JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Katika swala hili nimeona watu wengi wakijadili kwa mlengo wa kuwaonea huruma hao vijana waliotimuliwa JKT

Tukirudi nyuma, hii haikuwa ahadi ya kwanza kwa vijana wa JKT. Kuna wale waliojenga ukuta wa mererani nao pia walipewa ahadi Kama hii.

Tukitumia mfano huo wa waliojenga ukuta wa mererani tunaweza kujua Kama hao vijana walikurupuka au wameonewa

Kwanza inabidi tukubaliane kuwa jeshini au Taasisi yoyote wa namna yao ya kuajili watu wao. Haiwezekani ahadi itoke tu (tena kisiasa) halafu siku hiyo hiyo woooote wasajiliwe! Sidhani Kama huo ni utaratibu! Jeshi Kama jeshi wana vigezo vyao na taratibu zao lakini zaidi nao wanaajili kulingana na bajeti na uhitaji

Wale walioahidiwa baada ya kujenga ukuta wa mererani, sio kwamba baada ya kumaliza ujenzi wa ukuta basi kesho yake waliajiliwa na majeshi mbalimbali, HAPANAAA!

Kilichofanyika baada ya mkataba wao wa kujitolea kuisha wao waliendelea kubaki kwenye makambi mbalimbali ya JKT wakati wale ambao hawakuwa kwenye orodha ya ahadi ile walirudi nyumbani baada ya mkataba

Waliendelea kutumiwa bila malipo yoyote kusubilia utekelezaji wa ahadi waliyopewa mara pale kutakapokuwa na uhitaji na majeshi yetu na bajeti zitakaporuhusu kuajili nguvu kazi nyingine

Wapo walioshiriki kujenga hiyo hiyo ikulu katika hatua za mwanzo, wengine walijenga ukuta kule Kizuka TPDF na walikaa zaidi ya miaka mitatu baada ya ahadi ya Rais bila kuajiliwa na jeshi

Kulipotokea uhitaji wengi wao hadi sasa wamekwisha ajiliwa!

Nini nataka kusema?

Kuna watu walibeza kauli ya Ndugai juzi bungeni kuhusu vijana ya kutokuwa na uaminifu, lakini ile kauli si ya kubeza

Vijana wengi siku hizi ni wajuaji sana na wako speed mno!

Hawana subira wala hawana muda wa kutafakari kitu katika mapana yake

Wale vijana waliojenga ukuta wa mererani, Kuna vijana watatu nawafahamu walifikia hatua ya kutaka kukata tamaa!

Kwanza walikuwa graduate na mmoja wao alikuwa na mke na mtoto hivyo alifikia hatua ya kuona anapotezewa muda!

Katika kumpa moyo, swala pekee nilikuwa namuuliza ni "Kama unahis hawatawaajili, kwanini wamewabakiza kambini na wengine wameondolewa??

Hao vijana walikurupuka na hawafai kuwa wanajeshi.

Kwangu Mimi wangetimuliwa baada ya kugoma kurudishwa nyumbani kushinikiza kwamba waliahidiawa ajira na Rais ningekuwa upande wao kwa asilimia zote kwasababu ni ngumu sana jeshi kuja kuwachukua mtaani na kuwapa ajira, lakini hawakufukuzwa kambini! Walibakishwa kuendelea kusubiri ahadi wakati wale wengine wasio na ahadi walisharudi makwao

Ni kawaida majeshi kuwatumia sehemu mbalimbali pale wanapowahitaji ilimradi tu wako mikononi mwa jeshi na hakuna aliyesema ahadi waliyopewa ni batili!

Kwa hiyo wao walitaka wabaki hapo hapo chamwino hata Kama hamna kazi za kufanya??

Au walitaka kwasababu Rais katoa ahadi waajiriwe siku hiyo hiyo hata Kama hakuna uhitaji?? Wakiajiliwa wakakosa mshahara si utakuwa mgogoro mwingine!??

Tuwajengee vijana uwezo wa kupambanua mambo kwa kina kabla ya kuchukua hatua kwa mihemuko
 
Maandamano huwa ni kitendo cha watu kutosikilizwa madai yao.
 
“Tunasikitika kufuta mikataba ya vijana 854 wa JKT kutokana na kufanya vitendo vya uasi.”Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania - Jenerali Venance Mabey
----------



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo amesema wamefuta mikataba ya Vijana 854 wa JKT ambao ni miongoni mwa walioahidiwa kupewa ajira kwa kujenga Ikulu, Chamwino na hii ni kutokana na Vijana hao kufanya uasi kwa kugoma na kuandamana kwenda Ikulu.

Mytake ; Gharama kubwa zilizotumika kuwaandaa hao vijana ili kuja kulitumikia taifa zinarejeshwa vipi?
Ni bora kupata hasara kuliko kufuga Waasi. Jeshi Silaha yake kubwa ni utii. Tukiwa JKT miaka hiyo tulifundishwa kuwa Tii kwanza amri iliyotolewa. Hakuna muda wa mjadala jeshini. Mko Vitani kamanda anakwambia mpige risali adui unaanza kusema mkojo umenibana....mtakufa
 
Sasa hao vijana waliambiwa Ikulu kuna ajira? Waende kusini wakabangue korosho na mabomu
 
Upande wa pili ni ahadi ya ajira ambayo imeshindwa kutimilika sababu aliyewahaidi hayupo tena
 
Pumbavu! Hao wengine walioajiriwa ni special sana kwamba hawaendi chooni au, kama ni hivyo hao wengine wote walioajiriwa basi wafukuzwe kazi pumbavu
We jamaa unakaza sana kichwa...kabla ya kuenda jkt mnaambiwa kabisa JKT HAITOII AJIRA, ila vyombo vya usalam (polis, magereza, uhamiaji na jwtz) wakiwa na upungufu wa askar wakihitaji ndipo wanaenda jkt kuchukua vijana wenye sifa wanazozitaka...sasa ikitokea wamekuja jkt kuchukua vijana kama nawewe ukiwepo huko mkataba wako haujaisha ndo bahati imekuangukia ...
Ila ikitokea vyombo vya usalama haviitaji askari wapya basi tena imekula kwako mkataba ukiisha unarudi home kutumia ule ufanisi ulijifunza jkt kujikwamua kimaisha.
 
Sawa jiaminishe ivyoivyo watakapo anza kuchinja ovyo watu mtaani ndo utajua umuhimu Wa kuwaajiri hawa vijana.
Hakuna bongo hii wakuchinja mtu eti kwajili hana ajira.hajazaliwa mtu huyo.kama kuandamana tuu kudai Haki za msingi sukari imepanda bei watu wanashindwa itakuwa kukosa ajira?
 
Mgambo wana mafunzo gani zaidi ya kukimbiza kuku?

Mgambo wanapiga mafunzo km wajeda tu ndo maana kuna km maonyesho yalifanyika pwani ya Bagamoyo wagambo walishiriki vizuri tu zoezi na wao ndo jeshi la akiba ndo maana kila mkoa na wilaya kuna wajeda ambao ni washauri wa Mgambo
 
Ni vyema jeshi wakaona haja ya kurecruit hao vijana pindi kunapokua na uhitaji kuliko kuwapa mafunzo na kuwapigisha mzigo for years bila kuwa na uhakika wa kuwapa hizo ajira.
Huwezi shinikiza ajira jeshini lazima kea sasa ufanyiwe vetting ya nguvu hao wamejitoa wenyewe wakiwa kipindi cha kufanyiwa vetting

Wasilsumu mtu ujinga wao .Jeshi sio sehemu ya kila mti mlilia ajira
 
Hawa kwakuwa tayari wana mafunzo wanaweza kuunda vikosi vya kuasi na wakasumbua sana jeshi na amani ya nchi.Wawe makini sana.Hawa ni hatari kwa usalama wa taifa
Nadhani wamefundishwa zaidi shughuli za ujenzi. Wakitumia ujuzi huu vizuri, hawana haja ya kuiba. Kazi za kujenga zipo nyingii!
 
Tuangalie pande zote za shillingi. Tangu Mhe. hayati Magufuli awaahidi kuwa wataajiriwa imepita muda mrefu na mpaka sasa hawaajariwa. Natumaini wamefuatilia sana ili waajiriwe lakini Serikali bado ilikaa kimya. Kama Hayati Rais alitamka waajiriwe ni kwa nini hawajaariwa?. Natumaini kusubiri kwao ndo imeleta enough is enough.
 
Mimi nimeshangaa sana vijana hao kujipanga kufanya maandamano bila intelijensia ya jeshi kuwabaini mapema na kuwadhibiti.Hivi jeshi letu siku hizo likoje?
Kwan mkuu walivyo andamana kuna shida yoyote walileta mtaan kwa wakaz wa Dodoma na police walikua wapi chin ya kamanda muloto
 
Watu waliopitia mafunzo ya kijeshi ni wengi sana Tanzania, hao Iss tutawagawana kabla hata ya Mapolisi hawajaingilia kati

Tulivyopinda hivi halafu mtu aje na kilemba kutushurutisha,Magufuli mwenyewe kashindwa
Muanze kujifunza kumaliza siku bila kumtaja Magufuli. Mnamtaja mara nyingi kuliko wanavyomtaja wafuasi wake. Inaonesha mzimu wake unawatesa nyie nyumbu kuliko vile unavyowatesa wafuasi wake.
 
Hii nchi kuna kitu kikubwa kinaendelea sema hawasemi ila ipo siku Mungu atayaweka peupe.
 
Sasa vijana hawa walichoshwa na utapeli wa mzee pombe.
Anzeni kujifunza kutuma post bila kumtaja hayati. Ni ngumu ila mtazoea tu. Inavyoonesha legacy yake imepanga bure vichwani mwenu.

Viva JPM. Haters wako hawaachi kukutaja kwenye post zao huku mitandaoni.
 
Amiri Jeshi Her Excellency Madam President of URT Hon.Samia S.Hassan,please have mercy to those young Soldiers. They completed their task @building New State Houses, consider them and listen to what really happened there.
Hao ni vijana wetu,usikalie Ikulu iliyojengwa kwa dhulma ya nguvu za vijana hao.Waliahidiwa ajira je,wamepatiwa ajira/ujira waliostahili?Usikute wamewa provoke ili wapate jinsi ya kuwamwaga.Huko waendako ni salama?Kama wameasi huko mitaa kutakuwa salama?
Hawafai kuwa wanajeshi hao, askar unaitisha mgomo?, wakiingia huko si wataleta kirusi ndani ya jeshi, jeshi ni utii na uvumilivu,

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom