JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Kwa yoyote aliyepita jeshini anafahamu kuwa kosa la KUGOMA AU KUANDAMANA jeshini ni KOSA KUBWA. Ni UASI. Na kila siku tunawaambia kwamba mafunzo ya JKT ni ya kujitolea na sio sehemu ya ajira. Na kwa taarifa yenu vijana waliotumikia jkt na kurudi mtaani baada ya kumaliza muda wao ni wengi zaidi ya hao na wanaendelea na maisha mengine. Watumie skills za jkt kujiajiri na kuzalisha mali. Jeshini ni amri,subra,ukakamavu,uzalendo na uvumilivu
 
Ukisikia baadae watu wamejinyonga ndo hapo .....mtu AME hustle zile SIX WEEK afu anafutwa. Mungu awape moyo wa ujasir
Miaka 3 mkuu sio 6 weeks

Aisee ktk ujinga wanafanya service man ni huu yaani woote uwa wanawaza kuingia Jwtz tu ssa watachukua wangapi wataacha wangapi ata polisi,maliasili wakienda kambini kufanya usaili mijitu inakimbia kujificha eti wanasubiri JW waje wafanye usaili dadek acha WANYOOKE na WATANYOOKA TU
 
Karibu kitaa walio rudishwa
 
Vijana wajinga sana, Jeshi linahitaji uvumilivu. Ajira kwao lilikuwa ni jambo la muda tu. Huku jeshini kosa la kugoma tu hata dkk moja unakuwa umedisco. Tena bado vijana wadogo sana. Nendeni mkajifunze nidhamu
 
Anzeni kujifunza kutuma post bila kumtaja hayati. Ni ngumu ila mtazoea tu. Inavyoonesha legacy yake imepanga bure vichwani mwenu.

Viva JPM. Haters wako hawaachi kukutaja kwenye post zao huku mitandaoni.
Wajane mna tabu sana.
Naona na wewe umepost bila kumtaja marehemu pombe🤣🤣🤣
 
Kwani ISS Mozambique wing wametangaza nafasi za kazi?
 
Naona mkono wa chadema au TLS au wa askofubagonza. I cannot imagine mwanajeshi afanye maandamano unless wamepikwa wakapikika wakadai "haki zao za kikatiba", askofu huziita uhuru na maendeleo. Mlete tundulissu awatetee
 
Hawa kwakuwa tayari wana mafunzo wanaweza kuunda vikosi vya kuasi na wakasumbua sana jeshi na amani ya nchi.Wawe makini sana.Hawa ni hatari kwa usalama wa taifa
JKT wanapewa sehemu ndogo sana ya mafunzo ya kijeshi ndiomaana hata wale wanaopata bahati ya kuajiliwa jeshini lazima waende mafunzo tena

Kumbuka wale vijana waliokufa wakati wa mafunzo pale pwani mwaka Jana tukaambiwa walikula vyakula vyenye sumu mtaani....wale ni miongoni mwa wale vijana wa JKT waliojenga ukuta wa mererani
 
Umewaza vizuri sana mkuu.
Kuna watu humu kazi yao kuwaponda vijana wameasi wameasi bila kufikiri chanzo cha tatizo.
Alaf askari akiasi harudishwi nyumbani si kuna adhabu za kuuwawa na kufungwa? Mbona hawajafanya ivo?
Hapa ilitafutwa mbinu ya kuwatimua tu.
Walijua kabisa 2400 nafasi hamna kwa vyovyote hawa 800+ tukiwarudisha vikosini lazima wataleta kelele kwahiyo kelele zao zitatupatia mwanya wa kuwafukuza kwa justification ya kuasi.

Jkt imekuwa tofauti sana kama hujaenda kwenye ujenzi basi sahau ajira ilihali kuna watu walibaki vikosini kulima, wako sawa na waliokwenda kujenga sasa kwanini waliojenga ndo wapewe kipaumbele? Shida ilianzia hapa
 
Gharama kubwa zilizotumika kuwaandaa hao vijana ili kuja kulitumikia taifa zinarejeshwa vipi?
Kwani hata ukisoma mpaka kuwa Professor halafu ukafanya makosa unaweza futwa kazi na hata kufungwa .Haijalishi ulitumia gharama kiasi gani mpaka kufikiwa kuwa professor!
 
Wenye madaraka wana roho mbaya sana sijui ni damu za wapi hizo...wakipata wao ajira hawawafikirii wengine hata kidogo zaidi wanatamani kuongeza miaka ya kufanya kazi bila hata kutaka kustaafu ubinafsi tuu umewajaa...
 
Tatizo la mifumo mingi ya kijeshi na kiusalama hasa katika bara la africa huwa hawataki kuhojiwa wala kutaka watu wapate taarifa za ukweli au upande wa pili, Uasi ni suala pana sana hapo ni kwamba walikiuka taratibu za kinidhamu, lakini pia hawa vijana wametumika sana katika mambo mengi, Ukweli ni kwamba pamoja na hili jeshi kuonekana mbele za watu wana sifa mzuri sana, ila ukija ndani yake wao kwa wao kuna michezo yao mingi huwa wanaicheza tatizo hakuna chombo huru kinachoweza kuhoji au kuuliza ila yapo mambo yanahitaji majibu kwa kina pia mabadiliko makubwa yanahitajika katika mfumo wa hili jeshi ili kuendena na dunia ya sasa ilipo kuanzia jkt mpak JWTZ
 
Jambo jingine linalonishangaza ni kuwa vijana hawajui kuwa kuingia jeshini ni kusaini kuwa wakati wowote upo tayari kufa kwa risasi au bomu. Wao nadhani wanafikiri kujiunga na jeshi ni kwenda kula bata ndiyo maana wanalazimisha kuajiliwa.
Wao si wanawaona wenzao wanavyokula bata?
Anyway,wamewarahisishia wenzao waliobaki,kupata ajira fasta.
Jeshi liimarishe intelijensia ya kubaini mambo kama hayo kabla hayajatokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…