Kagera Sugar 1 - 0 Simba SC | Ligi kuu bara | Kaitaba
Hilo pila linalochezwa sijui mnauonea wapi. Mimi naona uchezaji wa kawaida tu, mechi imepooza, Simba uwezo wa kushinda wanao ila wongeze kasi kwenye kushambulia
Inawezekana labda huoni mashambulizi yanayo fanyika mkuu
 
Kwa jinsi Simba tunavyocheza ni kujitoa ufahamu kuamini kuwa bingwa msimu huu ni Simba. Timu inachechea mpira muda mwingi kuliko kupambana kiume kutafuta matokeo kwa kulazimisha. Akina Bwalya na wenzake wanachezea nafasi huku wakichelewesha mipira kitu kinachopelekea timu pinzani kujipanga kikamilifu kuziba nafasi. Mwisho wa siku tunailamu TFF na GSM wakati timu inacheza kitoto muda mwingi. Tukiendelea hivi hata nafasi ya pili tutaipata kwa mbinde
 
Henonga anathibitisha kwamba ile tuzo kule zenji hakuipata kwa kubahatisha
 
Kwa jinsi Simba tunavyocheza ni kujitoa ufahamu kuamini kuwa bingwa msimu huu ni Simba. Timu inachechea mpira muda mwingi kuliko kupambana kiume kutafuta matokeo kwa kulazimisha. Akina Bwalya na wenzake wanachezea nafasi huku wakichelewesha mipira kitu kinachopelekea timu pinzani kujipanga kikamilifu kuziba nafasi. Mwisho wa siku tunailamu TFF na GSM wakati timu inacheza kitoto muda mwingi. Tukiendelea hivi hata nafasi ya pili tutaipata kwa mbinde
Nilichokuja gundua ni kwamba hawa wachezaji ambao wanalipwa kufanya hiyo kazi ya kuwapatia matokeo mashabiki wala hawaumii kama wanavyoumia mashabiki ambao hata kumi hawalipwi haiwezekan game ambayo mnahitaji matokeo mnacheza show show halafu dakika za mwisho ndiyo wanajifanya wanaharaka
 
Duuuh hiyo rough mbona kama niliiona kwenye shaolin soccer
 
Back
Top Bottom