Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Kwahiyo kwa mfano kuamini Mungu ni kutarajia kwamba huyo Mungu atatokea in future ila sasa hayupo? Vp na mfano mtu kuamini karogwa hapo kipi hapo kinatarajiwa?Imani ni kwa jambo ambalo linatarajiwa kuwepo/kutokea in future
(Yani bado halijatokea)au halipo kabisa. Au kitu ambacho kinatarajiwa kuwepo/kutokea in the future au hakipo.
Mfano mwanafunzi akifanya mtihani anakuwa na imani kwamba atafaulu, kwa sababu bado ufaulu kwake haujatokea.(Ufaulu wake upo in future). Anaweza asifaulu vilevile, Akafeli.
kwa vile alikuwa na imani tu kwa jambo la "kufaulu" ni jambo ambalo lipo in future au linaweza lisiwepo, Akafeli.
Kujua kwa kudhani, Ni kwa jambo ambalo tayari lipo, Au kitu ambacho tayari kipo kweli kwenye uhalisia. Sema wewe ndio huna taarifa sahihi za uwepo wake.
Mfano una wazazi wako. Na wewe unaweza kujua kwa kudhani kwamba kweli hao ni wazazi, Kumbe inawezekana kiuhalisia hao sio wazazi wako. Kwa vile huna uthibitisho na taarifa sahihi za kuhakikisha kweli hao ni wazazi wako.
Lakini hata kama hao wazazi kiukweli sio wazazi wako, Bado wazazi wako wa asili waliokuzaa lazima wapo au walikuwepo ndio maana ulizaliwa. Sema huna taarifa sahihi za kuhakikisha uwepo wao.
Unabaki kujua kwa kudhani tu hao wasio wazazi, Ni wazazi wako. Kumbe sio.
Kiuhalisia una wazazi wako wa asili ambao bado huna taarifa sahihi, bado huja hakikisha na kuthibitisha uwepo wao.
Maelezo yako kuhusu kujua kwa kudhani yanaonyesha ni sawa na kitu ambacho moja kwa moja si cha kweli.