Julius Nyerere alikuwa mtu sahihi kupewa nchi kwa mazingira ya kipindi kile

Chan...
Nije na jibu kwani mimi ndiye niliyewafuta katika historia?

Mimi baada ya kuona hayo majibu yangu kwa historia hiyo iliyokuwa na upungufu mkubwa ni kitabu nilichoandika nikawataja wale waliofutwa.

Leo tuko hapa tunaijadili historia hii.
Una-majina yao ya hawa watu ambao nyerere aliwa-cancel unaweza waorothesha majina yao
 
Itapendeza ikiwa utasema wanahistoria badala ya Nyerere kwani ikiwa yeye hakuwataja popote katika maisha yake wanahistoria wangeweza kuwataja.

Alipofariki Abdul Sykes magazeti ya TANU Uhuru na Nationalist hayakuandika chochote kuhusu yeye lakini Tanganyika Standard katika gazeti lake la Sunday News 20 October, 1968 walichapa taazia yake:

1707129248348.png

mbona alimtaja kawawa
 
Uandishi sio mzuri mjitahidi
Kabla ya Julius Nyerere hajawa kiongozi wa TANU na hali ya siasa za Tanzania zilikua kama ifuatayo;-

Changamoto kubwa ya TAA na baadae TANU ilikuwa ni power struggle kila mtu alikua anataka awe kiongozi na hakuna mtu aliyeweza kuunganisha wanachama ambao walikua makundi makundi. Hii ilipelekea TANU kuwa na wakati mgumu sana sababu kama hamna maelewano kabla hata ya uhuru mkija kupewa nchi itakuaje

Hakuna kiongozi wa TANU aliyekua na maono mapana ya kuunganisha nchi kwani wengi wao walidhani wanadai uhuru wa Dar es Salaam, walikua na ufahamu na nchi nzima ili hawakuwapa uzito maeneo mengine ya nchi.

Changamoto lingine ni swala la udini, viongozi wa TANU walitaka nchi kuwa ya kislamu na kuongozwa kislamu kitu ambacho mkoloni alikikataa sababu walitaka mtu atakaye leta usawa kwa dini zote kumbuka kabla ya uhuru waislamu walikua asilimia 35 na wakristo 30 na ndio mara ya mwisho Tanganyika kufanya sensa kujumuisha kipengele cha dini.
Na concern kubwa sana ya mkoloni ni swala la udini sababu kuna kosa alilifanya India na Pakistani hakutaka tena lijirudie Tanzania swala la usawa kwa dini zote alilichukulia kwa uzito mkubwa sana

Mkoloni aliwapa masharti kabla hawajarudi tena ku-discuss juu ya uhuru wawe wamesha-sort out juu ya swala la uongozi kwa sharti la awe mkristo, amesoma na mwanachama hai wa TANU kwa hiyo bila kupenda ikabidi wamchague Julius Nyerere

Nyerere kuwa kiongozi wa TANU ni uamuzi wa kutokupenda kwa wapigania uhuru na ndio the only best choice ambayo ilikuwepo kunauwezekano wako ambao walikua wazuri zaidi kwa kigezo cha elimu na uongozi zaidi ya Julius Nyerere ila wengi wao walikua ni wachungaji na mapadre kwa hiyo ingewawia vigumu kuunganisha nchi

Kwa hiyo Nyerere na mapungufu yake alikua ni mtu sahihi kupewa nchi kwa mazingira ya kipindi kile
Kwahiyo waislamu walianza kubaguliwa kabla ya uhuru na mzungu aliogopa nchi ingekuwa ya kiislamu asipomuweka mkristo, au sio?

Haiingii akilini watu waliobaguliwa toka na wazungu, pia wawe ni wachache na bado muogope kuwa wataifanya nchi kuwa yao! ... Muslims have always been a majority in TZ, lakini hamtaki kusema!

Na hii ina-make perfect sense kwanini revolution ya Zanznibar na muungano immediately after that. Hii ikifuatiwa na kuwaundia waislamu Bakwata (chombo cha kuwa-limit na kuwa-control), simultaneously kustawisha taasisi za kikrsito (TEC), na hapo baadae kwenda kumpiga Iddi Amin kwa kigezo eti katuvamia kumbe kuna udini ndani yake.

Ukirudi nyuma zaidi utaona kabla ya kuja hao waingereza walikuja wareno na walikuta dola za kiislamu pwani yote ya Afrika mashariki.
 
mbona alimtaja kawawa
Chan...
Prof. Haroub Othman akitaabishwa sana na maswali mfano wa haya unayouliza wewe.

Hii ndiyo sababu aliomba miadi azungumze na yeye kuhusu kitabu cha Abdul Sykes:

Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli kutoka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU.

Ally Sykes ana stakabadhi ya hundi ya posta toka kwake kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru mwaka wa 1953.

Ally Sykes ana nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa.

Ally Sykes ana barua ya mwaka 1952 kutoka kwa Rashid Mfaume Kawawa akiwa Bukoba aliyomwandikia kumfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa.

Ally Sykes ana barua ya mwaka 1963 kutoka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

1707145347701.jpeg

1707145127225.png

1707144869422.png

Moja ya Nyaraka za Sykes​
 
We jamaa bwana!!..sensa ya mkoloni 1958 waislam ni 66%,sensa ya pili yenye kipengele Cha dini 1968 ikatoa hayo matokeo yako,huko duniani tukaulizwa waislam wamekutwa na janga gani wameisha kiasi hiki!?..tukaduwaa,tuliporudi tukafuta kipengele Cha dini Hadi Leo, wakatoliki wanadai wapo 13m,walutheri 8m..nchi Ina watu 65m,hapo wengi dini gani!?
TANU/TAA ilikuwepo mpaka tabora,waikela wa tabora alimshinda Nyerere kwenye kura, TANU ilikuwepo pwani kote,KAGERA..unakuja unasema TANU haikua kitaifa!!
Nyerere aliyapenda tu Sana madaraka,alipiga marufuku vyama vingi,akafunga waliomtambulisha na kulazimisha akubalike kwenye siasa,akaitumbukiza nchi kwenye umasikini na sera ya ujamaa baada ya kuvuruga miji iliyokuwepo nk
Kiukweli mikoa yenye waislamu wengi ni Lindi,mtwara,pwani,Tanga,Tabora na kigoma sasa hiyo 68% walifikaje?
 
Uandishi sio mzuri mjitahidi
Kabla ya Julius Nyerere hajawa kiongozi wa TANU na hali ya siasa za Tanzania zilikua kama ifuatayo;-

Changamoto kubwa ya TAA na baadae TANU ilikuwa ni power struggle kila mtu alikua anataka awe kiongozi na hakuna mtu aliyeweza kuunganisha wanachama ambao walikua makundi makundi. Hii ilipelekea TANU kuwa na wakati mgumu sana sababu kama hamna maelewano kabla hata ya uhuru mkija kupewa nchi itakuaje

Hakuna kiongozi wa TANU aliyekua na maono mapana ya kuunganisha nchi kwani wengi wao walidhani wanadai uhuru wa Dar es Salaam, walikua na ufahamu na nchi nzima ili hawakuwapa uzito maeneo mengine ya nchi.

Changamoto lingine ni swala la udini, viongozi wa TANU walitaka nchi kuwa ya kislamu na kuongozwa kislamu kitu ambacho mkoloni alikikataa sababu walitaka mtu atakaye leta usawa kwa dini zote kumbuka kabla ya uhuru waislamu walikua asilimia 35 na wakristo 30 na ndio mara ya mwisho Tanganyika kufanya sensa kujumuisha kipengele cha dini.
Na concern kubwa sana ya mkoloni ni swala la udini sababu kuna kosa alilifanya India na Pakistani hakutaka tena lijirudie Tanzania swala la usawa kwa dini zote alilichukulia kwa uzito mkubwa sana

Mkoloni aliwapa masharti kabla hawajarudi tena ku-discuss juu ya uhuru wawe wamesha-sort out juu ya swala la uongozi kwa sharti la awe mkristo, amesoma na mwanachama hai wa TANU kwa hiyo bila kupenda ikabidi wamchague Julius Nyerere

Nyerere kuwa kiongozi wa TANU ni uamuzi wa kutokupenda kwa wapigania uhuru na ndio the only best choice ambayo ilikuwepo kunauwezekano wako ambao walikua wazuri zaidi kwa kigezo cha elimu na uongozi zaidi ya Julius Nyerere ila wengi wao walikua ni wachungaji na mapadre kwa hiyo ingewawia vigumu kuunganisha nchi

Kwa hiyo Nyerere na mapungufu yake alikua ni mtu sahihi kupewa nchi kwa mazingira ya kipindi kile

Ndio ukweli...kuongoza nchi hakuhitaji unganga wa kupiga ramli na ujinga ujinga unaoendana na hayo. Kunahitaji akili na maarifa.
 
Kiukweli mikoa yenye waislamu wengi ni Lindi,mtwara,pwani,Tanga,Tabora na kigoma sasa hiyo 68% walifikaje?
Watu wengi hudhani ruvuma,singida si mikoa yenye waislam wengi,wakati huo iringa, Kilimanjaro,morogoro,kigoma,KAGERA Kuna namba kubwa tu ya waislam
 
Mfano;- mwaka 2012 walikuwa wanalazimisha kwenye sensu kuwe na kipengele cha kujua dini ipi wako wengi
Kikwete alikataa wazi wazi

Kuna mda unajiuliza kwanini wanalazimisha wao ni wengi
Chan...
Nimejadili suala hili katika kitabu cha Abdul Sykes (1998):

''Vyanzo tofauti vya takwimu vinatoa takwimu tofauti zinazopingana kuhusu hesabu ya Waislam na Wakristo katika Tanzania.

Hii inatokana na ukweli kuwa somo hili ni nyeti.

Katika nchi za Kiafrika ambazo zina wafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na Nigeria, uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha mgongano na mzozo.

Tatizo hili lipo Tanzania.

D.B. Barret anasema kuwa Waislam Tanzania ni wachache wakilinganishwa na Wakristo.

Takwimu zake zinaeleza kuwa Waislam ni 26%, Wakristo 45% na Wapagani ni 28%.

Takwimu za Tanzania National Demographic Survey za mwaka wa 1973 zinaonyesha kuwa Waislam ni wengi kidogo kupita Wakristo wakiwa 40%, Wakristo 38.9% na Wapagani 21.1%.

Lakini takwimu za Africa South of the Sahara, zinaonyesha Waislam ni wengi Tanzania kwa 60%.

Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka mwaka 1982.

Kwa kuwa utafiti wa Waislam wenyewe katika suala hili ni mdogo sana au haupo kabisa, suala la wingi wa Waislam katika Tanzania halijafanyiwa utafiti na Waislam wenyewe.

Mgao wa madaraka na kugawana vyeo haikupashwa kuwa sababu ya migongano na mifarakano katika Afrika.

Lakini kwa bahati mbaya sana hii imekuja kuwa sababu ya mifarakano katika serikali za wananchi wenyewe.

Jambo hili limekuwa ni suala nyeti kwa sababu ukabila, udini na kujuana ni kitu muhimu katika serikali za Afrika.

Mgawanyo wa madaraka na wingi wa wafuasi katika dini au kabila havikuwa vitu vilivyokuwa vikiwashughulisha wananchi wakati wa ukoloni kiasi cha kuleta mifarakano katika jamii.

Kwa bahati nzuri ukabila hauna nguvu Tanzania lakini dini imekuwa chanzo cha ubaguzi toka zama za ukoloni, tofauti ni kuwa wakati wa ukoloni waliokuwa wakiwabagua Waislam hawakuwa Wakristo weusi bali Wazungu.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Prof. Mazrui kalieleza tatizo hili kwa kirefu: Ali A. Mazrui, ''African Islam and Competitive Religion: Between Revivalism and Expansioní,'' in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2.

Mimi binafsi nimekuwa nalikwepa ila nililizungumza kwa kirefu katika mhadhara niliotoa University of Iowa nilipoletewa takwimu za CIA zinazoonyesha kuwa idadi ya Waislam ni ndogo Tanzania ukilinganisha na Wakristo.

Nilirejesha suala hili kwao na kuwauliza kama kuna nchi yoyote duniani ambayo ilivamiwa na wageni kutoka nje kama Wejerumani walipofika kwetu na waliosimama kupambana na wageni hao kwa silaha wakawa ni minority.

Hapa nilitoa mfano wa mapambano ya Wajerumani.

Nikawauliza pia kama ipo historia ya nchi yoyote ambayo siasa za utaifa zilipopamba moto baada ya WW II waliosimama kuongoza kudai uhuru walikuwa wale wachache na wengi wakawa pembeni.

Hapa nikatoa mfano wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ukumbi mzima ulibaki kimya.

Hakuna aliyechukua changamoto hii.

Katika hadhira hii kulikuwa na maprofesa wanne ambao wanaijua vyema historia ya Tanzania: Prof. James Giblin, Prof. Michael Lofchie, Prof. Jonathon Glassman na Prof. James Brennan.

Hawa wote wameandika vitabu wengine zaidi ya kimoja kuhusu historia ya Tanzania.

Jonathon Glassman kutokana na mjadala huu akanialika chuoni kwake Northwestern University, Chicago, tukafanya mjadala kama huu tuliofanya University of Iowa.

Niliukubali mwaliko na nilizungumza Northwestern University.

Katika mhadhara huu suala la Takwimu za CIA na Waislam wa Tanzania halikujitokeza.

Majibu niliyowapa University of Iowa nadhani yaliwatosheleza.

1707600595428.png

Prof. James Giblin
1707600663805.png

Prof. Michael Lofchie
1707601041067.png

James Brennan​
 
Nikawauliza pia kama ipo histori ya nchi yoyote ambayo siasa za utaifa zilipopamba moto baada ya WW II waliosimama kuongoza kudai uhuru walikuwa wale wachache na wengi wakawa pembeni.

Hapa nikatoa mfano wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ukumbi mzima ulibaki kimya.

Hakuna aliyechukua changamoto hii.

Katika hadhira hii kulikuwa na maprofesa wanne ambao wanaijua vyema historia ya Tanzania: Prof. James Giblin, Prof. Michael Lofchie, Prof. Jonathon Glassman na Prof. James Brennan.

Hawa wote wameandika vitabu wengine zaidi ya kimoja kuhusu historia ya Tanzania.

Jonathon Glassman kutokana na mjadala huu akanialika chuoni kwake Northwestern University, Chicago, tukafanya mjadala kama huu tuliofanya University of Iowa.

Niliukubali mwaliko na nilizungumza Northwestern University.

Katika mhadhara huu suala la Takwimu za CIA na Waislam wa Tanzania halikujitokeza.

Majibu niliyowapa University of Iowa nadhani yaliwatosheleza.

View attachment 2900130
Prof. James Giblin
View attachment 2900131
Prof. Michael Lofchie
View attachment 2900135
James Brennan​
Kuna mda nakuona uko sahii ila pia kuna mda mwingine namuona nyerere alikua sahii kwa uamuzi wake ambao unaochukuliwa sio wa-kistaarabu

Hao wapigania uhuru wa-dini ya kislamu wanahaki ya kuwa recognize ila inavyoonekana walikua wanataka jambo lingine zaidi ndo maana nyerere aliamua kuwa-cancel sababu hakufanya vile kwa bahati mbaya
 
Back
Top Bottom