Je, ni sahihi mzazi kumlaumu mwalimu moja kwa moja kutoka na kufeli kwa mtoto wake?

Je, ni sahihi mzazi kumlaumu mwalimu moja kwa moja kutoka na kufeli kwa mtoto wake?

Mr Mlokozi

Member
Joined
Jun 1, 2024
Posts
21
Reaction score
16
sote tunapaswa kukubaliana kwamba ili matokeo ya wanafunzi yawe mazuri panahiitajika ushirikiano uliotukuka katika mzazi, mwalimu na mwanafunzi huku kila mmoja akitimiza wajibu wake kadiri impasavyo kufanya na ikitokea mmoja au wawili kati yao hajatimiza majukumu yake daima matokeo yataendelea kuwa mabaya. Yaani ni kama mafiga matatu yanavyohitajika ili tu chakula kiweze kuiva vizuri bila figa moja chakula daima hakiwezi kuiva.

Jukumu kubwa la walimu ni kumfundisha mwanafunzi na jukumu kubwa la mzazi ni kuhakiksha mwanafunzi anapata mahitaji yote kwa kipindi cha masomo na Jukumu kubwa kabisa la mwanafunzi ni kuhakikisha anasoma kwa bidii.

Pamoja na majjukumu hayo mwalimu na mzazi majukumu mengine ya ziada katika kuhakikisha mtoto huyu anafauru ambayo ni pamoja na kumuhamasisha na kumtia moyo mtoto katika safari yake ya masomo laikini pia kumkanya pale ambapo hajafanya vizuri

Sasa kumekuwa na changamoto kwa wazazi hasa wale ambao wamewapeleka watoto wao katika shule binafsi ambapo wanalipa ada na michango ya shule kuishia kuwalaumu walimu pekee moja kwa moja kwa matokeo mabaya ya watoto wao kwa kudai kwamba wameshalipa ada inakuwaje mtoto anafel? bila kujali kwamba wao hawajatimiiza majukumu yao mengine kama wazazi

yaani unakuta mtoto akifeli wote wawili mtoto na mzazi wanaungana kumsema na kumlaumu mwalimu huku mtoto akilaumu kwamba kwa nini nimefeli na mzazi akilaumu kwamba kwa nn mwanganu kafeli.
huku lawama zote hizi zinapokuwa zikishuka kwa mwalimu unakuta yeye katimiza majukumu yake kikamilifu kafundisha vizuri kabisa kamaliza maada zote kadiri ya mtasali, katoa kazi nyingi sana kasahihisha na kufanya masihihisho katumia mda wa ziada kwa wanafunzi wenye kuelewa taratibu na pia katoa ushauri kwa kadiri alivyowe na matokeo chanya ya alichokifanya yanaonekana kwa wanafunzi wengine ndani ya darasa hilo

SASA JE NI SAHIHI MZAZI WA MWANAFUNZI HU ALIYEFEL;I KUMLAUMU MWALIMU MOJA KWA MOJA?
 
Sasa unataka nimlaumu nani?? Kama ningeweza si nisingelipa ada niwafundishe mwenyewe watoto wangu
 
Sasa unataka nimlaumu nani?? Kama ningeweza si nisingelipa ada niwafundishe mwenyewe watoto wangu
unaweza kumlaumu kama hajatimiza wajibu wake kikamilifu lakini kabla ya kumlaumu jiulize kwanza wewe umetiza wajibu wako?

Kuna wakati mwingine watoto wanafeli kutokana na stress za nyumbani hilo nalo ni jukumu la mwalimu?
 
Ni muhimu kukumbuka kuwa matokeo ya mtoto hayategemei tu ubora wa ufundishaji, bali pia kwa juhudi za mwanafunzi mwenyewe na msaada anaoupata kutoka kwa wazazi wake.
 
Ni muhimu kukumbuka kuwa matokeo ya mtoto hayategemei tu ubora wa ufundishaji, bali pia kwa juhudi za mwanafunzi mwenyewe na msaada anaoupata kutoka kwa wazazi wake.
kabisa hivyo mzazi pia anapaswwa kushiriki katika kumcoach mtoto na kuakikisha kuwa changamoto za kifamiia aziathiri saikolojia yake (anapaswa kuwa stree free)
 
unaweza kumlaumu kama hajatimiza wajibu wake kikamilifu lakini kabla ya kumlaumu jiulize kwanza wewe umetiza wajibu wako?
kuna wakati mwingine watoto wanafeli kutokana na stress za nyumbani hilo nalo ni jukumu la mwalimu?
Twende kiuhalisia mkuu, How often wewe umekuwa ukishuhudia mtoto anafeli kutokana na stress za nyumbani?? Tukiweka kwa namba kwa kufany rough estimations based on normal experience chini ya familia 50 tu kati ya 100 zinawezakuwa na migogoro that's 0.5 chance, katika hizo 50 ni chini ya 25 ndio zenye migogoro inayoathiri maendelea ya mtoto (sio migogoro yote inaathiri mtoto shuleni) still 0.5 chance so overall chance ya kuwa na migogoro na kuathiri maendeleo ya mtoto roughly less than 0.25, mimi naamini mwalimu akiwajibija ipasavyo kuna 0.5 chance ya mtoto kufanya vizuri, hivyo basi kwa hizi odds sina mwingine wa kumlaumu zaidi ya mwalimu
 
kweli kabisa kama ulivyosema twende kiuhalisia na kiuharisia kwa hali ilivyo hivi sasa si kwelikwamba ni asilimia 50 tu ndo zenye migogoro siku hizi migogoro katika familia ni mingi sana na ndiyo maana inapelekea kuongezeka kwa familiia za mzazi mmoja au watoto kuishi na wazazi wa kambo sasa unakuta mtoto yupo shule na mama anasema hiki baba anasema kile kutokana na kwamba wao hawapo katika makubaliano hivyo anabaki njia banda kuchagua kati ya mama na baba kitu ambaco lazima kitaathiri masomo yake sasa mtoto akifeli analaumiwa mwalimu wakati kulikuwa na uwezekano kushirikiana na kutatuachangamoto hii mtoto akafaulu vixuri tu bila kuathiriwa na migogoro hiyo
 
kweli kabisa kama ulivyosema twende kiuhalisia na kiuharisia kwa hali ilivyo hivi sasa si kwelikwamba ni asilimia 50 tu ndo zenye migogoro siku hizi migogoro katika familia ni ...
Hizo 50% ni rough estimation na hazifiki, usitake kunambia kati ya familia 1000 kuna familia 500 zina migogoro brother
 
Ni muhimu kufahamu kuwa matokeo ya mtihani yanategemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na juhudi za mwanafunzi, mazingira ya kujifunzia, na mbinu za kufundishia. Hata hivyo, kumlaumu mwalimu moja kwa moja kwa matokeo mabaya ya mtoto sio njia bora ya kutatua suala hilo. Badala yake, hapa kuna hatua ambazo mzazi unazoweza kuchukua na sio kukimbilia kumlaumu mwalimu:

  1. Mazungumzo na Mwalimu: Anza kwa kuzungumza na mwalimu wa mtoto. Uliza kuhusu maendeleo ya mtoto darasani na jinsi unavyoweza kumsaidia kuboresha matokeo yake. Mawasiliano mazuri na mwalimu ni muhimu.
  2. Kufuatilia Maendeleo: Fuatilia maendeleo ya mtoto kwa karibu. Jua ni wapi anahitaji msaada zaidi na jinsi unavyoweza kumsaidia kujifunza vizuri.
  3. Kuweka Mazingira Bora ya Kujifunzia: Hakikisha mtoto ana mazingira mazuri ya kujifunzia nyumbani. Kuwa na ratiba ya kujifunza, eneo la utulivu, na vifaa vya kujifunzia.
  4. Kuhamasisha na Kumsaidia Mtoto: Msaidie mtoto kujiamini na kumtia moyo. Onyesha kujali na kuwa tayari kumsaidia kwa njia inayofaa.
  5. Kushirikiana na Shule: Kushirikiana na shule ni muhimu. Hudhuria mikutano ya wazazi na ufuatilie maendeleo ya mtoto.
Kwa kumlaumu mwalimu moja kwa moja, hatutatui tatizo.
 
Hizo 50% ni rough estimation na hazifiki, usitake kunambia kati ya familia 1000 kuna familia 500 zina migogoro brother
naweza kukubaliana na wewe katika swala na asilimia hizo kwa maana sina takwimu kamili lkn naomba kuliza je jukumu la mzazi ili mtoto afauru ni kulipa ada na mahitaji ya shule pekee?
 
asante sana kwa maelezo mazuri sana hskika mzazi akitimiza majukumu yake hayo pamoja na mengine , mwalimu akafanya wajibu wake kikamilifu pamoja na mtoto kutia juhudi binafsi lazima mtot afauru tu
 
sote tunapaswa kukubaliana kwamba ili matokeo ya wanafunzi yawe mazuri panahiitajika ushirikiano uliotukuka katika mzazi, mwalimu na mwanafunzi huku kila mmoja akitimiza wajibu wake kadiri impasavyo kufanya na ikitokea mmoja au wawili kati yao hajatimiza majukumu yake daima matokeo yataendelea kuwa mabay...
Toto lenyewe jinga tu , Kwan wamefeli darasa zima
 
Ndiyo ni sahihi kabisa.

Siku hizi hizo sijui stress za familia mara migogoro ya familia.

Ni kichaka cha baadhi ya walimu wa siku hizi kukwepa majukumu yao ya kufaulisha wanafunzi.
 
Ndiyo ni sahihi kabisa.

Siku hizi hizo sijui stress za familia mara migogoro ya familia.

Ni kichaka cha baadhi ya walimu wa siku hizi kukwepa majukumu yao ya kufaulisha wanafunzi.
Kweli kabisa kaka, walimu hawatimizi majukumu yao.
 
naweza kukubaliana na wewe katika swala na asilimia hizo kwa maana sina takwimu kamili lkn naomba kuliza je jukumu la mzazi ili mtoto afauru ni kulipa ada na mahitaji ya shule pekee?
Sasa ni lipi mkuu?? Or unataka tuwafundishe wenyewe watoto wetu!?,
 
Ndiyo ni sahihi kabisa.

Siku hizi hizo sijui stress za familia mara migogoro ya familia.

Ni kichaka cha baadhi ya walimu wa siku hizi kukwepa majukumu yao ya kufaulisha wanafunzi.
walimu kama hao kweli wapo lakini lakini kiwa hivyo tunategemea zaidi ya robo tatu ya darasa wafeli lakini wengi wamefauru na wachache wamefelin bado huyu mwalimu hajatimiza wajibu wake?
 
usemacho kitakuwa kweli pale tu ambapo zaidi ya robo tatu ya darasa wamefeli lakini ikiwa ikiwa ni mwanao pekee ndo kafeli hapo kosa ni eidha la kwako mzazi au mwanao
 
Back
Top Bottom