JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Nchi nyingi zilozoendelea wamewekeza vyema kwenye ulinzi(jeshini)

Ukichukulia mfano marekani, urusi au China

Hawana maigizo kuhusu masuala ya ulinzi

Kama wanajua hawawezi kuwaajiri hao vijana jeshini kwa nini wanawasajili kwenye mafunzo hayo ya JKT

Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) hili ni sehemu ya jeshi kwenye wizara ya ulinzi


Dhumuni la kuanzishwa na jeshi hili ni kuwajengea vijana stadi za kiufundi na uzalendo kabla ya kuajiriwa rasmi kwenye jeshi la wananchi(JWTZ)

Ila kinachotokea sasa hawa vijana wanasajiliwa na kupata mafunzo haya baadae wanarudishwa mtaani bila hata vyanzo au mtaji kuendelea kujikimu au kuendeleza kile walichofundishwa huko jeshini


Kama hawawezi kuwapa hao vijana ajira sioni sababu ya kusajili vijana wengi wakati wanajua hawana uwezo kwa kiwaajiri kuliko kuwapotezea muda
 
Mutiny kwa askari yoyote ni kosa kubwa sana, sio Tanzania pekee duniani kote nidhamu ndio inayojenga askari imara.
 
Bahati mbaya sana. Maandamano jeshini hii kali kuliko? Huu si uasi ? kwa hatua walizo chukuliwa ni kielelezo tosha kuwa Taifa hili Mungu wa mbinguni kalijalia baraka ya Amani. Huko kwengine kama iran au korea kaskazini wangefanyiwa mazoezi ya kulenga shabaha.
 
Mwendazake aliwadanganya watoto wa wenzake huku akiwafanyisha Kazi kama ma cheapest labour kwenye ujenzi kwa ujira wa wali maharage kwa ahadi ya ajira.This is too bad.
Kazi si ndiyo kujitolea na kufundishwa ukakamavu
Jkt haitoi ajira

Ova
 
Halafu ujue vijana 800 ni sawa jeshi la nchi kwa baadhi ya nchi hapa duniani
Kwanza ujue mafunzo yao ni elementary sana, jeshi haliwapi mafunzo bila tahadhari, ndio maana hata ndani ya jeshi kuna makomando ambao wanaweza kudhibiti uasi wa jeshi lenyewe ikitokea sembuse JKT?
 
Shida kubwa wengine wanaongea bila kuangalia uhalisia wa mambo na hawajui kinachoendelea kisa uongo uongo adi jeshini. Makosa ya namna ya kuajiri vijana toka jkt ilianza baada ya uongozi wa awamu ya tano kuingia.
Vijana wanapmaliza mafunzo ya miezi sita ya awali walikua wanatawanyishwa kwenye makambi mbalimbali yaliyopo chini ya jwtz kwa ajili ya uzalishaji mali na ulinzi kama sehemu ya malezi.

Wakiwa kwenye makambi ya malezi ndipo jeshi..magereza..usalama..bot..takukuru n.k wanakwenda kufanya recruitment wa vijana hawa kulingana na sifa wanazohitaji pindi wakiwa na uhitaji na kwa kwenda kwenye makambi yote ya malezi.

Shida ikaanzia kipindi cha magufuli; yeye alitoa amri wa kuajiriwa waliojenga Ukuta Marerani lakini waliokua wanalima mpunga Chita..wanaolinda mipaka huko Kigoma na Uganda na Rwanda hakuona kama wanasifa ya kuajiriwa..waliokua wanalima mahindi huko Mgambo Tanga hakuona kama wanastahili kuajiriwa sijui alifikiri wote waje Mererani kujenga ukuta bila kuwepo mgawanyo wa ki majukumu.
CDF na mkuu wa jkt wakajikalia kimya bila kuona kuna upendeleo kwenye ajira.

Watu wenye uwezo wakawapanyika vijana wao humo humo na ikawa rushwa ndani ya jeshi.
Ujenzi ulipoanza tena Chamwino stori ikawa ile ile waajiriwe wanaojenga ukuta..hao CDF na mkuu wa jkt wakawa kimya tu; vijana waliopo makambi ya mbali wakawa na vilio mbona wanaajiriwa wa Dodoma tu? then wenye michongo wakafanya wanavyojua vijana wao wakaja nao Dodoma kwenye ujenzi.

Uchaguzi ulipowadia pia wanachukuliwa vijana kwenda kuaribu uchaguzi kwa upendeleo huohuo kua wataajiriwa.

Sasa leo wanawaona kama wanaketa uasi. Swali ni je kwanini hawakushauri Magufuli kipindi hicho kuhusu ajira? wamwambie kua wao wanataratibu zao za kuwapatia vijana wa jkt ajira?
Mambo ni mengi ngoja niishie hapa.
 
Fukuza wote,unagoma jeshin?aliyewadanganya kakosea sana.
 
Sasa nchi inaendeshwa kwa kanuni, sheria na taratibu, Watanzania inabidi tuelewe.

Raia inabidi tufahamu sio wote wanaojiunga na JKT wana sifa za kujiunga na JWTZ.

Wanataka kulazimisha kwamba wapo kwenye mafunzo ya JKT ni lazima waajiriwe na JWTZ. Ingekuwa hivyo hakina Zitto. Mdee na wengine sasa hivi wangekuwa wamehajiriwa JWTZ!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
China, S. Korea, Israel, N. Korea, Kijana yeyote akifikisha umri wa miaka kuanzia 17-19 shariti ajiunge na national service (I.e JKT kwa TZ), lakini siyo kwamba, akihitimu ndo anaajiriwa, ingekuwa hivyo basi kwa nchi hizo RAIA wote wangekuwa wanajeshi.

Tangu mwanzo tangazo la kujiunga na JKT huwa liko wazi kuwa hawatowi ajira bali ni mafunzo ya hiyari na kujitolea. Sema Mara nyingi 30%- 50% ya wahitimu wa mafunzo huajiliwa na idara mbali mbali za jeshi ikiwemo; JWTZ, polisi, magereza, Tanapa, zimamoto n.k. Lakini ieleweke kujiunga JKT ni kupata mafunzo ya ukakamavu, ujasiri, uzalendo, uzalishaji mali na kujitegemea.
 
Ni haki kuwa na wasiwasi lakini hali halisi ni kwamba once wamefukuzwa hule umoja wao huwa unakufa hapohapo kutokana na kutawanyika kwenye makazi yao tofauti tofauti na huwa wanaamriwa kuripoti kwa viongozi wa serikali kwenye maeneo wanayofikia.
Kwa sababu hiyo huwa wanafuatiliwa mienendo yao since day one wanaporipoti
 
True! Niuasi huo!
 
“Tarehe 8 Aprili 2021, vijana wa Jeshi la kujenga Taifa wapatao 2,400, walio haidiwa kupewa ajira na Mhe. Rais kwa kutekeleza ujenzi wa ofisi za ikulu ya Chamwino waliamua kugoma, kukataa kufanya Kazi eneo jingine na kuandamana kwenda Ikulu kumuona Mhe. Rais kushindikiza kuandikishwa Jeshi. Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbunge kawasihi kusitisha mgomo huo na kutoandamana hawakusikiliza.

Kitendo hiki haikikubaliki, kugoma au kuandamana Jeshini ni kosa la Uasi , wangekua askari wangefikishwa mahakamani kwa sababu hiyo Jeshi la kujenga Taifa limesitisha mkataba wa vijana hao 854 wa kujitolea na kurudishwa makwao.” Jen. Mabeyo


 
Ukisikia baadae watu wamejinyonga ndo hapo .....mtu AME hustle zile SIX WEEK afu anafutwa. Mungu awape moyo wa ujasir
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…