Kama Rais hataki kufanya kazi na Kassim Majaliwa amuombe ajiuzuru kama Philip Mpango

Kama Rais hataki kufanya kazi na Kassim Majaliwa amuombe ajiuzuru kama Philip Mpango

Kwa kutumia katiba ipi mkuu? Au haya ni mawazo yako binafsi?
Kuna Katiba na KATIBA
Mfano;
Alianza Julius Nyerere
Akafuata Ally H. Mwinyi
Akaja,Benjamini Mkapa
Baadaye,Jakaya Mrisho
Kisha,John Magufuli
Sasa ni S. S. Hassani
Ajaye ni mfuasi wa Yesu
Sijui umenipata mkuu?
 
Alichimbwa bit na state hawezi kumuondoa!

Mpango bado ni makam hadi Bungee litakapovunjwa na serikali kufika ukomo wake!
 
Kitambulisho mzanzibar mkaazi kukipata Kazi rahisi as long as kama Una Kadi ya ccm na NI mwanachama hai Basi📌
Mkuu kwani Zanzibar ni taifa la CCM? Ninachojua ni kwamba Zanzibar ni taifa la kiislamu. Ungeniambia kuwa ili kupata kitambulisho cha mzanzibar mkazi lazima uwe na cheti cha uislamu ningekuelewa.
 
Kuna ibara yoyote ya katiba imevunjwa kwenye hilo unalolalamikia? Samia hakuwa na ulazima wa kufanya hicho unachofikiria wewe kwahiyo hakuna baya lolote alilofanya vinginevyo unaweza kumshauri Majaliwa ajiuzulu kama hakubaliani na kilichotokea,uamuzi wa kujiuzulu ni wake siyo mpaka aambiwe na Rais.
Mkuu kuwa serious basi. Wewe unaona Sa100 kukata jina la Majaliwa na kuleta jina la Nchimbi ambaye ni muasi wa chama ni haki na sawa?
 
Watalingana na SUMAYE miaka kumi kama MAJALIWA hatapewa nafasi tena





Huelewi kama mitihani ya form 4 na 6 ni jambo la Muungano?
au ndio mmekariri kwa kua tangu 1964 nafasi kama hizo zinashikiliwa na Watanganyika?
Na ikitokea siku IGP au CDF akatokea upande ule usioupenda?
CHUKI HAZIJENGI.
Je, mbona wazanzibar wana baraza lao la mitihani (ZEC) si angemtafutia nafasi huko badala ya kuja kujaza nafasi za watanganyika? Kwani huku Tanganyika alikosekana mtu wa kuongoza NECTA hadi wamlete mpemba kuchukua nafasi ya watanganyika? Wewe unadhani ni haki na sawa wapemba kuchukua nafasi za watanganyika kizembe hivyo?
 
Nyinyi si mlikuwa mnashingilia kwa nderemo na vifijo. Acheni uchawa na unafiki, mkilalamikia hapa JF haitoshi kuweni jasori muyaseme haya kwenye vikao vyenu.
Mkuu nilipambana nikashindwa. Tatizo wajumbe wengi wana asili ya uchawa. Ukisema haya hadharani wanaweza wakakuua au unaweza kupotezwa kama alivyopotezwa Ben saane, Azory Gwanda na Kibao. Ndio maana natumia mbinu mbalimbali kupambana kila mahali ili kuwafungua bongo watanzania wajue nini kinaendelea.
 
Sitaki salamu, naingia kwenye mada moja kwa moja. Wahenga walisema akutukanaye hakuchagulii tusi na asiyekutaka hakuambii toka bali atakutoa kwa visa ovu dhidi yako.

Kabla ya kwenda mbali kwanza naomba ku declare intrerst kuwa mm ni mwanaCCM kindakindaki na juzi nilikuwepo ndani ya ukumbi kule Dodoma nikishuhudia katiba ikisiginwa bila woga wowote. Kitendo cha Rais Samia kumpendekeza Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake, hivyo automatically kuwa makamu wa Rais ikiwa CCM ikishinda kiti cha urais, ni ubaguzi mkubwa sana kwa waziri mkuu, Kassim Majaliwa. Majaliwa amefanya kazi chini serikali ya Magufuli tangu Rais Samia akiwa makamu wa Rais na baadaye kuwa rais. Ina maana kwa muda wote huo bado hajaona kama Majaliwa anafaa kwa lolote hadi anaenda kumuokota mtu aliyekiasi chama na kujiunga na team Lowassa ndiye awe makamu wa rais? Hili jambo mimi kama kada mwaminifu wa CCM linanisikitisha na kunikatisha tamaa kupindukia. Rais kama hamtaki majaliwa na anaona hafai kuwa kiongozi si amshauri ajiudhuru kama alivyofanya Philip Mpango?

Nina wasiwasi hata Mpango hukutakiwa kwenye uongozi wa sasa ndio maana alishauriwa ajitoe kwenye nafasi yake kwa kuandika barua halafu watu wanakuja kutuletea drama kwamba eti alikataa mwenyewe. Ashindwe kukataa kipindi cha Magufuli aliponyweshwa sumu aje kujiuzuru kipindi hiki ambacho tayari afya yake imeishaimarika? Tatizo mnatuona watanzania wote ni mazombie!

Hata kama hupendi kufanya kazi na mtu sio kumbagaza kiasi hiki mbele ya jamii na kusigina career yake ya kisiasa aliyoijenga kwa muda mrefu. Haipendezi hata kidogo.

Sote tumeshuhudia marais wakisuka safu zao za uongozi ndani ya chama chetu tangu kipindi cha mwalimu Nyerere lakini hatukuwahi kuona ubaguzi wa kiwango hiki. Na kibaya zaidi ubaguzi huu hauanzii kwenye uongozi wa juu tu bali hadi huku chini ni ubaguzi tupu. Ni katika utawala huu ndipo tumeshuhudia wazanzibar wakiteuliwa kushika nyadhifa za watanganyika wakati watanganyika hawawezi kupata nafasi kama hizo ktk nchi ya Zanzibar. Hivi inakuwaje raia kutoka Pemba anateuliwa kuwa RAS wa mkoa hapa Tanganyika? Hata Magufuli alikuwa dikteta lakini hatujawahi kushuhudia akifanya ubaguzi kama huu. Kwanza yule mpemba aliyepo kule baraza la mitihani aliingiaje pale? Haya mambo yanatia hasira sana. Yaani watanganyika wanakosa nafasi za ajira halafu wapemba wanakuja kujazwa kwenye nafasi za ajira za watanganyika? Ni nini hiki jamani?

Ujenzi wa Kizimkazi umetumia matrilioni ya fedha za watanganyika. Kana kwamba hii haitoshi, bado wapemba wanakuja kuchukua nafasi za watanganyika. Kwani Tanganyika imegeuzwa kuwa koloni la Zanzibar? Viongozi mnaofanya teuzi mnatuletea mambo ambayo yanaweza kuja kupelekea mauaji ya kimbari siku za usoni ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa kuacha kasumba hii mara moja. Time will tell.
Unaanza chokochoko,
 
Hv unatumia akili au makalio? Majaliwa ni waziri mkuu, amefanyiwa Nini, ht angempumzisha ni uamuzi wa Rais na si kt kigeni
Nchimbi ni katibu mkuu kwani yeye kafanywa nini? Labda ngoja tuanze hapa twende mdogomdogo huenda utanielewa mkuu.
 
Nyie hamjui na ukweli ndio huu, lengo la Samia ni CCM ianguke kwa masilahi ya Zanzibar ipate kujitenga kuwa Nchi huru,

Anajua kabisa hakubaliki na yeyote na hakuna mwenye akili timamu atayempa kura yeye na Nchimbi wake.

Samia anajitoa mhanga kwa masilahi ya Wazanzibar akijua kabisa Sera za CHADEMA ni kuvunja Muungano.

Siku mkija kugundua mtakuwa mmechelewa sana.
 
Mkuu kwa sheria ipi kipengele gani kifungu kipi kinacho eleza kuwa PM awe makamu wa 1 au wa 2 au mgombea mwenza???
Mkuu kwa sheria ipi kipengele gani kifungu kipi kinacho eleza kuwa PM asiwe makamu wa 1 au wa 2 au mgombea mwenza?
 
Hiki chama kina kawaida ya kusujudu sana wenyeviti wake Taifa hata kama ni weupe kiasi gani 🤣🤣
 
Nchimbi ni katibu mkuu kwani yeye kafanywa nini? Labda ngoja tuanze hapa twende mdogomdogo huenda utanielewa mkuu.
Nchimbi kateuliwa mgombeza mwenza, shida tunaingilia maamuzi ya chama Cha watu ambapo chombo mikubwa kuliko vyote mkutano mkuu ndio umefanya hayo, Nani mwingine wa kuingilia hayo maamuzi? Tuwe waelewa tufanye Mambo yetu
 
Sio kweli kikwete aliokuwa Muslim na makamu wake mzee ghalib bilali aliokuwa Muslim lkn WAZIRI mkuu aliokuwa mkatoliki mzee pinda
 
Ukiacha hayo macho yako yanavyoona. Ngoja nikupe jicho la tatu. Rais akiwa muislamu bakwata makamu anakuwa mkristo mkatoliki. Na Rais akiwa mkristo mkatoliki makamu anakuwa muislamu bakwata. Hutaki ckulazimishi
Huu upumbavu hatupaswi kuuendekeza kamwe vipi akitokeq mpagani tutafanyaje hebu tuache kuendekeza ujinga aise nchi haijawahi kuwa na dini
 
Raisi Samia -muslim
Majaliwa -Muslim

mkuu hapa tanzania ingekua ngumu kuwa na VP toka bara mwislamu ikiwa Raisi nj mwislamu......

kwenye hili nadhani unakosea, huwa inawezekana kuwa na Raisi toka bara mwislamu na makamu toka zenji mwislamu kaa sababu zenji wakristo kwenye siasa ni kama hawapo!
Zanzibar wakristo wapo lakini hawateuliwi?
 
Back
Top Bottom