Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Aisee ungemswekaa ndaniii
 
kwakweli inauma kuuwaamini ndugu unaweza kujinyonga, inaniuma mno kwa hasara hii nakumbuka ilikuwa tarehe 12/7/2015 na baadae 25/10/2015 nikamwamini mtu wangu wa karibu Magufuli tukampa nchi kwakweli yanayoendelea mungu ndo anajua
cc tindo
Hahahaaaaaaaa.... Unamwaminije mtu aliyeshindwa kupata combi (masomo 3 tu) toka form 4 kwenda form 5 eti aongoze nchi?
 
Aisee ungemswekaa ndaniii
Hapo ya kwanza niliachana nae bila kumpa chochote bimkubwa analaumu nimemwachaje bila kumpa chochote ikabidi nimpe kiduka flani cha uswazi nilianzia nacho maisha kilikua na km m2 plus nacho akaua tena, ndio baada ya miaka m4 kaja kuomba msamaha ndio nkamfulia hilo la mwisho.
 
MAMA YAKO ATAKUTAPELI KIVIPI? AMEKULA VYAKE. NANI KAMA MAMA.
Hata mimi nashangaa. Mama kama anataka pesa, anaomba tu. Kuna watu mnakopeshana na mama zenu? Inaonekana mama zenu bado vijana sana.
 
Kamuoa dada yangu kabisa aisee. Aliniahidi atanikabidhi Leo lakini simu hazipokelewi

...Mkuu, Unatakiwa ukazushe bonge la Valangati mbele ya dada yako ili ajue kaolewa na mtu gani! Si ajabu anajisifia kwa dada yako kwamba amekumalizia kazi yako iliyopita ila hutaki kumlipa! Chukua hatua....[emoji35][emoji35]
 
Majaribu haya nimeyapitia sana - marafiki na ndugu. Nina karibu mil 10 kwenye mikono ya watu huko nje tangu 2005. Sitaki kueleza jinsi ilivyotokea ili nisije kujulikana identity yangu (Omusolopogasi) kwa hao watu. Lakini nimejaribu kusahau na tumeendelea na mahusiano kana kwamba hakuna kitu. Ila kuanzia hapo, sijakopesha ndugu/rafiki na wala sitakopesha tena. Kama hali inaruhusu, ninatoa tu - pesa ndogo ndogo - wala si kukopesha. Kama kuna mgonjwa, namnunulia dawa nampa nk nk.
 
...Ulifanya jambo jema sana Mkuu. Ubarikiwe [emoji120][emoji120]
 
Me mtu wa karibu mno kanitapeli.Nikimdai anasema anakumbuka atanipa but hafanyi utekelezaji
 
Reactions: Aza
Hii mambo ya mtu kukupiga cha juu unapomwomba asimamie mradi wako halafu baadae ukija kumuuliza anakugeuzia kibao yapo sana Bongo.
 
Aisee kwenye suala la pesa sitakaa nimuamini mtu yeyote... Mpaka leo bado nina majeraha ya dhuluma niliyodhulumiwa mwezi wa 5. Almanusura nilazwe, niliumwa mno...
Jikaze nakuhakikishia baada ya muda utapata kushinda hizo ulizopigwa. Miaka kama mitano iliyopita nilijiwa na jamaa yangu akaniambia kuna biashara ya masandaku na mabegi anayofanya na inalipa sana lakini hana mtaji wa kutosha kuzungusha. Akanishauri niongezee mtaji halafu biashara (duka) iwe yetu sote. Nikampa milioni 5. Kweli jamaa akachakarika baada ya mwaka na nusu akawa amenunua bajaji mbili na duka limependeza kweli. Sasa kilichonishangaza kila nikitembea kwenye biashara naona jamaa amenibadilikia na kununa sana.. Uchangamfu wote umeisha. Mimi nilikuwa naishi mkoa mwingine. Nikawa najiuliza kwanini? . Basi siku moja akaniondolea uvivu. Akanieleza makavu makavu kuwa biashara inaenda vibaya na kuna uwezekano fedha zikapotea. Akasema hataki lawama hivyo atarudisha fedha zangu. Nilisikitika sana lakini sikuwa na la kufanya nikakubaliana naye. Nikampa account namba arudishe. Baadae ndiyo nikaja kugundua kuwa baada ya biashara kuchanua alipata tamaa ya kuimiliki mwenyewe na alikuwa na mpango wa kurudisha kweli milioni 5 yangu. Lakini alivyonifukuza tu mambo yakaanza kwenda mrama mpaka sasa hana kitu tena na fedh yangu alishindwa kurudisha.
 
...Mkuu, Unatakiwa ukazushe bonge la Valangati mbele ya dada yako ili ajue kaolewa na mtu gani! Si ajabu anajisifia kwa dada yako kwamba amekumalizia kazi yako iliyopita ila hutaki kumlipa! Chukua hatua....[emoji35][emoji35]
Siku zake zinahesabika. Nimetumwa hela aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…