Je, ni wakati wa vijana kufikiria kutafuta kazi nje ya nchi?

Je, ni wakati wa vijana kufikiria kutafuta kazi nje ya nchi?

Hizo kazi huko nje ni nyingi ndio na vigezo unaweza kua navyo, shida ni visa hata visa sponsored job wanataka mtu extraordinary ambaye nchini kwao kuna upungufu wa mtu huyo, msifikiri hizo kazi zote zipo kwaajili yenu wenyewe serikali zao zinalimit idadi ya watu wanaoingia kufanya kazi ili soko la ajira na uchumi wao usishuke, kwahyo uwe na kitu cha ziada ili upate visa ya kazi au uingie hiyo nchi kwa namna yoyote kihalali ndo utapata hizo kazi cheap
 
Yani tusipoanza sisi wenyewe kupendana yani wantanzania tupendane ona shida ya mwenzako kama yako yani msaidie mwenzako kulingana na uwezo wako siyo ufikilie et nikimsaidia atakuja kunipita maendeleo BC hakuna taiga lingine litatupenda ikiwa sisi wenyewe hatupendani.mfano wakati nilipokuwa naomba connection kuna Mtanzania kama Mimi aliniambia ili nitimize ndoto yangu et lazima niwe Shoga au nitafute vibibi vya kizungu nioe wakati Mimi na miaka 24 et nitafute vibibi nioe
 
Komaaaa

Ova
Kukomaa na kumtanguliza mungu pekee ndo silaha yangu nikweli najua maisha ya MTU yako kwa MTU lakini hatupaswi kulazimisha watu wengine watusaidie kama hawataki kikubwa nitafanya kulingana na uwezo wangu naimani mungu atabariki
 
Kwamba serikali yao inajipanga kwa miaka 60 ! [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Dunia imeisha now kila MTU anajifikilia yeye kwanza yani ule upendo wa asili wa kibinadam now hakuna.maisha tumetofautiana wewe ambaye unauwezo BC saidia wengine ndugu zangu hakuna fulaha nzur uone MTU uliyemsaidia akifanya maendeleo yani inapendeza sana pi kama hutaki kusaidia ni bora ukae kimya kuliko kuja hapa kuandika Uzi wa kujimwambafai ili tujue wewe uko mbele na tukikuomba msaada unazingua
 
Kwenye nchi zilizoendelea kwasasa kuna uhaba mkubwa wa vijana wa kufanya kazi lakini wakati huohuo kuna janga kubwa la vijana wasikuwa na kazi Tanzania. Pamoja ni jitihada nyingi za serikali za kusaidia vijana kupata kazi na kufanya shughuli za kilimo ni lazima vijana nao wajiongeze walau kuweka mikakati ya muda wakati serikali ikijipanga vizuri hasa kwenye viwanda na mashamba ya mikakati. Badala ya kushinda vijiweni huu ni wakati wa serikali kufikiria zaidi ya Tanzania kwenye mambo ya ajira.

Tatizo tofauti na jamii za nchi jirani kama Kenya na Uganda watu wengi Tanzania wameweka utamaduni wa kuaminisha vijana wakienda nje tu kutafuta maslahi eti sio wazalendo. Ni bora wabaki vijiweni na kupuyanga wakati hawana uwezo wa kuchangia chochote kwa familia zao na wazazi wao. Naomba mlielewe siongelei vijana wote lakini nacho sema hapa tusiweke madongo kwa wale wanaotafuta maslahi nje ya nchi. Je, kuna fursa zipi hasa na nashauri nini. Hii ni kwa wale vijana wasio na kazi wala vipato

1. Serikali msione aibu kuongea na kampuni kubwa za teknologia ambazo zinaajiri watu nchi nyingine. India mfano wanafanya kazi nyingi sana za nchi nyingine kuanzia engineering design, accounting, programming, computer coding, technology training. Sasa je, ni kwanini hakuna jitihada zozote za kuwezesha Watanzania waweze kuajiriwa wakiwa Tanzania. Nasema hivyo kwasababu mimi nipo USA na naona hizi nchi kuna watu wengi sana wanafanya kazi kutoka nchi nyingine. Kuna kampuni ya Houston, Texas ambayo ina wafanyakazi zaidi ya 100 na wanafanyia kazi India!. sasa hawa wametuzidi nini. Mawaziri wetu wa teknologia hata kujiangaisha au kufikiria haya hawafanyi.

2. Serikali iweke uhusiano mzuri na diaspora na kuwawezesha diaspora wenye nafasi za kiungozi kuweza kuajiri Watanzania. Tatizo kwasasa hakuna sheria ambazo ziko wazi mfano kama manager diaspora yupo Canada na anataka kumpa kazi kijana Mtanzania na afanyie kazi kutoka Tanzania je ni sheria gani za kikodi na uwazi zipo kwasasa ili yule mwajiri aweze kuwa na uhakika anafuata sheria? Je tunasheria za hivi au hatuna? mafao na kodi zinalipwa vipi?

3. Watanzania vijana wahangaikie kazi za muda. Nchi nyingi zina kazi za muda kuanzia kwenye kilimo, meli za wageni, hospitali, mahoteli.. na hata ujenzi. Vijana badala ya kushinda mitandaoni na kuendesha bodaboda kwa Tsh 10,000 kwa siku tumia muda wako kutafuta kazi nje. Hizi kazi ni za mikataba mwaka mpaka miaka mitatu halafu unaweza kurudi wakati serikali nayo imejipanga. Mjue tu miaka ya 1995-2000 kuna watanzania wengi tu walienda USA kwenye program ya summer camp. walitafuta wenyewe lakini vijana wa siku hizi ni wepesi kulalama badala ya kutafuta fursa.

4.Vijana tafuteni " mentor" au washauri wenye uzoefu. Kuna Watanzania Dunia nzima wewe ni kijana wa miaka 20's badala ya kulalama tafuta mtu mzima wa kukushauri ambaye anafanya kitu ambacho wewe unapenda. Tatizo leo mnashinda kufikiri na kutaka kuwa kama Diamond au Nandy badala ya kutafuta wataalamu au wafanyabiashara ambao unataka kuwa kama wao. Sio lazima wawe Tanzania. Jioulize Je una account ya linked? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi? Hata hapa vijana kuna watu wengi wakuwapa mawazo lakini mnakimbilia kupiga madongo!madongo yanakusaidia nini?

5. Vijana msisubiri serikali. Serikali haijawahi kusaidia vijana kama wakati huu lakini vijana wa huko nyuma miaka ya 1990's na 2000's walienda kutafuta vyuo na maslahi huko nje wenyewe na marafiki zao sio kwa msaada wowote wa serikali. Tatizo vijana mnasubiri sana serikali ambayo itachukuwa muda sana kuweka mambo ya ajira sawa. Nawashauri tafuteni kazi popote Duniani ilimradi unasaidia familia yako. Lakini usisahau nyumbani

Kukaa nyumbani vijiweni na kulalama siku hadi siku sio uzalendo. Na usijidanganye kuwa wewe ni mzalendo kuliko yule kijana anayetuma pesa kusaidia familia yake.

Nishatoa ushauri huu

Ubunifu ni muhimu sana kwa nchi. Ushauri wangu huu ni serious sana kuliko watu nwengi wanavyofikiria.

Mimi ni diaspora hapa USA naona jinsi ambavyo kazi nyingi za technolojia zinafanywa kutokea India. Sasa najiuliza kuna ugumu gani ya vijana wetu wanaomaliza shule na kufanya kazi hizi kutokea Tanzania? inawezekana kabisa lakini kunatakiwa kuwa na makubaliano na hizi kampuni.

Nashauri serikali ifanye mwaliko wa hawa maguru na wakubwa wa hizi kampuni ili wafungue data center Tanzania waweze kuajiri wataalamu tofauti hasa kwenye teknolojia. Tusione aibu kuandikia barua na kualika hata kama wakisema hawana muda tunaweza kubahatisha mmoja.

Niongezee tu kwenye soko la hisa za Marekani 50% ni kampuni za teknolojia hizo hapo ni thamani za kampuni mfano Apple hapo ni $T2.3 na Oracle ni $240B

bolCompanyCap Rank
1-27-23
Market Cap
1-27-23
1d Chg
1-27-23
1m Chg
1-27-23
12m Chg
1-27-23
AAPLApple12,311.01.4%12.2%-8.3%
MSFTMicrosoft21,848.00.1%4.7%-17.2%
GOOGLAlphabet31,294.3-0.9%-1.1%-34.6%
AMZNAmazon41,042.6-1.6%-10.6%-48.1%
BRK-ABerkshire Hathaway5682.80.0%1.7%1.9%
TSLATesla6561.811.0%63.0%-35.6%
NVDANvidia7501.02.8%44.2%-7.2%
TSMTaiwan Semiconductor8483.9-0.2%25.5%-19.8%
VVisa9477.23.0%12.2%12.3%
XOMExxonMobil10476.1-1.8%4.9%53.9%
UNHUnitedHealth11454.1-1.3%-8.6%5.3%
JNJJohnson & Johnson12439.8-0.4%-5.2%-1.4%
JPMJPMorgan Chase13411.60.2%6.5%-3.4%
METAMeta14397.93.0%29.8%-48.5%
WMTWalmart15386.50.8%-0.4%5.5%
MAMastercard16359.6-0.9%8.1%6.7%
CVXChevron17347.0-4.4%-0.1%32.6%
PGProcter & Gamble18331.6-0.4%-8.7%-11.7%
LLYEli Lilly19325.1-1.7%-6.2%44.5%
HDHome Depot20322.80.9%-0.9%-11.1%
BABANvidia21313.4-1.8%31.7%5.9%
BACBank of America22284.40.3%9.0%-22.0%
MRKMerck23267.2-1.4%-6.0%30.8%
ASMLASML24266.6-2.4%24.2%5.2%
KOCoca-Cola25261.6-0.5%-5.8%1.4%
ABBVAbbVie26258.7-0.8%-10.3%7.6%
AVGOBroadcom27247.0-1.3%6.8%9.0%
PFEPfizer28245.8-1.0%-14.4%-18.0%
ORCLOracle
Larry Ellison-Oracle Corporation
1675091721306.png

Tesla-Elon Musk
1675091739883.png

Microsoft-Satya Narayana Nadella
1675091764181.png

Alphabet-Google-Sundar Pichai
1675091784044.png

SAP CEO Christian Klein
1675091807608.png

IBM CEO Arvind Krishna's
1675091826399.png
Teknolojia Tz ni Nape! Like kichwa unakifahamu vizuri?
 
Jioulize Je una account ya linked? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi?

Ukweli tuambizane tu hata hiyo LinkedIn siyo bure kama unavyoisemea. Ni kweli ina proffesional wengi lakini ili uweze kupata connection nzuri ni mpaka ULIPIE na kama unavyojua sisi vijana wa kitanzania kila inapotokea suala la kulipia huduma hasa za kimtandao wengi wetu huamini kama UTAPELI.
Nadhani bado tuna safari ndefu sana.

Halafu kuna hawa watu wa uhamiaji wanakera sana kwenye utoaji wa hati za kusafiria.
Siyo kwamba hatupendi kuchangamkia fursa ila kuna mambo yanafanywa makusudi na mamlaka ili tudhoofike.
 
Hizo kazi huko nje ni nyingi ndio na vigezo unaweza kua navyo, shida ni visa hata visa sponsored job wanataka mtu extraordinary ambaye nchini kwao kuna upungufu wa mtu huyo, msifikiri hizo kazi zote zipo kwaajili yenu wenyewe serikali zao zinalimit idadi ya watu wanaoingia kufanya kazi ili soko la ajira na uchumi wao usishuke, kwahyo uwe na kitu cha ziada ili upate visa ya kazi au uingie hiyo nchi kwa namna yoyote kihalali ndo utapata hizo kazi cheap
Tatizo watu wakiambiwa nje ya nchi wanajua ni USA,UK, Canada, Australia lakini kumbe kuna nchi hazina usumbufu kupata visa na kazi za vibarua zipo nyingi na malipo ni mazuri.
 
Halafu kuna hawa watu wa uhamiaji wanakera sana kwenye utoaji wa hati za kusafiria.
Siyo kwamba hatupendi kuchangamkia fursa ila kuna mambo yanafanywa makusudi na mamlaka ili tudhoofike.

Hebu ona majirani zetu wakenya hawana mambo mengi
IMG-20230208-WA0002.jpg
 
Jioulize Je una account ya linked? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi?

Ukweli tuambizane tu hata hiyo LinkedIn siyo bure kama unavyoisemea. Ni kweli ina proffesional wengi lakini ili uweze kupata connection nzuri ni mpaka ULIPIE na kama unavyojua sisi vijana wa kitanzania kila inapotokea suala la kulipia huduma hasa za kimtandao wengi wetu huamini kama UTAPELI.
Nadhani bado tuna safari ndefu sana.

Halafu kuna hawa watu wa uhamiaji wanakera sana kwenye utoaji wa hati za kusafiria.
Siyo kwamba hatupendi kuchangamkia fursa ila kuna mambo yanafanywa makusudi na mamlaka ili tudhoofike.
Hivi unapata raha gani kuchanganya rangi hivi? Unaandika content ya msingi ila unaanza kuipodoa podoa
 
Tatizo watu wakiambiwa nje ya nchi wanajua ni USA,UK, Canada, Australia lakini kumbe kuna nchi hazina usumbufu kupata visa na kazi za vibarua zipo nyingi na malipo ni mazuri.
Mkuu ni nchi gani hizo ungeziorodhesha hata kwa uchache ndio msingi wa thread kama hii
 
Hivi unapata raha gani kuchanganya rangi hivi? Unaandika content ya msingi ila unaanza kuipodoa podoa
Highlighting inamaana haifai hasa pale unapolenga ujumbe fulani?
Mkuu sijapodoa podoa chochote ila nadhani umenitafsiri tofauti.
Nawasilisha 🙏
 
Nafikiri zama zimebadilika na vitu vingi vimebadilika pia miaka ya 90 tofauti Sana na sasa enzi hizo matishio kama ugaidi hayakuwepo/ hayakusikika kama miaka ya 2000 na kuendelea hata nchi nyingi zimezidi kubadilisha taratibu na sera za mambo ya nje kutokana na mazingira ya sasa. Lakini hiyo haiondoi fursa kwa vijana wengi kujaribu kutafuta maisha nje ya nchi yao hasa mataifa ya magharibi kiukweli balozi zetu zimekaa kisiasa zaidi kuliko uhalisia wenyewe ni ngumu kwa wao kutafuta fursa na kiziweka bayana kwa wenzao walioko nyumbani

Wakati huu fursa ni nyingi zaidi kuliko wakati wetu
 
FYI hata sisi tupo USA so you're preaching to the choir. Sijasema vijana hawabebi lawama kabisa ila nimesema serikali inabeba lawama zaidi. Ni wazi kupata passport bongo ni kazi wakati nchi zingine passport ni haki yako. Serikali ambayo haitaki hata paypal utaiambia nini kuhusu kuvutia tech companies? Unadhani ni kwanini Microsoft, google, twitter, BBC, Visa, FB hadi NALA kampuni ya mbongo kabisa are headquartered in Kenya badala ya TZ? Hapo napo utalalamikia vijana? Ndo maana nasema 80% ya shortcomings za vijana in the tech world ni sera mbovu za serikali.

Nisome hapa: Diaspora Hawatoi connection?

Napenda kutoa maoni na kujenga kuliko kulaumu na hiyo naona ni kati ya tofauti ya vizazi. Ingependeza zaidi kama ungetoa maoni tufanye nini step kwa step tuondokane na tatizo. Mfano kama passport zinasumbua basi tafuta mtu aliyefuatilia ili tujue ni sehemu gani hasa inakwamisha mambo ili tuweze kuwaelekeza wahusika kwa uhalisia. mfano tatizo ni wanataka documents nyingi, rushwa, technologia, muda au pesa ya kibali chenyewe?
 
Jioulize Je una account ya linked? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi?

Ukweli tuambizane tu hata hiyo LinkedIn siyo bure kama unavyoisemea. Ni kweli ina proffesional wengi lakini ili uweze kupata connection nzuri ni mpaka ULIPIE na kama unavyojua sisi vijana wa kitanzania kila inapotokea suala la kulipia huduma hasa za kimtandao wengi wetu huamini kama UTAPELI.
Nadhani bado tuna safari ndefu sana.

Halafu kuna hawa watu wa uhamiaji wanakera sana kwenye utoaji wa hati za kusafiria.
Siyo kwamba hatupendi kuchangamkia fursa ila kuna mambo yanafanywa makusudi na mamlaka ili tudhoofike.
linked ni bure kulipia ni mahitaji binafsi. Mimi sijawahi kulipia na nime connect na watu zaidi ya 100!
 
linked ni bure kulipia ni mahitaji binafsi. Mimi sijawahi kulipia na nime connect na watu zaidi ya 100!
Ooh sawa mkuu kwa upande wako.
Huenda ikawa mimi nilitaka connection kubwa sana. 100k+ purchase
 
Back
Top Bottom