JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Wangeenda ukraine kupigana na Urusi, sio kupigana na nguo.
 
LOlote wanalofanya jeshi, nyuma yao yupo Amiri Jeshi Mkuu.

Yeye ndo ametoa maagizo wananchi washughulikiwe na jeshi wanatafuta namna ya kukinukisha
Yan katuma SS tushughulikiwe , kumbe wezanke wamepiga U-turn
 
Boss, Maoni yangu yamemlenga kuruta anayekutana na raia aliyevaa nguo inayofanana na jeshi mtaani na siyo sababu halisi ya hiyo OP.
Kwani kuruta ni soldier 🤣
 
Mtu avae swat ya marekani mseme sare zenu
 
Kwani kuruta ni soldier 🤣
Hahaha. Ushaelewa lakini. Hata hivyo, ukipata nafasi ya kazi jeshini, siku ya kwanza kabisa ukiwa unawasili unatambuliwa kama mwanajeshi.
 
Kwamba tusiongee??Labda wakutake wewe Shangazi yao...ila ni ushamba, km hawana kazi wakaombe mechi ya kirafiki uko Somalia
 
Akili zako ndio kama hizi wacha dp world waje
 
Nawakubali sana Hawa Jamaa,ila zoezi hili wasijetengeneza chuki na raia kwa kupiga,nitawazereuu kama pongo wetu. Viva JWTz
 
ni mambuzi na makenge tuu hawana jipya zaidi ya kutishia raia...lango Muhimu l nchi linauzwa wameshindwa hata kupenyeza sabotage ishindikane wanasaka
vitambaa vya makamasi mtaani.
 
Nyumba 100 unazijua mzee?
Vitongoji vitatu hivyo.
Watu zaidi ya mia tano,uwe unafikiri kabla hujaandika.
Tukio lilitokea ndio, ila Nyumba 100 hapana.
Mkuu, jaribu kufatilia hili swala, lilikuwa ni jambo baya Sana na la maudhi
 
Kwanza wajue kabisa wanavunja katiba na sheria za nchi.

Chombo PEKEE ambacho kina idhini kikatiba kufanya msako au upekuzi ni Jeshi la polisi, ikiwa nchi haiko katika hali ya hatari.

Hatujawahi kusikia kwamba Tanzania katika kambi yoyote ya Jeshi, kumeibiwa sare za Jeshi na hivyo wanaanza msako kizikamata.

Hatujaskia kwamba Kuna fununu au taarifa kwamba Kuna watu au kikundi Cha watu au kampuni imeingiza sare za Jeshi Tanzania ama Kwa Nia ovu au ya kibiashara.

Hakuna mahali katika sheria za nchi askari wa Jeshi anaruhusiwa au kupewa mamlaka ya kufanya upekuzi au upelelezi juu ya makosa ya uhalifu isipokua jukumu lao ni kuhakikisha mipaka ya nchi Iko salama muda wote.

Hii inaleta picha nyingine tofauti inayofuatana na ya Jeshi la polisi kutuambia watu flani walipanga uhaini. Hivyo tuamini kwamba ndani ya muda mfupi hata ndani ya Jeshi kulikua na sura ya uasi na Kwa maana hiyo askari wa Jeshi wameiba sare na kuwapatia wananchi au paramilitaries Kwa ajili ya kujiandaa na Mapinduzi husika.

Nchi inakua banana republic na Kwa maana hiyo Kila mtu anaonesha tentacles, mnafanya nchi ionekane kituko duniani Kila uchwao,. Sijui ni elimu Gani Hawa watu wanasomea hawajui Sheri, katiba na wajibu wao.
 
Kwamba tusiongee??Labda wakutake wewe Shangazi yao...ila ni ushamba, km hawana kazi wakaombe mechi ya kirafiki uko Somalia
Somalia ni pamoto kule.Mtu akienda,kurudi ni majaaliwa.Sasa BATTLE kama hizo,hazitiliwi maanani,badala yake anakunjwa na kupigwa mitama,mtanzania ambaye hajajifunza hata matumizi ya silaha wala ngumi.Na huyo mtanzania,akipigwa,aliyempiga anaonekana MWAMBA,wakati aliyepigwa hana mafunzo yoyote.Somalia kule baadhi wana mafunzo,ndo inatakiwa mtu aonyeshe UMWAMBA kwa wale wasomali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…