JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Ukosefu wa ajira ,ajira ,ajira na kunyima haki,uonevu ni chanzo cha kuibuka kwa vikundi vya kigaidi duniani,Note my words
Ni kweli ajira ndiyo huchochea vijana kuwa occupied na mambo ya maendeleo na kutojihusisha na mambo ya uvunjifu wa sheria, lakini kitendo walichokifanya hao vijana ni cha hatari sana, huenda wangeenda mbali na hata kufanya mapinduzi ya kumpindua raisi.
 
Dhana ya uasi ni pana sana na ipo kimkakati sana.
Tushukuru Mungu kuwa amani nchini imetamalaki na hakuna wala dalili za uasi nchini kwetu.

Siyo kwamba madhara hayapo kwenye uamuzi huu, yapo hata kama hayaonekani moja kwa moja.
 
Inasikitisha na kuumiza sana Mkuu. Jasho lao halitokwenda bure. Mungu anawaona waliowadhulumu Vijana wale. Eti fanyeni kazi kwa bidii kisha Ujenzi wa Ikulu utakapomalizika basi mtaajiriwa kwenye Vikosi mbali mbali vya Majeshi yetu. Leo wamekuwa Waasi?? Au kwakuwa kazi yao imeisha??
 
Kwa tetezi nasikia wamefanya kazi zaidi ya miaka 3+, wamejenga Chamwino, Ukuta wa Mererani, majengo ya magereza Ukonga, ndio walio ratibu wizi wa kura na usimamizi wa uchaguzi 2020 na n.k, pia waliahidiwa baada ya kumaliza shughuli zote hizo watapewa ajira jeshini lakini baadae upepo ukageuka na ndio maana walifanya mandamano kwenda Chamwino.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mfumo wa maisha ambao kuuvunja ni vigumu! Ni awamu ya marehemu Magufuli watu kutoka familia za "kawaida" waliweza kuajiliwa usalama wa taifa, JWTZ, TRA, BOT na kadhalika.
Enzi zetu zikitangazwa nafasi za Polisi au Jeshi unashangaa watu kutoka Dar es salaam, Moshi, nk wanakuwa wazaliwa wa Kwimba!
"...aliyenacho ataongezewa na asiye nacho hata kile kidogo alichonacho atanyanganywa..."
 
Kama waliandamana baada ya kugeukwa, hiyo ni sahihi kabisa.

Hata hivyo, ndio wajifunze kuwa CCM sio wema.
 
Hata watumishi wote waliokuwa wameshauriwa ikulu na mwendazake mtasikia wametimuliwa wote wameshauriwa wengine wapya wa dini ile
 
Meko alitoa ahadi ya kuwaajiri Kwa Mhemuko. Kumbe kiuhalisia Jeshi halikuwa limejipanga kuwaajiri..
 
Ila mkataba unasema hawakuahidi ajira.
 
Ngoja kwanza vuguvugu hili liishe na ionekane hakuna msukumo uliyowapekea wafanye hivyo ila ni kweli kama wanavyodai basi mama Samia anaweza kuwaonea huruma na kuwarudisha kwani toka raisi aingie madarakani kuna tetesi za kuwepo baadhi ya watu wasiyo waaminifu kutaka kuleta fujo, na nadhani ilimpelekea hata mama Samia mwenyewe kusema na kunukuliwa kuwa "huyu aliyesimama hapa ndiye raisi". Hivyo hivi vitu tusivione ni kama kuwanyanyasa hao vijana lakini nidhamu na utii wa sheria lazima ufuatwe.
 
[emoji848]hivi wakisharudi Nani atawaajiri wakati tayari ni waasi?
 
Vijana wameonesha ushujaa wa Hali ya juu Sana, tutegemee kuona mabadiliko siku zijazo kuhusu ili swala, sela Mbovu za mwenda zake zimeharibu vijana, zimetukosesha nguvu za kiume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifuatilia vizuri maelezo ya mabeyo,anasema Kama wangekuwa ni askari wangefikishwa mahakamani,swali ni je, Kama sio askari wanaitwaje waasi?
Kama sio askari wamezuiliwaje kuandamana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…