Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Nakazia, hakuna ushahidi wa kimaandiko kwamba Petro ndiye mwamba. Mwamba ni Yesu tu.
Mkuu hayo maandiko ya bibilia wamiliki ni hao wakatoliki

Wao ndio waliyakusanya na kuyatafasiri wenyewe kwenda kilatini

Kwani hujui vipande vya maandishi waliunganisha wenyewe

Kwani hujui hao wakatoliki hata kalenda ya sasa wamepanga wao na kazi alifanya Papa Gregory na kalenda hii inaitwa Gregorian calender

Sasa Papa Gregory aliamua yeye kututengenezea jinsi ya kuhesabu miaka hii ya sasa au hujui hilo?

Mfumo mzima wa sasa wa kupanga leo Christmass ,Pasaka wamepanga hao wakatoliki mpaka ijumaa kuu wamepanga wao taratibu hizo

Wakatoliki wameshikilia ukweli hapo vatikani kuna mambo wanasema na mengine wapo kimya wanatuchora tu

Hiyo bibilia wameandika wao na baada ya karne kadhaa wakaamua kuweka hiyo mistari na aya kwa kuweka namba

Ili upate habari kamili lazima uende huko vatikani kwenye makumbusho yao ingawa taarifa zingiine hawawezi kuzitoa kwa maslahi yao

Ila hao wakatoliki hiyo bibilia walikusanya maandishi wao,Wakaandika wanayotaka na mengine wakayaacha

Wakaunganisha vitabu vyao walivyokusanya wakaita bibilia
 
Unachosema hapa kina ukweli fulani hasa ukisoma kitabu cha Ufunuo wa Yohana. Hapa wakatoliki walishindwa kabisa kuelewa Yohana aliandika nini hapa.

Katoliki ilisimikwa na serikali ya Rumi. Na ikabadilishwa kabisa ikaacha kuyafanya mapenzi ya Kristo bali likaanza kufanya mapenzi ya Rumi.

Ndio maana Papa walikuwa wanaua sana watu Hadi 1798 Papa alikamatwa na akafa huko ufaransa(google usome).

Kanisa lilibadilishwa na kupewa nguvu za kiselikali. Likaanza kutawala kwa mkono wa chuma.

Katoliki sio kanisa la kwanza. Ila nikanisa lilipewa uwezo na falme ya Rumi na agenda nyingi za Serikali zinapitia humo Hadi sasa.
 
HAKUNA UPAPA ALIOUACHA MTUME YEYOTE!

PAPA NI KIONGOZI WA KUZIMU ANAEWAKILISHA HUKU DUNIANI KWA KUWEKA TAWALA ZOTE ZILIZOPO BILA MAPATANO NAE HUWEZI TAWALA!!!

SASA JE PETRO ALIKUA NA MAPATANO GANI NA SERIKALI YA KIRUMI!!?
Umemezeshwa matapu tapu
 

PAPA/MTUME PETRO NDIYE ALIWEKA SHERIA YA KUOA MKE MMOJA, NA SIJUI MKISHA OANA HAKUNA CHA KUWATENGANISHA,
ambayo kwa mtazamo wangu hakuiangalia vizuri kwani imetujazia watoto wa mitaani, masingle mother, na watu kuishi kwenye ndoa kwa mateso makali kwa sababu tu Petro alisema wasiachane...kwa maono yake ya kipindi hicho
 
Nahitaji ushahidi wa Biblia. Tukianzia kwa Petro, ni nani aliyempa cheo cha Upapa? Wikipedia sio Biblia.
SASA KAMA HUAMINI PETRO ALIKUWA PAPA, MBONA UNA AMINI SHERIA ALIZO TUNGA PETRO; MFANO KUOA MKE MMOJA, WATU WAKISHAOANA WASITENGANISHWE HADI KIFO HATA KAMA WANAPITIA MATESO MAKALI; NK NK SHERIA AMBAZO ZINATESA WAFUASI WAKE HADI LEO KWA KUWA NA WATOTO WA MITAANI KILA PAHALA MIJINI KWANI WANAUME WANASHINDWA KUWA OA MAMA ZAO, SINGLE MOTHER IMEKUWA NI FASHENI NA TUENDAKO UMUHIMU WA BABA UNAONDOKA KWENYE FAMILIA KWA SABABU YA HII SHERIA YA PAPA/MTUME PETRO AMBAPO WATOTO WENGI Wanalelewa na single mother hivyo kulelewa na tabia za kike kike bila kupata fursa ya kupata malezi ya baba/tabia za mwanamme na hivyo kutokuona umuhimu wa baba NK NK
 
Hiyo sentensi "KANISA LA KWANZA" imeandikwa wapi, mkuu. Nimetafuta sijaiona
Not direct , ila reference za mafundisho na kanisa kwa misingi ya injili ni kushuka kwa roho MTAKATIFU pale kwenye kusanyiko la kwanza wakati mitume wamejifungia
 
SASA KAMA HUAMINI PETRO ALIKUWA PAPA, MBONA UNA AMINI SHERIA ALIZO TUNGA PETRO; MFANO KUOA MKE MMOJA,
Petro hakutunga Maandiko ya Biblia. Wote walioandika Biblia waliongozwa na Roho Mtakatifu. Hakuna mtu(awe Papa, awe nani) anayeruhusiwa kuongeza wala kupunguza chochote kilichoandikwa kwenye Biblia.
Ufunuo 22:18-19:
Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyazidisha, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika mji mtakatifu, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki.
 
Kanisa linalozungumziwa kuwa la kwanza halikuwaabudu ama kuwaomba wafu.

Maria ni mfu

Petro ni mfu

Paulo na wengineo ni wafu.
 
Nahitaji ushahidi wa Biblia. Tukianzia kwa Petro, ni nani aliyempa cheo cha Upapa? Wikipedia sio Biblia.
hakua anaitwa papa elewa, ila alikua kiongozi mkuu wa kanisa baada yake akaja mwingine na mwingine kanisa kikazidi kukua kiti hicho hicho ndo hiki cha papa imepita miaka mingi tekriban elfu mbili ulitaka kwenye biblia waandike papa ?

alikua kiongozi mkuu wa kanisa
 
kama katiliki sio kanisa La kwanza je kanisa la kwanza ni lipi ?
 
Imeandikwa wapi Petro alikuwa kiongozi mkuu wa Kanisa? Unapozungumzia hoja yoyote ya Kikristo ni lazima uijenge kwenye Maandiko(Biblia). Askofu ametajwa kwenye Biblia, Mchungaji ametajwa, Nabii ametajwa...
Hicho cheo cha Upapa mnachosema ndio cheo kikubwa sana, kwanini Biblia haikitaji? Mmekitoa wapi?
 
Hii imekaa vizuri zaidi,naikubali.Ukiwa protestant unatafuta namna ya ku twist maana kwenye mistari iliyopo kwenye biblia kama mtoa mada anavyofanya kwenye michango yake.
 
Contradictions kama hizi ni uthibitisho tosha kwamba Biblia yenu ni HEKAYA.

Ndio maana mnapata mkanganyiko kufahamu nani haswa, Alikuwa Papa wa kwanza.
Hamna mkanganyiko hapo, mkanganyiko upo kwenye kitabu kinachoami juu ya Taurat, Zabur, na Injeel wakati chenyewe hakina!

Vv
 
MKUU

HATA HAYA YA LUKA YALIKUWA NA ROHO MTAKATIFU.👇👇

1Kwa kuwa watu wengi wameweza kuandika kwa utaratibu habari za mambo yaliyotimizwa katikati yetu, 2 kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3 nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, 4upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
 
hivi wewe unataka hadi iandikwe kwa maneno unayoyataka

sehemu ni nyingi zinaonyesha oetro alikua kiongozi mkuu wa kanisa kuanzia alivyoachiwa mamlaka na Yesu

"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."


"Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewaomba kuwapepeta kama vile ngano; lakini mimi nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka, waimarishe ndugu zako."

“Lisha kondoo zangu… chunga kondoo zangu…”

afu matendo ya mitume ndo kina kila kitu ukitaka kujua katiliki

ndo maana katokiki inaitwa janisa ka mitume
Kanisa Takatifu Katoliki La mitume
( watu wake wanaweza wakawa sio wa takatifu ila kile cheo ni kitakatifu Petro aliachiwa na Yesu mwenyewe )

kwenye matendo ya mitume amefanya mambo yanayoonyesha uongozi wake


Kuchagua mjumbe kuchukua nafasi ya Yuda

Kuhubiri siku ya Pentekoste (Matendo 2),

Kuwa msemaji mbele ya Baraza (Matendo 4),

Kuongoza maamuzi katika Kanisa la kwanza

je utasemaje hakua kiongozi
 
Utapoteza nguvu kwa hao wakatoliki kwanza wao wana misimamo wala hawabishani na mtu kwani wao ndio wameanda bibilia na hizi sherehe za christmass,Pasaka,Ijumaa kuu

Baada ya kupitia historia kupitia kwenye makongamano ya kisabato ndio nikajua nguvu zao,Wasabato wao wanasoma sana vitabu baadhi katoliki walivyoficha hivyo wana uelewa mpana zaidi kidogo

Wanawekeza kwenye ardhi na majengo dunia nzima,Wakiamua kujenga kanisa sehemu nzuri watakununua kwa pesa yeyote ile

Kama ni mwenyeji wa Dar hao watu wamepima upepo wameamua kwenda kujenga Basilica haijawahi kutokea huko kigambona baada ya kuona ST Joseph pa askofu wao mambo yao hayaendi wanavyotaka

Elewa aliyeandika bibilia ni huyo mkatoliki,Akafika sehemu na kuandaa kalenda tunayotumia sasa ya Papa Gregory inaitwa gregorian Calender

Mkatoliki akafuta miaka ya nyuma akaanza kuhesabu na leo ni mwaka 2025

Amekusanya maandishi akayaunganisha na mengine akayaacha hapo vatikana na vitabu hivyo vipo kwanini hakuviweka na kwanini alivitoa anajua yeye

Akaa akaamua kuweka mistari na namba kwenye bibilia huko watu wakibishana soma mstari huu mara ule yeye mwenyewe haongelei hiyo soma hapa wala pale

Makumbusho ya Vatikani yana siri nyingi,Ukifika huko utaacha hata kusali na utajiuliza mbona wao wanasali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…