Maji kukosekana ni rahisi kukosoa kama huangalia hali halisi kwa kina. Mkaa wote wa Dar unatoka mkoa wa Pwani, jiulize hiyo inamaanisha nini katika suala la mazingira.
Pwani inakuwa jangwa kwa faida ya matumbo ya watu wa Dar. Kumbuka pia ukame ni eneo lote la afrika kuanzia Djibouti mpaka Tanzania. Hivyo huwezi kuwa na hali ambayo mifugo inakufa halafu maji yasiwe tatizo, kwa akili za kawaida tu.
Mfumuko wa bei hauwezi kukwepeka ikiwa rais anazijali sekta zote, anatoa pesa za ujenzi wa madarasa, pesa za ukarabati wa miundo mbinu ya kila namna. Anakarabati bandari zote za TZ pia anawapa uhuru wakulima kuuza mazao mahali wanapopataka bila ya bughudha. Mfumuko wa bei katika hali kama hizo ni suala la kawaida tu.
Kumbuka kuwa frames mbalimbali zilizokuwa zinakula vumbi awamu zilizopita kwa sasa zimeanza tena kuuza, zinafanya biashara. Mzunguko wa pesa unaanza kuimarika hivyo masuala ya mfumuko wa bei hayawezi kukwepeka, tazama upande mzuri wa uchumi na sio kuishia kuutazama mfumuko wenyewe kama wenyewe.
Elimu inaimarika siku baada ya siku, sema ushindani wa soko la ajira ni mzito sana. Mtanzania aliyepata elimu ya chuo kikuu anakuja kupambana na msomi kutoka Kenya au nchi za kusini mwa afrika mwenye CV pana na uzoefu wa kazi na uwezo wa mawasiliano kwa maana ya kingereza, anakutana na wakati mgumu.
Cha muhimu sana alichonacho SSH ni kuwa positive minded a leader, kiongozi mwenye mtazamo chanya kila anapoongea na watu mbalimbali. Hatangulizi ujuaji wala ujeuri ambao ni sawa na upofu kwa kiongozi mkuu wa taifa.