JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Ili tujue ukweli ni vema tusikilize upande wa pili.

Kuna stori moja ya jeshini ningeweka ila basi tu, kuna wakati watu huonewa sana kwa kisingizio cha nidhamu ya kijeshi
Jambo la muhimu ni msingi wa haki yenyewe. JKT huwa wak straight tangu siku ya kwanza kwamba hawatoi Ajira ila watu huwa wanaenda kucheza kama kamali tu.

Labda kama kuna haki tofauti wanadai.
 
Mkuu jkt toka lini kukawa na ajira? Kule huwa ni kujitolea mkuu .
Afadhali serekali ingeongeza nguvu , vijana wawe wanaenda veta kupata ujuzi kuliko huko kwenye upuuzi Wa jkt , kule Hua ni kwenda kupoteza muda Tuu,
Alafu Kazi Ya jeshi Hua ni kufuata amri tu Ya viongozi ukikaidi unakua ni uhain na unatimuliwa
 
Jambo la muhimu ni msingi wa haki yenyewe. JKT huwa wak straight tangu siku ya kwanza kwamba hawatoi Ajira ila watu huwa wanaenda kucheza kama kamali tu.

Labda kama kuna haki tofauti wanadai.
Kuna fitna kule usione watu wako na uniforms ukadhani wamepata kirahisi.

Walikuwa 2400 sasa wamepunguzwa 800+ inawezekana jeshi limefanya analysis limegundua halitaweza kuchukua wote 2400 sasa linawatoa kwenye reli kijanja.
Hii nchi usiichukulie poa vimemo kila kona mkuu
 
Ukitaka haki saaana au ukihitaji kutumia akili yako, usiwe mwanajeshi.

Hutaweza
 
kabla ya kupewa mkataba JKT mnaambiwa kabisa..JKT haitoi AJIRA bali inatoa mafunzo ya uzalendo na kujiajiri..Wewe unaamua kukubali afu usipoajiriwa unalalamika
 
Orodha na majina ya hao waasi iko wapi ili watanzania wawe makini nao
 
Suala hili likifumuliwa tutaona mengi.
 
Kugoma ni UASI na hiyo kitu ni hatari..emu fikiria Mtu wa namna iyo unamuajiri Awe askari kamili...uyu anaweza kumsikiliza mkubwa wake?..
.na adhabu za kufanya mgomo jeshini kwa askari kamili iwe kukataa amri kutoka kwa mkuu wako adhabu yake uwa ni kufukuzwa jeshini, kufungwa na inategemea wapi umegoma muda mwingine adhabu huwa ni KIFO
 
Mwendazake aliwadanganya watoto wa wenzake huku akiwafanyisha Kazi kama ma cheapest labour kwenye ujenzi kwa ujira wa wali maharage kwa ahadi ya ajira.This is too bad.
 
Uliwahi kuajiriwa jeshini?
Kama hukuwahi nyamaza tu
Kuna watu wanaonewa na wakubwa wao mpaka mtu anakosa uvumilivu anakoki silaha jeshi lisikie kwa watu, kama upo huko basi uko position ya juu huonewi ndio maana uko comfortable
 
Lakini hao sio wanajeshi awajaajiriwa.
 
Uliwahi kuajiriwa jeshini?
Kama hukuwahi nyamaza tu
Kuna watu wanaonewa na wakubwa wao mpaka mtu anakosa uvumilivu anakoki silaha jeshi lisikie kwa watu, kama upo huko basi uko position ya juu huonewi ndio maana uko comfortable
Kiapo kinasemaje bro?
Utatekeleza yale yote utakayopewa na mkubwa wako..kama unaonewa nenda kashitaki kuna sehem za kupeleka malalamiko..hiyo ndo maana ya UTII, UAMINIFU NA UHODARI
We toka uzaliwe ushawahi sikia wapi askari anagoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…