Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Sijasoma mpaka mwisho wala sikujua kilichotokea au kinachotokea ila nimeishia hapa kabla sijaondoka inabidi nijibu...

Nimefarijika na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa @JamiiForums kwa kuondoa/kufuta mada zote zinazowadhalilisha walimu na kada nzima ya ualimu na kuwapa adhabu stahiki wale wote waliokuwa vinara kwenye hilo.
"I might disagree with what you say.., but I will defend to the Death for your right to say it"

Yaani watu wamekuwa Mambi Pambi and this is Political Correctness going Mad..., Yaani mwalimu uone umedhalilika sababu fulani anakudharau (who cares) na badala ya kuwaziba midomo wanaosema kwanini usiwapuuze na kama wengine wanasema na mtu huna hoja ya kuweza kupangua hoja zao , You might not have become a teacher in the first place.... What a Disgrace......

 
Kutumika na wanasiasa ni moja ya vitu vili/navyowashusha hadhi.

Lakini pia umoja tepetepe pia, walimu ni wengi nchini, matatizo yao yanafanana almost nchi nzima. Ni ajabu kutokua na umoja thabiti kutetea maslahi yao.
Ni nani asiyetumika na wanasiasa kwa maisha ya sasa, watumishi wa umma walio wengi wanafanya kujipendekeza Kwa wanasiasa tazama wakurugenzi, wakuu wa idara na hata vyombo vya dola, kwa asilimia kubwa utawaona kwa sehemu kubwa "wanatumika" na wanasiasa!
Hivi unapoona polisi wanashambulia watu kwa mabomu ya machozi, virungu, na maji ya kuwasha ni Kwa maslahi ya nani?

Walimu mnawaona wanyonge sio kwa ubaya wa kazi yao, bali ni kwa sababu ya kazi yao kutokuwa na mianya ya udokozi, mshahara ndiyo chanzo kikuu cha mapato yao, lakini wakiamua kuwanyonya wanyonge kupitia watoto wao nakuhakikishia jamii itapata taabu sana, na kuna ambao hawatasoma!

Walimu Mungu awabariki sana, miaka hiyo tunasoma (sekondari) 2000s, jamaa yetu alifaulu kwenda Tosamaganga PCM, nyumbani kwao hali ilikuwa mbaya sana, walimu wetu walijichanga na kumpa mahitaji yake yote, ikaundwa kamati ya kumfuatilia jamaa anapoishiwa wanam-boost mpaka kumaliza form six, jamaa alienda kusoma diploma ya mambo ya Maji, (taasisi ya maji Dar).

Na sasa anahudumia wananchi wengine huko kusini, bado mnawananga walimu?jitafakari sana kijana!
 
Mkuu unamawazo mazuri sana ila anza ukiwa kazini yakitiki kopa wekeza mifugo yako na mashamba then timua. Kuna watu wanamake hela mashambani na hata hawa habari na ajira ila sema mtu ukiajiriwa unahofia kupoteza ajira.
Kweli kaka, tumejengwa kwenye hofu, Kuna sehemu natamani yawe makazi yangu Ili nikafanye nachokipenda Ila zengwe ninalopigwa huku Halmashauri acha tu Mpwayungu aendelee kusema Kila siku.
 
Si vema kufanya vitu nusu nusu hutaweza kukamilisha utakacho ama kufikia lengo utakalo na huku kwenye mabandiko unaweza kuwa mis-informed kwakuwa na tabia hii ya kusoma kitu bila kumalizia na kuona tamati inasemaje
 
Walimu Mungu awabariki sana, miaka hiyo tunasoma (sekondari) 2000s, jamaa yetu alifaulu kwenda Tosamaganga PCM, nyumbani kwao hali ilikuwa mbaya sana, walimu wetu walijichanga na kumpa mahitaji yake yote, ikaundwa kamati ya kumfuatilia jamaa anapoishiwa wanam-boost mpaka kumaliza form six, jamaa alienda kusoma diploma ya mambo ya Maji, (taasisi ya maji Dar).

Na sasa anahudumia wananchi wengine huko kusini, bado mnawananga walimu?jitafakari sana kijana![emoji1548][emoji818][emoji817]
 
Si vema kufanya vitu nusu nusu hutaweza kukamilisha utakacho ama kufikia lengo utakalo na huku kwenye mabandiko unaweza kuwa mis-informed kwakuwa na tabia hii ya kusoma kitu bila kumalizia na kuona tamati inasemaje
Nimejibu hio Qoute hayo mengine nina Mtizamo wangu kama wengine wenye mtizamo wao (wengine wanatukana tu waalimu sababu ya Chuki zao binafsi au uelewa mdogo; wengine wanatania (banter) in short who cares (To each their Own)...,

Nilichojibu mimi ni kilichonigusa mambo ya kufuta uzi au watu kuzibwa midomo eti kwa so called kudhalilishwa ni pettiness - Ukizingatia kama wewe unaona umevaa vizuri mtu akija akasema umevaa vibaya ukianza kukubaliana nae au kuumia nadhani matatizo ni yako na sio yake....
 
Point sana mkuu,lawama zote ni kwa wanasiasa(serikali) wanawanyonya sana walimu,karibu kada zote za serikali wanapata posho isipokuwa walimu kwanini wasiwe na kinyongo,walimu wanakaa miaka 7 daraja moja kwanini wasidharaurike,mfano watu wanaanza kazi mwaka mmoja arafu kwenye kupanda madaraja wanatofautiana kwanini asiwe na kinyongo.Serikali imeshindwa kuweka mifumo sahihi ya haki za walimu mwisho wa siku wanazalisha kizazi kisichokuwa na maarifa(kisichojua umuhimu wa walimu katika nchi) ambacho ndiyo kinachowadharau walimu wetu.
 
Hii point pengine hujaielewa vema...
[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Nimefarijika na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa JamiiForums kwa kuondoa/kufuta mada zote zinazowadhalilisha walimu na kada nzima ya ualimu..!!!

Sijapongeza kufutwa kwa mada zote ziwe za kusifia au kukosoa au kushauri bali zile tu ZINAZODHALILISHA KADA YA UALIMU NA WALIMU
 
Ni kweli kabisa unachosema. Tatizo lipo namna ya kuwaweka ktk mzani ili kujua wapi ni masikini. Watu wamekuwa wana generalize bila kujua kuna Walimu wamepiga hatua kubwa sana kuliko tunavyodhania. Miaka ya 2012 nilikuwa hapo Morogoro, Kuna shule moja ya msingi kutoka Msavu kuelekea mjini kituo Cha Kanisani nilikuta magari yamejaa nilipouliza wenyeji km hapo kuna kikao Cha wazazi nikaambiwa hizo ni gari za Walimu na wengi ni wanawake ndiyo wanamiliki hizo ndinga.

Kwa hiyo mtu asichukulie maisha ya Mwalimu aliemfundisha au anaeishi naye akadhani wote ni pompoma. Tena Nikuambie tu kuwa Walimu wa sasa ni tofauti sn na wazamani. Km wewe mwenyewe ulivyosema zamani ualimu ulikuwa ni wito, kwa sasa ualimu ni ajira. Hujiulizi kwa nini undergraduate wanalilia ualimu hata kwenda shule ya msingi wakati zamani kufundisha msingi ilionekana mtu wa elimu ya chini.

Sasa hivi Mwalimu mwenye malengo akiajiliwa tu ndani ya miaka michache anatoboa. Tusiangalie wale walevi wa kupindukia na wazinzi, tuangalie wale waliosoma na kuelimika na kujua nini wanakihitaji ktk maisha yao. Wapo wengi tu wanaosomesha watoto wao English medium, na nafikiri unajua bei ya huko. Sasa ebu hao bodaboda waliokuwa wanawadhihaki huko mtaani wanaosomesha watoto wao English medium wapo?. Kebehi za hovyo tu kwa hawa Walimu. Mwalimu leo akihitaj mkopo Bank yoyote hata kuanzia 15m atapewa, sasa hao bodaboda watapewa kwa dhamana gani waliyo nayo.

Maisha ya mtu ni uamuzi wake, wapo wafanyakazi wa serikali wenye mishahara minono lakini maisha yao ni spana mkononi, wengine hata kwenda likizo kwao wanashindwa sababu hata kibanda huko hawana. Km wewe ni mfuatiliaji wa mambo utakubaliana nami kwa hili. Kuna Uzi humu unaohusu viongozi wa serikali waliofariki bila kujenga, tafuta humu wametajwa wachache.

Sema nao Walimu siku hizi walio wengi kasi ya ufundishaji imepunguwa, most of them are struggling to earny their daily bread out of their career. Ndio maana utakuta wengine ni Walimu lakini muda huo huo ana goli sehemu au ni bodaboda.

Tatizo Walimu wa zamani waliyaweka maisha yao ktk ualimu 💯% bila kufikiri nje ya box. Walikuwa committed kwelikweli kwa sababu jamii na serikali waliwathamini sn. Na ndiyo maana maisha yao hayakuwahi kuwa mazuri sababu kuheshimiwa tu na jamii waliona inatosha. Walimu wa sasa kwa kiasi hawapati hiyo hadhi ndiyo maana na wao wameamua kutafuta maisha nje ya kazi yao. Kifupi wapo kimaisha na masilahi zaidi kuliko kuheshimiwa.

Hapo nadhani utakuwa umenielewa vyema.
 
Hao wengine kutumika na wanasiasa ndio kunawapa wao huo uhalali ama??

Wimbi la walimu kudharaulika halijaanza miaka ya zamani sana bali ni hii hii miaka ya 2010+ ndo imepamba moto.
Na sababu wao ndo wanachaguliwaga kusimamia mambo ya kiserikali kama uchaguzi na sensa, na haohao kwenye hizo chaguzi ndo huleta figisu. Na ndo hapo wakaanza kudhaniwa vibaya na jamii.

Mi nawashauri wawe na umoja skanganga
 
Hao sio walimu kwa wito
Hao sio walimu waliopikwa wakaiva
Hao sio walimu waliokomaa kiakili na kifikra
Hao sio walimu waliosoma na kufaulu masomo ya haiba, misingi na falsafa
Mkuu Mshana Jr walimu pia tuna haki zote za kufanya shughuli zote za kitaifa..

Shida ni pale ambapo inatokea baadhi yao wanadhalilisha taaluma hii nadhimu kwa kuhonga ili wapate kazi hizo..

Lakini pia sioni sababu kuwalaumu wanaozipigania nafasi hizo kwani kipato cha walimu ni kidogo mnoo.
 
Uko sahihi kabisa blogger huyo nilimjibu hivyo kwakuwa kuna kitu aliandika ngoja nikiweke hapa[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Haiwezekani ishu za kuandikisha ugawaji wa mahindi Mwalimu anaomba, kuandikisha kupiga kura wanagombania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…