Nimepitia posts zilizowekwa hapa, nimegundua kuwa Watanzania wengi siku hizi hawajui kuwasiliana kwa kutumia mitandao, wanatumia lugha ambazo si za kistaarabu. Sijui huwa ni matokea ya frustrations za maisha au vipi, ila wengi hutumia mitandao kuandika pumba sana. Kuna mifano hata nje ya hapa JF inayoonyesha ninalozungumzia:
(4) hapa JF watu huandiaka matusi kila wakipishana mawazo: maneno; mpumbavu, mjinga, fala, bwege, na kadhalika yamekuwa ya kawaida sana kwenye mijadala hapa. Kuna sehemu moja kwenye psychology inayosema watu wenye upungufu fulani wa akili huwa ni wepesi wa kutumia lugha kali za matusi ili wasionekane kuwa wana upungufu wowote.