Kama kweli tunamuamini Mungu katika majanga ni kwanini tulikatazwa kumuombea Tundu Lissu alipopigwa risasi?

Kama kweli tunamuamini Mungu katika majanga ni kwanini tulikatazwa kumuombea Tundu Lissu alipopigwa risasi?

Punguzeni Utani na Matabaka kwny Swala Nyeti kama hili.
Mbona mnakuwa kama mafarisayo Ulitaka unapomwombea Lisu kila mtu barabarani aone unaomba? Ndo Mungu angejibu au?,au kwa kuomba vile ungemshurutisha Mungu ajibu.?
Kwani ungemuombea ukiwa chumbani kwako Mungu asingeskia?
Mbona ulipozuiwa bado watu waliomba majumbani kwao Lisu hakufa,alipona Hata sasa anaishi!!!.
Kuna wengine wapenda maombi ya kinafiki,
Hupenda sala zao sikiwe na kila mtu.
Sasa mbona ndugu yenu ,ametangaza kwenye vyombo vya Habari maombi ya siku 3,kwani hadi utangaze?mbona viongozi wa dini wakitoa waraka wa kuwakosoa muache udhalimu,wote mnaitikia kama mazuzu,ooh muache kuchanganya dini na siasa.mweeeeee!
 
Punguzeni Utani na Matabaka kwny Swala Nyeti kama hili.
Mbona mnakuwa kama mafarisayo Ulitaka unapomwombea Lisu kila mtu barabarani aone unaomba? Ndo Mungu angejibu au?,au kwa kuomba vile ungemshurutisha Mungu ajibu.?
Kwani ungemuombea ukiwa chumbani kwako Mungu asingeskia?
Mbona ulipozuiwa bado watu waliomba majumbani kwao Lisu hakufa,alipona Hata sasa anaishi!!!.
Kuna wengine wapenda maombi ya kinafiki,
Hupenda sala zao sikiwe na kila mtu.

Kulikuwa na ubaya gani kujumuika kwa pamoja kumuombea? Ni nani alilazimishwa kumuombea?
 
Kama ndivyo uaminivyo iweje leo tupewe muongozo wa maombi tena kwa siku tatu? Ameona/amegundua nguvu gani ktk maombi?? Hapo ndipo unapogundua ni aina gani ya viongozi tulionao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmhh ndugu yangu ngoja kwanza nikuulize hivi ukipatwa na banga wewe hapo au Mimi ni aina gani ya janga ni la kitaifa?,kidunia,?je zitangazwe siku ngapi za kuniombea Mimi au wewe?, na nani yuko responsible kuniombea/kukuombea? Na wasipoomba je.?

Vipi kuhukuhusu Corona ni aina gani ya janga,
Ni nani wako responsible kuomba ,na wasipoomba je?
 
Hili ni swali namba tatu la mwaka 2020.

Swali namba moja ni Corona Virusi ni Natural au man made?

Swali namba mbili, kama corona virus ni man made je ilitengenezwa kwenye laboratories za wuhan au wapi?

Kama corona virusi ni Natural? basi swali hili automatically linakuwa ni swali namba mbili la mwaka 2020.
 
Tuli katazwa kukusanyika na kumuombea kiongozi na mbunge wetu alipopigwa risasi 16. Tulikatazwa kuvaa T-shirts za Pray 4Tundu Lissu.

Ni Mungu yupo huyo anaechagua maombi. Hata kwenda kumjulia hali Tundu Lissu hospitali lilikuwa kosa la jinai.

Nchi imekuwa ya matabaka, viongozi wa upinzani wanaonekana kama wahalifu. Hawa ni viongozi tuliowapigia kura na tuna imani na uongozi wao.
Unafukua….....!!
 
Duh kwa hiyo Lissu mmoja analinganishwa na janga la corona linaloua watu elfu mbili kwa siku moja!.

Marekani imetangaza kuwa na raia milioni 22 wasiokuwa na kazi na bado idadi inaongezeka, halafu corona inalinganishwa na mwanaharakati fulani wa Tanzania.
 
Tuli katazwa kukusanyika na kumuombea kiongozi na mbunge wetu alipopigwa risasi 16. Tulikatazwa kuvaa T-shirts za Pray 4Tundu Lissu.

Ni Mungu yupo huyo anaechagua maombi. Hata kwenda kumjulia hali Tundu Lissu hospitali lilikuwa kosa la jinai.

Nchi imekuwa ya matabaka, viongozi wa upinzani wanaonekana kama wahalifu. Hawa ni viongozi tuliowapigia kura na tuna imani na uongozi wao.

Acha ufala,lisu ni janga?
 
Ninachokumbuka walikataza baada ya sheikh mmoja kutaka kufanya albadir kwa waliompiga risasi, vaa viatu vya jiwe ungefanyaje
Jiwe kulikimbia Taifa lake na kwenda kujificha Chato wewe unamuona ni mzima kweli?sisi tunaona ni Albadiri inafanya kazi yake barabara na mpaka atawehukia Ikulu
 
Kwenye swala la kumuabudu Mungu kamwe usiamini mtu na ogopa sana yule ambaye kila wakati anamtajataja Mungu, huyo ndio muovu mkubwa na wa kutupwa.

Ukiangalia vizuri huwezi kukuta watu weupe wakitajataja jina la Mungu, achana na waarabu.

Kwenye mambo na changamoto zinazokukabili Mungu aliishakupa akili na kukuweka hapa duniani hivyo ni jukumu lako sasa kupambana na kwa hili ndio maana watu weupe wanafaulu sana.

Kubaki kumtajataja jina hakusaidii lolote na inakufanya uonekane mnafiki tu kwani wakati unamtaja taja utakuta una maovu kibau ambayo wakati huo unamtaja taja wala utakuta hauwezi kuyatubu na ndio maana hata hizo sala hazijibu. Anawaona wasanii na wanafiki tu.
 
Nimeishi na watanzania wenzangu kwa miaka mingi. Wengi kwa kweli ni watu wema, peace yaani. Kuna watu hata siwajui lakini tukipishana barabarani au kwenye madaladala wanakusalimia vizuri sometime kwa bashasha kabisa na story wanaanzisha. Ukipotea njia, kwa sisi wenzangu na mie wenye poor sense of direction, yaani watu kadhaa wanaweza kuacha shughuli zao na kuanza kukuelekeza njia mpaka una appreciate. Haya ni machache sana ila huwa yananipa amani na deep feeling kwamba bado tuna watu wema.

Lakini kuna wachache kati yetu ni mbwa mwitu. Watu wanajifanya ni wacha Mungu kumbe ni wanafiki na mashetani wakubwa ndani ya ngozi ya kondoo. Hawa sio tu wanaamuru lakini pia wanapiga wenzao risasi 32, wanateka,wanatesa,wanaua,wanapoteza watu na kubambikia binadamu wenzao kesi.
Basi na muwe waangalifu.
 
Back
Top Bottom