TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sana maisha mafupi dear
Enzi kile kigrocery pale makaburini kino kwa mzee maende sahv breakpoint,ndugai alikuwa anasogea sana wao wanatokea pale ndani mwembe jini kwenye zile ofisi,nkajuana naye na wkt huo nafanya clearing vijana wa mjini wkt huo tunatamba,nshamtolea gari zake kadhaa,mara ehh kawa mb mara spika 😄

Kifo kiboko ya mwanadam kweli

Ova
Alikua mmoja wa watu wa ile ofisi mwembejini!?.. kweli vyeo tz wanapewa wao tu!!..nchi ngumu hii
 
Vita Inakua Kali.

Kwa mara nyingine Wana mtandao wamefanikiwa kumuondoa Moja ya Mzalendo wa Taifa.

KOSA MOJA ALOFANYA NDUGAI, ni kutojiamini katika Kila anachokisema.

Anasema Leo hivi, kesho anaomba MSAMAHA.


Hii Majuzi wakati Samia anaahirisha Mkutano wa Wajumbe na kutimkia Zanzibar, zipo taarifa za uhakika kua Wazalendo walitaka kutoa Hoja ya kumuondoa Samia .



Ndugai alipoona Samia Kastuka nankukimbilia Zanzibar, akaanza Tena kuomba omba MSAMAHA.


Wamemuacha aingie kwenye Mbionza utia Nia, kwenye Kampeni kapigwa Tukio.

Leo Kafa.


Wazalendo Tujifunze namna ya Kupambana na vita za watu wahuni.

KOSA hilihili pia ndio ALILOFANYA MAGUFULI .


Nimeumizwa sana na Kifo Cha Mzalendo huyu.
 

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Mod hapo kwenye wasifu angalieni mrekebishe miaka. Naona inaonyesha primary school alisoma 1991 hadi 1997
 
Maisha ya mwanadam ni mafupi sana!!. Rip kwake l, lkn kama amekufa hajatubu makosa ya kumnyanyasa Lissu na Kufanya ukandamizaji dhidi ya Raia bado na mzigo mzito mbele za mungu!!.

Lissu bado ana dunda na watesi wake wawili sasa hatunao hapa Duniani!.
 
Huyu ndio alisema Lissu ni mtoro bungeni na hajui alipo huku watu wote pale bungeni walijua Lissu alikuwa akijiuguza na operation zaidi ya 20 uhamishoni tena kwa msaada wa wasamaria wema.

Sio pesa yake ya matibabu wala stahiki nyingine za kibunge zililipwa.

Tutawakumbusha hata msipotaka hatuwezi kufukia uovu alikuwa na nafasi ya kuwa na ubinadamu ila akafuata madaraka kwanza kumfurahisha Magufuli.

Magufuli akamwambia washugulikie humo ndani wakitoka nje mimi nitawashughulikia nje huku.

Haya leo nguvu na mamlaka hayo wote wawili hawana na hawapo.


View: https://youtu.be/UKdf8ecyhQs?si=2wyg-nq0N0Up4kxy

Yeye na mwendazake walitaka Lissu asipone au afe kwa msongo wa mawazo wakati anajiuguza. Ndiyo maana walikuwa wanamfanyia mambo ya hovyo
Wote wamekufa wamemwacha Lissu anadunda.

Hata aliyemtengenezea kesi ya uhaini atakuwa atamwacha Lissu.
 
Back
Top Bottom