Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Imani ni kwa jambo ambalo linatarajiwa kuwepo/kutokea in future
(Yani bado halijatokea)au halipo kabisa. Au kitu ambacho kinatarajiwa kuwepo/kutokea in the future au hakipo.

Mfano mwanafunzi akifanya mtihani anakuwa na imani kwamba atafaulu, kwa sababu bado ufaulu kwake haujatokea.(Ufaulu wake upo in future). Anaweza asifaulu vilevile, Akafeli.

kwa vile alikuwa na imani tu kwa jambo la "kufaulu" ni jambo ambalo lipo in future au linaweza lisiwepo, Akafeli.

Kujua kwa kudhani, Ni kwa jambo ambalo tayari lipo, Au kitu ambacho tayari kipo kweli kwenye uhalisia. Sema wewe ndio huna taarifa sahihi za uwepo wake.

Mfano una wazazi wako. Na wewe unaweza kujua kwa kudhani kwamba kweli hao ni wazazi, Kumbe inawezekana kiuhalisia hao sio wazazi wako. Kwa vile huna uthibitisho na taarifa sahihi za kuhakikisha kweli hao ni wazazi wako.

Lakini hata kama hao wazazi kiukweli sio wazazi wako, Bado wazazi wako wa asili waliokuzaa lazima wapo au walikuwepo ndio maana ulizaliwa. Sema huna taarifa sahihi za kuhakikisha uwepo wao.

Unabaki kujua kwa kudhani tu hao wasio wazazi, Ni wazazi wako. Kumbe sio.

Kiuhalisia una wazazi wako wa asili ambao bado huna taarifa sahihi, bado huja hakikisha na kuthibitisha uwepo wao.
Kwahiyo kwa mfano kuamini Mungu ni kutarajia kwamba huyo Mungu atatokea in future ila sasa hayupo? Vp na mfano mtu kuamini karogwa hapo kipi hapo kinatarajiwa?

Maelezo yako kuhusu kujua kwa kudhani yanaonyesha ni sawa na kitu ambacho moja kwa moja si cha kweli.
 
Duh! We jamaa naona hatuelewani kabisa una tatizo la kushindwa kuelewa unachosoma.

Nachokupinga ni hizo kauliza za kusema sayansi inakubali kukosolewa mara sayansi inasema, unafanya sayansi ni kama mtu hivi kitu ambacho naona unakosea kuelezea hivyo. Mimi sipingi sayansi wala kuidharau sayansi.
Kwa hiyo Kwa wewe Sayansi haikosolewi!!?
 
Msemo wa sayansi imesema..... unatumika sana na watu hufanya hivyo kupata urahisi wa kuelezea hivyo sio ajabu ila shida yako ni mtazamo wako kuhusu sayansi.

Angalia sentensi yako ya kwanza kwamba unaposema ukipinga tafiti ya sayansi ndio umeipinga sayansi, kuna tafiti ngapi za sayansi ambazo sio sahihi zinapingwa leo hii ukiniambia ukipinga tafiti ndio umepinga sayansi unanishangaza inaonyesha jinsi gani una mtazamo usio sahihi kuhusu sayansi.
Hoja yangu niliijenga kuzungumzia kupinga ujumla wa tafiti zote za Sayansi na ndio maana utaona huko awali nilitoa maelezo kuwa Sayansi inaruhusu kukosolewa.

Kupinga tafiti za kisayansi at single particular research sio sawa na kupinga Sayansi in general.
 
Sababu kila mtu anaona dini yake ni sahihi, ndio maana tunakuja au kinakuwa na hatua ya kuzihakiki dini husika.

Msingi wa kwanza lazima dini ya kweli iendane na maumbile, hili nimelitaja huko awali.

Pili, lazima tuangalie historia na na chimbuko la dini husika.

Tatu, lazima tuangalie ilikuwaje ikawepo na ilianzishwaje na marejeo ya maandiko yake ni wapi.

Labda nikuulize swali rahisi maana naona unakimbia hoja. Wewe unatumia njia gani kuhakiki habari au unaokoteza okoteza ?
Nani wakuamua kuwa misingi ya uhakiki wa dini ni lazima ifuate vitu hivyo ulivyovitaja?
 
Wanasema Mungu ni roho yupo kila sehemu ila haonekani kwasababu hana mwili.

Ila ukumbuke huyo huyo Mungu anayetajwa kuwa hana mwili ana jinsia ya kiume na ukifanya mocking kwa kumuita mwanamke utakumbana na ghadhabu za waumini kuwa umemdhalilisha Mungu wao.

Huyo huyo Mungu ambaye hana material body ana makazi yake huko juu yanaitwa Mbinguni, and just in case ukumbuke kuwa huko juu sio kama amesimama wima hapana maandiko yanasema ameketi kwenye kiti cha enzi kwa ajili ya kutu-monitor sisi. That means he's got a butt too.

But when it comes to evidence he disappears like poof.
It makes senses,Ifike hatua watu wajikite kwenye kujua na kutafuta sababu(Rational Thinking) na kuachana na kuamini.

Imani zimekaa kama propaganda au manipulation flan ivi.
 
Hili tatizo lingine, ulichokiweka bado kinahitaji marejeo, inabidi usome pia namna ya kurejea na kunukuu jambo.

Hapa nakuuliza tena, huyu aliweka haya huku Wikipedia marejeo yake ni wapi ?

Kingine hoja ya dini nyingine kukubali kuwepo kwa miungu msingi, nimeielezea huko juu kwa kuashiria mfano wa makafiri wa Makkah, Hawa walikuwa Wana miungu 360 na kila Mungu alikuwa na jukumu lake, lakini walikuwa wanajua na kuamini ya kuwa Mungu Mkuu ni yule ambaye ameumbwa mbingu na ardhi na ndio muendesha mambo na ndio anayepaswa kuabudiwa, lakini katika ibada zao walikuwa Wana waabudu hao miungu wao.
Aliyeweka kumjua si muhimu. Tunajadili hoja hatujadili mtu.

Wikipedia ina njia zake za ku verify taarifa na ndio maana kuna link za external sources ambazo unaweza kuzitumia kuhakiki taarifa kama legit.

Link hii hapa

Kuhusu Makavel kuwa na miungu mingi halafu wao wakiamini kwenye hiyo miungu yao hakuna Mungu muumba kwasababu waliamini Mungu mkuu ni yule ambaye ameumba mbingu na nchi ambaye sio miongoni mwa miungu yao.

Haina maana kwamba na dini zingine zenye kuamini Mungu zaidi ya mmoja nazo ziwe na mtizamo huo.

The fact kwamba kuna dini inaabudu miungu zaidi ya mmoja ambao hakuna Mungu muumba, haiwezi kuwa sheria ya kufanya dini zingine zinazoamini Mungu zaidi ya mmoja nazo zisiwe na Mungu anayehusika na uumbaji.
 
Mpaka tunafikia hapa ni wewe kutokujibu hoja zangu. Hii inaondoa maana ya mjadala.

Msingi wangu Mimi ni lazima tujue ukweli wa kila tubalo lijadili ili isiwe tunapoteza muda. Huwezi kujengea hoja mambo ambayo huyajui na huna elimu nayo.

Suala la uthibitisho juu ya uwepo wa Mungu, tumeshathibitisha sana na hili ni rahisi sana kwetu. Shida inakuja kwenu ambao hamna na hamtoweza kuja kuthibitisha ya kuwa hakuna Mungu. Sababu akili iliyo salimika haikatai hilo. Kwahiyo hili ni jambo dogo sana kwetu.
Kitu ambacho naweza kuwa na uhakika nacho mpaka sasa ni kuwa unajaribu kuibua mjadala katikati ya mjadala ili uonekane maswali yako hujajibiwa upate sababu ya kukwepa hoja ya kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Kwa kulijua hilo na kwa faida ya wasomaji nataka twende hivyo hivyo unavyotaka wewe kwasababu haitokuwa busara kukushinikiza ujibu hoja ambayo inaonekana kuwa ni kubwa kwako.

Kwa hiyo tutaenda kwa mfumo huo huo unaoutaka wewe.
 
Huu ni utoto mwingine, maana kitu kinachojulikana ni rahisi kukiletea marejeo, au wewe umeyaota haya ? Inakuwaje tunapoteza muda kwenye hakuna ?

Wewe weka umeyaota wapi ? Tatizo la kujibu maswali mnayo ulizwa kunawafanya mzidi kuonekana ni madhaifu sana.
Nimeyatoa kwenye tafsiri ya hili neno la Polytheism

Polytheism ni imani ya kuabudu miungu zaidi ya mmoja. Katika dini za kipolytheism, kuna miungu mingi, kila mmoja akiwa na majukumu na sifa zake maalum. Dini nyingi za kale, kama vile za Wagiriki, Warumi, na Wahindu, zina miungu mingi inayosimamia nyanja tofauti za maisha na asili.

Kwa mfano, katika dini ya Kihindu, kuna miungu kama Brahma (mungu wa uumbaji), Vishnu (mungu wa ulinzi), na Shiva (mungu wa uharibifu). Kila mungu ana jukumu lake maalum na huabudiwa kwa njia tofauti.
 
Kwahiyo kwa mfano kuamini Mungu ni kutarajia kwamba huyo Mungu atatokea in future ila sasa hayupo?
Mungu hawezi kutokea in future kwa sababu imani yenu haisemi hivyo. Imani yenu ina waaminisha Mungu tayari yupo, ilhali kiuhalisia hayupo.
Vp na mfano mtu kuamini karogwa hapo kipi hapo kinatarajiwa?
Kurogwa ni jambo lisilo na uthibitisho.
Maelezo yako kuhusu kujua kwa kudhani yanaonyesha ni sawa na kitu ambacho moja kwa moja si cha kweli.
Si cha kweli kwa sababu bado huna uhakika wa hicho unacho kidhania kama ni kweli.

Ukishapata uhakika na uthibitisho wa hicho unacho kijua kwa kudhani, Basi kinakuwa ukweli.

Hukidhanii tena. Bali unajua kwa ukweli uliyo na uhakika, ushahidi na uthibitisho.
 
Hoja yangu niliijenga kuzungumzia kupinga ujumla wa tafiti zote za Sayansi na ndio maana utaona huko awali nilitoa maelezo kuwa Sayansi inaruhusu kukosolewa.

Kupinga tafiti za kisayansi at single particular research sio sawa na kupinga Sayansi in general.
Ndio maana nakwaambia unaichukulia sayansi kama dubwashwa fulani hivi, sikulaumu sana kwa sababu siku hizi sayansi imefanywa kuwa imani fulani ya dini yani watu hupinga kitu kisa tu hakina ushahidi au maelezo ya kisayansi.
 
Makala hii nitaiweka kwa vipande kuepusha kero ya usomaji.

Moja ya hoja maarufu kutoka kwa watu wanaoamini Mungu (Theists).

Ni hoja ambayo imelenga kuweka matumaini ya mwelekeo katika maisha ili kuwafanya watu waone kuamini Mungu yupo ndio uchaguzi bora zaidi (rational) kwasababu haitakupa matokeo mabaya mwishoni.

Hii ni Analogy iliyopata sana umaarufu miaka ya 1640s na muazilishi aitwaye Pascal Wager.

Huyu jamaa alihoji kuwa ni vyema ukaamini kuwa Mungu yupo ukafa na usimkute kuliko kutokuamini halafu ukafa ukamkuta.

Pascal analaani kuwa kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi kuliko kutokuamini kuwepo kwake, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake. Hii ni kwasababu zifuatazo.

  1. Kama Mungu yupo na tutamwabudu, tutapata thawabu ya milele (kama ushindi mkubwa).
  2. Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (kama hasara ndogo).
  3. Kwa upande mwingine, kama Mungu yupo na hatumwamini, tutapata adhabu ya milele (hasara kubwa).
  4. Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (ushindi mdogo).

Hivyo, Pascal anasema kwamba kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi, kwasababu unaweza kupata thawabu ya milele na kuepuka adhabu ya milele, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake.

Swali: Je Atheists hawatuogopi siku ya mwisho kukutana na hukumu ya Mungu na kutupwa kwenye moto wa milele?

Hatuogopi kubaini kuwa hadithi za mitume zinazosimuliwa kuhusu Yesu na Muhammad kuwa ni za kweli na kwamba tumepoteza nafasi ya kuishi maisha ya milele peponi kwa kutoamini?

Je isingekuwa vyema Atheists kuwa upande salama wa kumuamini Yesu, Muhammad na Mungu kama backup just in case?
Hayo ni maneno ya waliokosa kutetea hoja ya uwepo wa Mungu. Wenye uhakika na uwepo wake hatu kauli za kinyonge kama hizo.
 
Ndio maana nakwaambia unaichukulia sayansi kama dubwashwa fulani hivi, sikulaumu sana kwa sababu siku hizi sayansi imefanywa kuwa imani fulani ya dini yani watu hupinga kitu kisa tu hakina ushahidi au maelezo ya kisayansi.
Na ndio maana nakuambia hizi inferiority zako huwenda ni matokeo ya makuzi yako uliyokuzwa ukiaminishwa kuwa elimu ya madrasa pekee ndio msingi mzima wa maisha ya binadamu.
 
Mungu hawezi kutokea in future kwa sababu imani yenu haisemi hivyo. Imani yenu ina waaminisha Mungu tayari yupo, ilhali kiuhalisia hayupo.

Kurogwa ni jambo lisilo na uthibitisho.

Si cha kweli kwa sababu bado huna uhakika wa hicho unacho kidhania kama ni kweli.

Ukishapata uhakika na uthibitisho wa hicho unacho kijua kwa kudhani, Basi kinakuwa ukweli.

Hukidhanii tena. Bali unajua kwa ukweli uliyo na uhakika, ushahidi na uthibitisho.
Mimi nimetumia tafsiri yako ulipoelezea maana ya imani ndio nimeuliza kama kuamini ni kutarajia kitu kutokea in future je imani ya kuamini Mungu hapo inakuaje? Au kuamini Mungu sio imani? Maana ni wewe ndio umefanya imani inahusu wakati ujao tu haihusu wakati uliyopo au uliyopita.

Ndio kurogwa hakuna uthibitisho ndio maana ni jambo la imani ama si hivyo?

Uthibitisho haufanyi kitu ndio kiwepo au kiwe cha kweli, kwa sababu huko kujua kwa kudhani kuhusu wazazi wako inaweza kuwa ndio kweli wazazi wako hata kama hauna uhakika wala uthibitisho wakati huo.
 
Na ndio maana nakuambia hizi inferiority zako huwenda ni matokeo ya makuzi yako uliyokuzwa ukiaminishwa kuwa elimu ya madrasa pekee ndio msingi mzima wa maisha ya binadamu.
Unarudia tena kuona kuwa mie napinga sayansi.
 
Mimi nimetumia tafsiri yako ulipoelezea maana ya imani ndio nimeuliza kama kuamini ni kutarajia kitu kutokea in future
Imani ni kwa kitu chochote.
je imani ya kuamini Mungu hapo inakuaje? Au kuamini Mungu sio imani?
Kwa muktadha wa imani za kidini. Ninyi mna amini tayari kuna Mungu ila hamna uthibitisho wala uhakika.

Na hapa ndio utata unaanza.

Mnaamini kwamba Mungu yupo, ila kumthibitisha hamuwezi. Sasa huoni kwamba hayupo?

Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Kila mtu angejua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho kabisa kwamba kuna Mungu.
Maana ni wewe ndio umefanya imani inahusu wakati ujao tu haihusu wakati uliyopo au uliyopita..
Kulingana na maandiko yenu ya kidini. Mnatafsiri imani kama kuwa na uhakika wa jambo, kumbe kiuhalisia sio tafsiri sahihi.

Imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho.
Ndio kurogwa hakuna uthibitisho ndio maana ni jambo la imani ama si hivyo?
Ndio
Uthibitisho haufanyi kitu ndio kiwepo au kiwe cha kweli, kwa sababu huko kujua kwa kudhani kuhusu wazazi wako inaweza kuwa ndio kweli wazazi wako hata kama hauna uhakika wala uthibitisho wakati huo.
Lakini huwezi kujua mpaka ufanye uhakiki upate uhakika wa either hao ni wazazi wako kweli, Au sio wazazi wako.
 
Back
Top Bottom