Nimesoma habari moja kuwa JKT imesitisha mikataba na kuwafukuza vijana zaidi ya 800 baada ya kuandamana Ikulu wakinishinikiza kuajiriwa
Baada ya hao vijana kuja mtaani,wanajua kushika silaha na mafunzo ya awali ya kujihami,je hao vijana hawawezi kujiunga na vikundi vya kigaidi kama cha ISS huko Msumbiji?
Je serikali inawafuatilia hao vijana zaidi 800 mienendo yao mitaani kama sio rahisi kushawishika kujiunga na vikundi vya kigaidi kwa ukosefu wa ajira na kuleta majanga nchini?
Au unaweza ukawa mtego,wakashawishiwa kugoma wadai ajira ili watimuliwe wakajiunga na ISS huko Msumbiji
Serikali ibuni mikakati ya kuajiri vijana au kuwawezesha kupata mazingira rahisi kujiajiri ili kuepuka kushawishika kuvuka mpaka kule kusini na kujiunga na ISS
Narudia kuwatimua vijana 800 JKT ni hatari zaidi kwa usalama uliopo kusini mwa Afrika