UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Yehova ni katika majina mengi ya Mungu ambayo amejitambulisha nayo, kabla ya Musa hakuwahi kujitambulisha kwa jina Yehova. Sasa wewe kukataa kuwa hivyo vitabu si vya Allah na kuamini ni vya Yehova tu hilo tatizo la kukosa uelewa tu.Allah kutaja vitabu ambavyo sio vyake bila kumtaja mwenye hivyo vitabu yaani Yehova huoni kama huo ni wizi/plagiarism?
Ni Sawa na hamornize atoe Remix ya wimbo wa Diamond bila kumhusisha Diamond huo ni wizi.
Alafu hoja inayozungumziwa ni kuwa Quran haiwezi kutumika Kama rejea kuu kwani licha ya kufanya Plagiarism na forgery lakini pia haijitoshelezi kutoa taarifa sahihi na zilizojitosheleza.
Mfano ninaweza kukuuliza,
Yakobo alifia wapi, akiwa na umri upi, na wake zake walikuwa wangapi na kina nani, utajibuje na kupata majibu wapi bila kutumia Biblia?
Embu jibu hiyo hoja mbele ya mahakama
Chengine ambacho nitaendelea kukumbusha ni kwamba Biblia imekusanya maandiko kutoka kwenye vitabu tofauti tofauti na kuweka sehemu moja ila Qur'an si kitabu kichokusanya maandiko ya vitabu vyengine pamoja na ndipo ikaitwa Qur'an bali inajieleza kuwa ni kitabu cha mwisho katika mfululizo wa vitabu vya Mungu na ndio maana imevitaja vitabu vyengine vya Zaburi,Torati na Injli.