Kama siku zingerudishwa nyuma ungefunga hiyo ndoa?

Kama siku zingerudishwa nyuma ungefunga hiyo ndoa?

Hata mimi 12 years siwezi kumwacha kamwe. Huwa nayatafakari mazuri yake tuu. Sikubali kabisa kupoteza muda eti kufikiria mapungufu yake.... Maana mazuri yake ni mengi mno kuliko mapungufu.

Pili kila nikimwazia pale anaponikosea basi wazo hunijia je mimi namkosea mangapi?? na ananivumiliaaa... Nikiwaza hayo nasamehe haraka tunasonga mbele.. Penye upungufu wake ni wajibu wangu kukamilisha.. Na Penye udhaifu wangu basi yeye ndiye wa kunishika mkono.
Uko sahihi na uko matured enough, no one is perfect loh, but case za uzinifu uliokubuhu ni vizuri kila mmoja achukue hamsini zake.
 
Nimejibu sema we si kipanga!!!humu asilimia kubwa wanajuta kufunga ndoa hizi za kirumi ambazo ni ndoano kwao!!!!

Warumi wangeleta sheria ya mke zaidi ya mmoja ndoa zingedumu sana na wanawake wivu wa kijinga ungeisha na wanaume tungeishi maisha marefu!vifo vyetu vinachangiwa na kuoa mke mmoja!!!!
Ndoa za wake wengi za waislamu ndio zinaongoza kwa talaka na kuachana hovyo na wanaoa wake wengi na matatizo kedekede tunajionea. Hamna aliye kamili wewe oa hata wake kumi uone ka utakuwa na amani moyoni zaidi ya kufa na pressure, amani na furaha ni tunda la moyoni na sio watu wakukufuraisha
 
Niko peace sana, loh Hadi watu hunishangaa
Unajua nini? Juzi nilishtuka sana kwenye ule uzi wa Controla uliposema eti nawe kuna njemba humu ilikutapeli ukaiwashia moto mpaka ikakulipa. Nilishangaa kwamba kuna njemba zenye ujasiri mpaka wa kumtapeli mwanamke wa shoka, shujaa na ngangari asiyeogopa kitu kama wewe kweli? Nilishangaa mno na mpaka sasa sijaamini [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Inabidi nimfuate anipe maujanja.
 
Back
Top Bottom