JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Kama waliandamana baada ya kugeukwa, hiyo ni sahihi kabisa.

Hata hivyo, ndio wajifunze kuwa CCM sio wema.
Inasemekana walipelekwa msata kupiga kwata la maana baada ya hapo wakaomba warud majumban kwao wale wabishi walipelekwa ngelengele kwa wale jamaa wa kuvuta magari kwa meno
 
Kwanini waliwaahidi kuwa wajitolee kwenye ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino kisha watapewa ajira ya kudumu Jeshini?? Kazi imeisha wametimuliwa. Kwani ni kosa kuwakumbusha Wahusika ahadi yao kwao??

Kuna jambo lipo nyuma ya pazia.
Amiri Jeshi Her Excellency Madam President of URT Hon.Samia S.Hassan,please have mercy to those young Soldiers. They completed their task @building New State Houses, consider them and listen to what really happened there.
Hao ni vijana wetu,usikalie Ikulu iliyojengwa kwa dhulma ya nguvu za vijana hao.Waliahidiwa ajira je,wamepatiwa ajira/ujira waliostahili?Usikute wamewa provoke ili wapate jinsi ya kuwamwaga.Huko waendako ni salama?Kama wameasi huko mitaa kutakuwa salama?
 
Nimesoma habari moja kuwa JKT imesitisha mikataba na kuwafukuza vijana zaidi ya 800 baada ya kuandamana Ikulu wakinishinikiza kuajiriwa

Baada ya hao vijana kuja mtaani,wanajua kushika silaha na mafunzo ya awali ya kujihami,je hao vijana hawawezi kujiunga na vikundi vya kigaidi kama cha ISS huko Msumbiji?

Je serikali inawafuatilia hao vijana zaidi 800 mienendo yao mitaani kama sio rahisi kushawishika kujiunga na vikundi vya kigaidi kwa ukosefu wa ajira na kuleta majanga nchini?

Au unaweza ukawa mtego,wakashawishiwa kugoma wadai ajira ili watimuliwe wakajiunga na ISS huko Msumbiji


Serikali ibuni mikakati ya kuajiri vijana au kuwawezesha kupata mazingira rahisi kujiajiri ili kuepuka kushawishika kuvuka mpaka kule kusini na kujiunga na ISS

Narudia kuwatimua vijana 800 JKT ni hatari zaidi kwa usalama uliopo kusini mwa Afrika

Wengi tu wapo kitaa wanapiga kazi, wajiungenao waache kuchagua kazi.


Kujiunga isis sii mpaka wazungu/wahusika wa hicho kikundi watume mawakala wao waje huku wawaandikishe, ama watajipeleka wenyewe!!!!!
 
Kwa tetezi nasikia wamefanya kazi zaidi ya miaka 3+, wamejenga Chamwino, Ukuta wa Mererani, majengo ya magereza Ukonga, ndio walio ratibu wizi wa kura na usimamizi wa uchaguzi 2020 na n.k, pia waliahidiwa baada ya kumaliza shughuli zote hizo watapewa ajira jeshini lakini baadae upepo ukageuka na ndio maana walifanya mandamano kwenda Chamwino.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Kama waliratibu au kushiriki kwenye wizi wa kura mimi ni nani ni wahurumie ?
 
Unaongea sana ndio maana hata huwa hujui unatafuta nini.

Kwanza hakuna asiyejua kuwa JKT tangu wanatoa matangazo yao, hawatoi AJIRA. Ni sehemu ya kujitolea.

Kwa vyovyote wasipokupa Ajira, huna msingi wa kudai.
Ili tujue ukweli ni vema tusikilize upande wa pili.

Kuna stori moja ya jeshini ningeweka ila basi tu, kuna wakati watu huonewa sana kwa kisingizio cha nidhamu ya kijeshi
 
Jeshi linaongozwa na utii na hutakiwi kuhoji chochote kutoka juu, bali kutekeleza, kinyume na hapo watakuondoa tu.
 
Kama walishiriki kuratibu wizi wa kura basi ni karma inawatafuna. Amini nakwambia wote waliofanya au kushiriki udanganyifu na kutangaza kibabe ushindi ule!! Lazima walipe Kuanzia Juu mpaka chini. Mungu yuko kazini sababu Binadamu tulishindwa na Matokeo mnayaona.
Kama walishiriki kuiba kura zetu wale wangewatoa pale hata kwa viboko.
 
Kama walishiriki kuratibu wizi wa kura basi ni karma inawatafuna. Amini nakwambia wote waliofanya au kushiriki udanganyifu na kutangaza kibabe ushindi ule!! Lazima walipe Kuanzia Juu mpaka chini. Mungu yuko kazini sababu Binadamu tulishindwa na Matokeo mnayaona.
Au ndiyo wale walikuwa na masweta yameandikwa jeshi la akiba ?
 
Yaani wameshindwa kabisa kukaa nao chini wakamalizana hadi wawafukuze? Kwahio tuna jeshi bado linalotumia nguvu zaidi kuliko akili zaidi. Kwa babahti mbaya sana hata wakiwahoji hawataweza kuandika chochote, hatuna waandishi wenye uthubutu huo

Jeshini Hakuna mazungumzo ya Kudai haki au kukataa amri. Hilo liko wazi
 
Nani aliwambia jkt wanatoa ajira?
Tatizo wanasiasa wanaingilia mambo ya jeshi,mwishowe miluzi inakuwa mingi
Sana

Ova
 
Hesabu ziligoma kuwaajiri vijana 2400 sio mchezo nyie [emoji1787]

Ilibidi wakate kibangala 800+ili wabaki wachache [emoji1]
 
Siwafundishi kazi, bali naamini taalamu yenu inawataka mfanye hivyo na si kuishia kupata taarifa za upande mmoja tu kwa maana ya maelezo ya viongozi wa Jeshi na serikali tu bila kuwahoji Vijana waliofukuzwa.
Ungetuletea mahojiano yako ungetusaidia badala ya kutuma waandishi
Jeshini hakuna siasa,migomo,maandamano hayo ni Mambo ya raia,jeshini ni amri tu
 
Hata tafsiri ya askari kuasi nadhani ipitiwe upya.
Askari wanaonewa sana kuanzia kwenye maslahi, maisha yao ya kiutumishi n.k
Lakini wahusika mara zote wanawambia wakihoji watashtakiwa kwa kuasi, hili neno limekuwa ni kichaka cha kunyanyasa watu huko majeshini, watu wanahamishwa kwa fitna, wanapigwa adhabu za chuki lakini hawawezi kuhoji wala kuuliza kwa kisingizio hiki cha kuasi jeshi.

Kuna watu wanadhulumiwa mpaka posho zao zilizowekwa kisheria lakin sentensi ya kuasi jeshi inahalalisha dhuluma hiyo.
CDF ni mzazi kaa na hao watoto hebu wasikilize neno kwa neno, CDF hata ww una watoto, una wajukuu n.k
Wakati mwingine wafuasi wako wanaweza kukupa maneno ya ukakasi ukajua ndio sura halisi ya jambo lakin mengine unaweza usiambiwe.
 
Back
Top Bottom