Al-mukheef
JF-Expert Member
- Feb 2, 2025
- 8,442
- 10,464
Hehehe!!!Maswala ya nani Kati ya mwanamke na mwanaume anapaswa kuchangia pesa katika familia hayana mpangilio maalumu, hayana kanuni na hayapaswi kabisa kuwekewa kanuni au Sheria kama mnavyotaka.
Binafsi huwa ninakerwa Sana na kauli inayosema "mke akiwa na milioni moja halafu mume ana laki tano familia ina laki tano kwa sababu mwanamke pesa zake anajua atazituamia vipi". Hii kauli ni ya kipuuzi mno, kwangu mimi pesa za mume ni za familia na pesa za mke pia ni za familia.
Nasema hivi kwa sababu siko tayari kuhudumia kiumbe ambacho hakina mchongo wowote zaidi ya kupiga domo. Hata ninyi mnaojaribu kujadiliana kujua nani anapaswa kuchangia acheni mara moja tabia hii, Kila mtu adili na mkewe/mumewe. Kama mtu hataki mke wake asichangie asipotoshe watu wengine humu.
Mke wangu atachangia Sana katika familia labda afiche pesa zake nisizione. Siko tayari kufanya mambo kwa presha ya jamii.
Eti "hamna hela ya mboga" halafu ana hela, NYAMBAFU!!
Al-mukheef Monetary doctor
Sio anavyoona ni sawa, sema anavyoona ni sahihi. Ukisema "sawa" hapa kwa asilimia kubwa umeongozwa na hisia, ukisema "sahihi" hapa umeongozwa na tafakuri ya kimantiki(na huo ndio uanaume)Ni kweli sio muongozo.
Kila mwanaume aongoze familia yake vile anavyoona ni sawa.
Kweli hiyo pesa zake azitumie kuwahonga vijana barubaru siyo?Hehehe!!!
Mwanamke ana haki ya kutumia hela yake bila kulazimishwa kuitumia kwa ajili ya familia.
Kama ataamua kusaidia kwa hiari basi hiyo ni sadaka na wema wake tu!
Kusaidiana katika ndoa ni jambo muhimu, lakini msaada wa mwanamke haupaswi kuwa wa lazima kwa kipato cha familia. Kila ndoa ina muundo wake, na kinachofanya ndoa iwe imara ni makubaliano ya wawili hao, si sheria ya lazima kwamba mwanamke achangie kifedha. Kuhusu maandiko, hata Mithali 31 inazungumzia mwanamke mwenye bidii lakini haielezi kwamba ni lazima achangie kifedha bali ni sifa ya kujituma na hekima. Pia, wakati wa bibi zetu hali ya maisha ilikuwa tofauti, na leo wanawake wengi wanachapa kazi si kwa sababu ni wajibu wa ndoa, bali kwa sababu wanataka maendeleo yao binafsi pia. Ndoa bora inategemea usawa na makubaliano ya wawili hao, si sheria za kulazimisha mchango wa kifedha.Majibu yapo kwenye biblia kama we ni msomi kasome!
Mwanamke aliumbwa kama msaidizi Kwa mwanamme Kwa Hali zote!hwakusema kulea watoto TU na kupika !MSAIDIZI!
ukisoma mithali 31 najua hampendi kusoma na hamtaki kukubaliana mwanamke anaonekana anachapa KAZI na anafananishwa na merikebu ya chakula yaani meli iliyosheni vyakula! Akileta mapato nyumbani mwake!!
Kizazi Cha kikahaba Cha wanawake wa kileo kilichojaa ubinafsi kinataka kujiuza ndani ya ndoa Kwa kutoa mchango wa tendon la ndoa na mapishi plus kulea watoto TU ndicho kinachosumbuka na kuuliza uliza maswali kana kwamba hakijui asili na wajibu wake!!
Tangy zamani bibi zetu walilima mazao ya biashara na mababu zetu ,walikamua ngombe wakauza maziwa na mapato wakayaleta ndani ya familia na kulea wakalea watoto katika bidii na kazi!na mababu wakabaki kama viongozi wenye kuongoza jahazi na kutoa uelekeo familia iendapo!!!
MWANAMKE UNAEJIULIZA MASWALI KAMA HAYA UNAPASWA UKASOME HISTORIA YA BIBI ZAKO WALISHIRIKI VIPI SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA KUSAIDIA FAMILIA ZAO,PIA KASOME MITHALI 31!
zamani hakukua na michepuko coz mitara iliruhusiwa na baba alioa pale alipopataka!Sasa leo Dini zimekataza tusioe mitara nasema DINI na sio maandiko Wala neno la Mungu wamekataza mitara ndio mnalia na michepuko kama kigezo Cha kuleta ubinafsi ndani ya familia!NASEMA DINI NA SIO MAANDIKO YA MUNGU!HAKUNA MWANAMME ANAWEZA KUWA MKRISTO KULIKO IBRAHIM BABA WA IMANI MWENYE WAKE WAWILI,YAKOBO MWENYE WAKE WANNE,MUSA MWENYE WAKE WAWILI,YESU HAKUOA MSIFANANISHE ANGEOA TUNGEANDIKA MENGINE!!
RUDINI KWENYE MISINGI ACHENI KUULIZA ULIZA NA MAJIBU MNAYO!
Hehehe!!!
Mwanamke ana haki ya kutumia hela yake bila kulazimishwa kuitumia kwa ajili ya familia.
Kama ataamua kusaidia kwa hiari basi hiyo ni sadaka na wema wake tu!
Nachangia inapobidi. Nisome vizuri. Mara nyingi anaweza kufanya mwenyewe na hajaomba msaada.Sio anavyoona ni sawa, sema anavyoona ni sahihi. Ukisema "sawa" hapa kwa asilimia kubwa umeongozwa na hisia, ukisema "sahihi" hapa umeongozwa na tafakuri ya kimantiki(na huo ndio uanaume)
Ni sawa kwa mwanafamilia kuwa na kipato na asichangie bill za nyumbani, lakini sio sahihi.
Si kila mtu ana mtazamo sawa kuhusu mgawanyo wa kipato kwenye ndoa. Kila familia ina njia yake ya kusimamia fedha kulingana na makubaliano yao. Kama wewe na mkeo mmekubaliana kushirikiana kifedha na mna furaha, basi hilo ni jambo jema kwa ndoa yenu. Lakini si sahihi kulazimisha kila ndoa iwe hivyo. Mwanamke anaweza kuchangia kifedha kwa hiari, lakini haipaswi kuwa sharti la ndoa. Kila ndoa ina mfumo wake wa uwajibikaji kulingana na hali na makubaliano ya wahusika.Nilivyosoma comment kwenye hii thread nimegundua wanaume mtaani tumebaki wachache
Haingii akilini mwangu eti kipato cha mke wangu ni chake na ndugu zake ila kipato changu ni cha mke wangu na watoto.
Ninashukuru mke wangu tunashirikiana vizuri sana katika mgawanyo wa kipato na tunaishi kwa furaha
Hapana,atatumia kwa mahitaji yake binafsi na kuisaidia familia kama akitaka na sio lazimaKweli hiyo pesa zake azitumie kuwahonga vijana barubaru siyo?
Hapo sawa. Mimi mwanamke ambaye siwezani naye ni yule ambaye ana pesa lakini hataki kuitumia kabisa kwa matumizi ya nyumbani.Nafanyia mambo yangu kwanza, zinazobaki nachangia kwenye familia
Good!No kwa huyu hilo haiwezekanii atatoa...!!
Kipato cha mwanamke hakina uhusiano wa moja kwa moja na mafanikio ya ndoa yake. Kuna wanawake wengi wenye vipato na ndoa zao zinaendelea vizuri kwa sababu wamepata wenza wanaoelewa maana ya kushirikiana. Pia, si kila mwanamke anayeingiza kipato anachukua ‘majukumu ya kiume’—wanawake wengi hufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na kusaidia pale wanapoweza. Ndoa inajengwa kwa maelewano na ushirikiano, si kwa mgawanyo wa majukumu wa kizamani unaomnyima mwanamke nafasi ya kujitegemea kifedha.Wanawake wenye vipato huwa hawana ndoa,bali wengi wao ni ma single mama,mwanamke wajibu wake ni kulea watoto na mwanaume ni kutafuta pesa kwa ajiri ya familia,ukimkuta mwanamke ana majukumu ya kiume katika familia basi hakuna ndoa hapo.
Inamfanananisha na merikebu ya chakula Tena anaamka Asubuhi na mapema kupalilia bustani,na huyo ndio MKE MWEMA WALA HAPEPESI YAANI MKE MWEMA NDIO ANAVYOPASWA KUWA HAKUNA COMPROMISE KWENYE HILO!!KASOME VIZURI!!Kusaidiana katika ndoa ni jambo muhimu, lakini msaada wa mwanamke haupaswi kuwa wa lazima kwa kipato cha familia. Kila ndoa ina muundo wake, na kinachofanya ndoa iwe imara ni makubaliano ya wawili hao, si sheria ya lazima kwamba mwanamke achangie kifedha. Kuhusu maandiko, hata Mithali 31 inazungumzia mwanamke mwenye bidii lakini haielezi kwamba ni lazima achangie kifedha bali ni sifa ya kujituma na hekima. Pia, wakati wa bibi zetu hali ya maisha ilikuwa tofauti, na leo wanawake wengi wanachapa kazi si kwa sababu ni wajibu wa ndoa, bali kwa sababu wanataka maendeleo yao binafsi pia. Ndoa bora inategemea usawa na makubaliano ya wawili hao, si sheria za kulazimisha mchango wa kifedha.
Mgawanyo wa kipato kwenye ndoa ni suala la makubaliano kati ya wanandoa. Hakuna asilimia maalum inayopaswa kuwa sheria kwa kila familia. Kila wanandoa wanapaswa kujadili na kupanga kulingana na hali yao ya kifedha, vipaumbele vyao, na maelewano yao. Jambo muhimu ni uwazi, ushirikiano, na kuhakikisha kila mmoja anahisi haki yake inaheshimiwa bila kulazimishwa kufuata mfumo fulani.Kama vipato vinaendana inashauriwa mkipata pesa mtoa asilimia 60 kila mtu kwa ajili ya maendeleo ya familia na 40 kwa matumizi yenu binafsi yaani bia,saluni, michango ya send off harusi, kusaidia ndugu nk
Kama pesa anazo ni lazima, labda kama kiasi alichinacho kinagota kwenye matumizi yake.Hapana,atatumia kwa mahitaji yake binafsi na kuisaidia familia kama akitaka na sio lazima
Kwa akili yako wewe unadhani kazi ya mwanamke ni nini kwenye familiaKumekuwa na mijadala mingi kuhusu mchango wa mwanamke kifedha ndani ya ndoa. Wengine wanasema ni lazima awe na mchango ili ndoa iwe na usawa, wengine wanaamini kuwa majukumu ya kifedha ni jukumu la mwanaume, huku mwanamke akihusika zaidi na malezi na uangalizi wa familia.
Mimi binafsi naamini kuwa kila mtu ana majukumu yake ndani ya ndoa, na kusaidiana kifedha ni suala la hiari, si wajibu wa lazima kwa mwanamke. Ikiwa mke anafanya kazi na anataka kuchangia, ni sawa, lakini haipaswi kuwa sharti ili kuthibitisha thamani yake kwenye ndoa.
Nimekutana na watu wanaoamini kuwa mwanamke asiyesaidia kifedha ndani ya ndoa ni mzigo kwa mwanaume. Pia, wengine wanasema mwanaume asiyemudu majukumu ya kifamilia pekee hatakiwi kuoa.
Je, mna maoni gani kuhusu hili? Ni wajibu wa mwanamke kuchangia kifedha kwenye ndoa, au ni suala la hiari kulingana na uwezo wake?
Karibuni kwenye mjadala!
Yaani mke atoke asubuhi saa 12 asubuhi kwenda kazini, anarudi usiku saa 2, huo muda wa kukushauri na kuhudumia familoa anatoa wapi wakati yuko busy na boss wake na zaidi kama anamkubali boss wake anaanza kukulinganisha naye.Huyu akipata mshahara lazima kiasi kirudi kwenye familia, otherwise akae nyumbani alee familia.Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Sasa hata kama ukioa anaye ingiza kipato alafu kipato chake kisiwe na impact yeyote kwenye familia ana kwambia majukumu ya kifamilia sio jukumu lake si bora uoe huyo goli kipa.?
Unaishi kizamanI mkuu.Ishu ya uchumi ni jukumu la mwanaume bora nioe mama wa nyumbani lakini ananipa energy ya kupambana ananipa amani na utulivu wa akili
MmeoanaNimeoa au nimeolewa ?
Hopeful kuna tofauti kubwa sana ya kipato baina yenu wawili au shughuli unazofanya wewe hazina kipato established yaani leo umepata kesho hauna kitu. lakini kama vipato vyenu vinalingana/vinakaribiana basi kuchangia ustawi wa familia inatakiwa iwe wajibu sio hiari.Nachangia inapobidi. Nisome vizuri. Mara nyingi anaweza kufanya mwenyewe na hajaomba msaada.
Wewe utasaidiwa na mke wako kila siku maana huna uwezo wa kutekeleza kila kitu. Wengine wanaweza..na hawajali kama mke ana kipato au la.