JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Hawa kwakuwa tayari wana mafunzo wanaweza kuunda vikosi vya kuasi na wakasumbua sana jeshi na amani ya nchi.Wawe makini sana.Hawa ni hatari kwa usalama wa taifa
 
Jkt ni kujitolea alafu wanalazimisha ajira
Wanaandamana wakati kazi yao ni kupokea amri
Walitakiwa wawe wavumilivu hata kama kweli walikua wasiajiriwe wamewapa watu sababu kwa kuandamana kwao
 
Sawa jiaminishe ivyoivyo watakapo anza kuchinja ovyo watu mtaani ndo utajua umuhimu Wa kuwaajiri hawa vijana.
Sasa unaajiri mwanajeshi aliyegoma? Bado hawajapewa ajira ila wamejioganise na wamechagua kiongozi kisha wakagoma, Unajua tafsiri yake kijeshi na kiusalama wa nchi?

Umejiuliza kwanini sababu imetajwa kuwa ni uasi?

By the way, waliingizwa jeshini na nani na kwa nia gani? Huenda siasa iliingizwa jeshini.
 
Jkt ni kujitolea alafu wanalazimisha ajira
Wanaandamana wakati kazi yao ni kupokea amri
Walitakiwa wawe wavumilivu hata kama kweli walikua wasiajiriwe wamewapa watu sababu kwa kuandamana kwao
Kuna sehem katika clip ya mabeyo kasema kuwa waliahidiwa ajira.Au Mimi ndio sijasikia vizuri?
 
Yaani watu wanapodai haki zao ndiyo uasi! Bora tu niliahirisha kwenda Monduli enzi zile. Maana mpaka muda huu ningekua nimeshambamiza mtu risasi ya kichwa.
Bora hukwenda maana unaonekana hufai kuaminiwa hata kwenye Ulinzi Shirikishi. Yaani unaunga mkono Askari Kugoma na kuandamana.

Halafu eti umeweka Picha ya Nyerere hapo.
 
Sasa unaajiri mwanajeshi aliyegoma? Bado hawajapewa ajira ila wamejioganise na wamechagua kiongozi kisha wakagoma, Unajua tafsiri yake kijeshi na kiusalama wa nchi?

Umejiuliza kwanini sababu imetajwa kuwa ni uasi?

By the way, waliingizwa jeshini na nani na kwa nia gani? Huenda siasa iliingizwa jeshini.

Mkuu hawajajua askr kugoma hii ni picha mbaya hta kwake raia na nnchi kwa ujumla uliza nnchi zenye vikosi vya uasi inakuwaje afuu unakuja hapa unashabikia ujinga
 
Nimesoma habari moja kuwa JKT imesitisha mikataba na kuwafukuza vijana zaidi ya 800 baada ya kuandamana Ikulu wakinishinikiza kuajiriwa

Baada ya hao vijana kuja mtaani,wanajua kushika silaha na mafunzo ya awali ya kujihami,je hao vijana hawawezi kujiunga na vikundi vya kigaidi kama cha ISS huko Msumbiji?

Je serikali inawafuatilia hao vijana zaidi 800 mienendo yao mitaani kama sio rahisi kushawishika kujiunga na vikundi vya kigaidi kwa ukosefu wa ajira na kuleta majanga nchini?

Au unaweza ukawa mtego,wakashawishiwa kugoma wadai ajira ili watimuliwe wakajiunga na ISS huko Msumbiji


Serikali ibuni mikakati ya kuajiri vijana au kuwawezesha kupata mazingira rahisi kujiajiri ili kuepuka kushawishika kuvuka mpaka kule kusini na kujiunga na ISS

Narudia kuwatimua vijana 800 JKT ni hatari zaidi kwa usalama uliopo kusini mwa Afrika
Ziko oparations kibao uraiani huko tangu 2012 hawana kazi tena ni wengi kuliko hata hao waliojiunga suma jkt kwa shughuli za ulinzi.
Hivi ulibahatika kuona ule mtiti uliokusanyika pale ilala ofisi ya aliekuwa mkuu wa mkoa p. Makonda?
 
Kwa kichapo walichopata hawatakuja kusahau, nasikia walikomaa wanataka kwenda msata kuhenya hapo washamgomea Mbuge wanataka onana na Samia tu, zikaletwa karandinga haya pandeni mwende msata kufika msata MP Kama wote wanawasubiria, wakapata kipigo heavy na kusafirishwa makwao.
 
Siwafundishi kazi, bali naamini taalamu yenu inawataka mfanye hivyo na si kuishia kupata taarifa za upande mmoja tu kwa maana ya maelezo ya viongozi wa Jeshi na serikali tu bila kuwahoji Vijana waliofukuzwa.

Wateendeni haki hawa vijana ili umma uweze kuwahukumu kwa haki maana teyari wameshaitwa waasi(sifa mbaya sana katika Jamii na kila watakokwenda).

Mazingira ya kufukuzwa hawa vijana, kwa mtazamo wangu, hayana tofauti na mazingira ya wale vijana waliofukuzwa UDOM na hayati Magufuli mwaka 2017.

Yangu ni hayo tu.
 
Ndio maana huwa wanawasafirisha. Labda waungane kupitia WhatsApp
Sidhani kama walipitia mafunzo kamili ya kijeshi, hakuna mwanajeshi aliyekamilika kimafunzo anayegoma kirahisi rahisi na kuandamana. Wale ni watii 100% wa maagizo ya Jamhuri maana wanajua tafsiri ya neno uasi.
 
Back
Top Bottom