Kwa kifupi MK54 ile dhana ya "mabeberu" wanahusika inatilia mkazo na watu wengi ktk media zillizo huru zinazojaribu kujua kilichosababisha mkuu wa nchi kufariki akiwa madarakani huku akiwa na ulinzi mkubwa pamoja na kuzungukwa na madaktari bingwa.
Tabu ni kuwa hata kama itakuwa kweli mabeberu wamehusika, itakuwa ngumu serikali ya Tanzania kusema hadharani kwani italeta taswira ya udhaifu mkubwa ndani ya vyombo vyake ya ulinzi na usalama.
Ni dhahiri suala hili la mikono ya mabeberu kuhusika, litabaki kuwa siri ya taifa na pia somo kubwa kuwa waimarishe vyombo vyake kupambana na tishio la mabeberu toka nje badala ya kuwekeza nguvu zote za intelejensia, udukuzi, ulinzi na usalama kuwadhibiti waTanzania wenye kupaza sauti za upinzani ktk siasa za Tanzania.
Wakati ukweli ni kuwa wapinzani siyo tishio kwa nchi bali ni sauti za kizalendo hasa zinazoitakia mema zaidi nchi yao ya Tanzania kwa kukosoa sera za kiuchumi, kisiasa na kijamii ila taifa liweze kufikia maendeleo ya juu zaidi ktk maeneo ya siasa, uchumi na jamii kwa ujumla .