Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo. Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni 1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address 2:Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania) 3:Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1:CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2:KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3:KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4:KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?
hii iko hivi.... 1:Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted. 2:Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.comhii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.
Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao
Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2:COMGATEWAY
link-http://comgateway.com/ hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na uona wana policy nzuri sana,cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani,hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3:BORDERLINX
link- Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4:SHIPITO
link-USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5:STACKRY
link- Stackry - US shopping, global shipping hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi. STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU please evaluate kindly.

nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi . maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila ithink there r limits.. help Mwl.RCT

Nimekuwa nikijaribu kujiunga na PayPal hapa Tanzania bila mafaikio. Msaada tafadhari
 
Mkuu nimefikia hapa sijaelewa niendelee vipi
 
Attachments

  • 1419073832540.jpg
    1419073832540.jpg
    57.9 KB · Views: 596
Mkuu nimefikia hapa sijaelewa niendelee vipi

Hapo kilichobakia mkuu ni kuuship mzigo kuja tanzania pamoja na kufanya malipo kwa comgateway tu.ngoja niongee na admin aniongezee nafasi ya thread niweze kuonesha vizuri zaidi mkuu..
 
Hivi pale kwenye thamani ya kitu ni thamani ya bei uliyonunulia au thamani gani yanayohitaji?

Maana nilinunua betri amazon kwa US$38.36 , nilipoona kuna sehemu inadai niandike thamani ya kitu ninachotaka kusafirisha nikaandika hiyo hapo juu. Gharama ya kusafirisha mzigo ikawa US$ 64.60.

Nikaona gharama ya kusafirisha ikawa mara 2 ya kununulia

Au kuna sehemu nilikosea kuchagua namna ya usafirishaji?
 
Yan kannt read all the posts but.. Kazi Nzuri mnafanya!! Honestly I didn't know but atleast now sitaogopa kihivo.. Unajua kukosa elimu ndo kunatufanya Watz Tunakua nyuma kwenye maendeleo.. Koz hem fikiria mtu anataka bidhaa kutoka marekani but Anaona Bora asafir kuufata mzgo and arud nao which is so costly compared to this system ya online purchase!! Worth thread!
 
Nawashuku sana wadau wa uzi wenu na kwa wato waliochangia uzi huu nimefanikiwa kuagiza kitu na kimefika bila zengwe mwanzoni nilihisi kama itakuwa ni ndoto ila ni kweli vitu vinafika SHUKRANI za pekee kwa MZEE RULA jamaa amenisaidia tangu hatua ya kwanza hadi ya mwisho shukrani sana TANZANIA hasa jamii forum kuna vitu vizuri sana mtu unaweza ukajifunza kupitia watu wa JM na ukapata kitu haihitaji kwenda darasani much respect to all
 
nikipata pesa nitarudi huu uzi. maana sitaki nitumie account yangu ya mshahara. nipate pesa nifungue account maalum kwa hiyo shughuli
 
Njia unayotumia ni POSTA tu, la muhimu uwe na sanduku la uhakika baasi

unanunua mzigo kwenye Mtandao kisha wao wanakutumia kwa Adress uliyoweka kule mtandaoni

unapewa tracking number kisha unaanza kutrack movement zake inachukua two weeks kutoka china/hong kong/ singapore mpaka Tanzania

kuna trick ya kukwepa kodi ila siwezi iandika hapa maana unaweza kuumia sana ukiwa hujui jinsi ya kufanya KODI ni kubwa mno baadhi ya items na carriers

in short na enjoy kununua mtandaoni na kusubiri two weeks kitu genuine kuliko kulipa sh. 100,000 zaidi madukani kariakoo au POSTA

mkuu heshima kwako, naomba huo ujanja wa kukwepa kodi, kuna item nategemea kuipata this week, naomba ni pm siunajua kodi inaumiza.
 
Kodi unaikwepa Wakati unanunua pale Kama nilivyosema kwenye post zangu zingine
 
KWA ANAYE HITAJI CM, IPAD & CAMERA
Zipo digital camera za aina mbali mbali pamoja na professional camera, cm kama huwawei ascend y 530, tecno M3, tecno P5, htc, lg na nyingine nyingi tu, zipo na lenovo ipad kwa yeyote atakayehitaji tuwasiliane kwa no: 0715-546818
 
Huu uzi ni wa maana saana ngoja nipitie wote kabla sijauliza maswali yangu na mimi
 
eti kunamakato ya kutumia/ku activate online transaction kwa crdb? au makato yoyote kwa hiyo huduma?

Sidhani kama yapo mkuu na kama yapo ni kidogo sana mimi natumia NBC sijakatwa chochote
 
mi nataka niagize metal detector kutoka amazon ila sina mastercard af nipo mza naombeni msaada
 
Back
Top Bottom