nyingi za kale, kama vile za Wagiriki, Warumi, na Wahindu, zina miungu mingi inayosimamia nyanja tofauti za maisha na asili.

Kwa mfano, katika dini ya Kihindu, kuna miungu kama Brahma (mungu wa uumbaji), Vishnu (mungu wa ulinzi), na Shiva (mungu wa uharibifu). Kila mungu ana jukumu lake maalum na huabudiwa kwa njia tofauti.
 
Kwahiyo kwa mfano kuamini Mungu ni kutarajia kwamba huyo Mungu atatokea in future ila sasa hayupo?
Mungu hawezi kutokea in future kwa sababu imani yenu haisemi hivyo. Imani yenu ina waaminisha Mungu tayari yupo, ilhali kiuhalisia hayupo.
Vp na mfano mtu kuamini karogwa hapo kipi hapo kinatarajiwa?
Kurogwa ni jambo lisilo na uthibitisho.
Maelezo yako kuhusu kujua kwa kudhani yanaonyesha ni sawa na kitu ambacho moja kwa moja si cha kweli.
Si cha kweli kwa sababu bado huna uhakika wa hicho unacho kidhania kama ni kweli.

Ukishapata uhakika na uthibitisho wa hicho unacho kijua kwa kudhani, Basi kinakuwa ukweli.

Hukidhanii tena. Bali unajua kwa ukweli uliyo na uhakika, ushahidi na uthibitisho.
 
Ndio maana nakwaambia unaichukulia sayansi kama dubwashwa fulani hivi, sikulaumu sana kwa sababu siku hizi sayansi imefanywa kuwa imani fulani ya dini yani watu hupinga kitu kisa tu hakina ushahidi au maelezo ya kisayansi.
 
Hayo ni maneno ya waliokosa kutetea hoja ya uwepo wa Mungu. Wenye uhakika na uwepo wake hatu kauli za kinyonge kama hizo.
 
Ndio maana nakwaambia unaichukulia sayansi kama dubwashwa fulani hivi, sikulaumu sana kwa sababu siku hizi sayansi imefanywa kuwa imani fulani ya dini yani watu hupinga kitu kisa tu hakina ushahidi au maelezo ya kisayansi.
Na ndio maana nakuambia hizi inferiority zako huwenda ni matokeo ya makuzi yako uliyokuzwa ukiaminishwa kuwa elimu ya madrasa pekee ndio msingi mzima wa maisha ya binadamu.
 
Mimi nimetumia tafsiri yako ulipoelezea maana ya imani ndio nimeuliza kama kuamini ni kutarajia kitu kutokea in future je imani ya kuamini Mungu hapo inakuaje? Au kuamini Mungu sio imani? Maana ni wewe ndio umefanya imani inahusu wakati ujao tu haihusu wakati uliyopo au uliyopita.

Ndio kurogwa hakuna uthibitisho ndio maana ni jambo la imani ama si hivyo?

Uthibitisho haufanyi kitu ndio kiwepo au kiwe cha kweli, kwa sababu huko kujua kwa kudhani kuhusu wazazi wako inaweza kuwa ndio kweli wazazi wako hata kama hauna uhakika wala uthibitisho wakati huo.
 
Na ndio maana nakuambia hizi inferiority zako huwenda ni matokeo ya makuzi yako uliyokuzwa ukiaminishwa kuwa elimu ya madrasa pekee ndio msingi mzima wa maisha ya binadamu.
Unarudia tena kuona kuwa mie napinga sayansi.
 
Mimi nimetumia tafsiri yako ulipoelezea maana ya imani ndio nimeuliza kama kuamini ni kutarajia kitu kutokea in future
Imani ni kwa kitu chochote.
je imani ya kuamini Mungu hapo inakuaje? Au kuamini Mungu sio imani?
Kwa muktadha wa imani za kidini. Ninyi mna amini tayari kuna Mungu ila hamna uthibitisho wala uhakika.

Na hapa ndio utata unaanza.

Mnaamini kwamba Mungu yupo, ila kumthibitisha hamuwezi. Sasa huoni kwamba hayupo?

Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Kila mtu angejua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho kabisa kwamba kuna Mungu.
Maana ni wewe ndio umefanya imani inahusu wakati ujao tu haihusu wakati uliyopo au uliyopita..
Kulingana na maandiko yenu ya kidini. Mnatafsiri imani kama kuwa na uhakika wa jambo, kumbe kiuhalisia sio tafsiri sahihi.

Imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho.
Ndio kurogwa hakuna uthibitisho ndio maana ni jambo la imani ama si hivyo?
Ndio
Uthibitisho haufanyi kitu ndio kiwepo au kiwe cha kweli, kwa sababu huko kujua kwa kudhani kuhusu wazazi wako inaweza kuwa ndio kweli wazazi wako hata kama hauna uhakika wala uthibitisho wakati huo.
Lakini huwezi kujua mpaka ufanye uhakiki upate uhakika wa either hao ni wazazi wako kweli, Au sio wazazi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…