TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
PRO wa bunge hayuko serious kuhusu wasifu wa Marehemu Ndungai;
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997🙄
 
Hapo kwenye Miaka ya elimu ya msingi kuna typo error
 
kupata elimu yake ya msingi na sekondari katika shule mbalimbali za Tanzania. Alihitimu kutoka shule za msingi na baadaye shule za sekondari ikiwemo Old Moshi Secondary School.

Baada ya hapo, alisomea Diploma ya Usimamizi wa Wanyamapori katika Mweka, kisha Shahada ya Sayansi (BSc) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Shahada ya Uzamili (MSc) kutoka Chuo cha Kilimo cha Norway. Aidha, alipata Shahada ya Uzamivu wa Biashara (MBA) kupitia ESAMI, kujiandaa vyema kwa uongozi.

Job Ndugai alianza siasa kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Kongwa mwaka 2000 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliendelea kupandisha hadhi mpaka mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania. Mwaka 2015, alichaguliwa rasmi kuwa Spika wa Bunge, na aliendelea kushikilia nafasi hiyo kwa muhula wa pili mwaka 2020.

Mnamo Januari 2022, Job Ndugai alijiuzulu kutoka nafasi ya Spika wa Bunge baada ya mzozo kuibuka kati yake na serikali kuhusu mjadala wa deni la taifa na suala la matumizi ya madaraka bungeni. Kujiuzulu kwake kulitokea katika hali ambayo alihisi kutokuwa na msaada wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake kama Spika.

Hayati Job Ndugai atakumbukwa kwa uongozi wake thabiti na mchango wake mkubwa katika siasa za Tanzania.
 
Shikamoo pesa.Maaskofu kibao waongoza ibada ya kuaga maiti ya Ndugai ibadavinsyoonyeshwa Live TBC

Kwenye pesa kila kitu kinawezekana
 
Back
Top Bottom