Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana


Hivi unafikiri Kenya,Uganda na Rwanda hawajui silaha tulizonazo hadi wasubiri 9/12 ndio wazione?
 
BUK haiwezi kutungua drones. Zimeshindwa kina Pantsir na Tungushka ambazo ni modern sembuse hizo BUK. Labda ukisema vidrone uchwara
Acha kuizalilisha Buk.Urusi kila siku wanatungua Drone za waasi wa Syria kwa kutumia Buk-missile.Syria wenyewe walitungua drone nyingi za mturuki kwa kutumia Buk na Pantsir
 
Hiyo picha ya pili kutoka chini ni anti aircraft gun? Dunia ya sasa AA batteries zipo tu ila unaweza usizitumie popote
Ndo yenyewe kaka, ni aibu kubwa mno.

Sijui nani utamtungua kwa Anti Aircraft Gun ulimwengu wa sasa, labda haya madege yetu ya miaka ya 60 ndo yanaweza angushwa na hizi takataka.

Uganda ana mashine matataa saaaana za angani, ana Sukhoi SU-30 Sita. Huyu akiamua hata Ikulu anadondosha mzigo na anatembea pasipojulikana.
 
Nitashangaa kama kilichooneshwa ndo kilichopo...
Anyway kwa uchache pale stadium alikuwepo Kagame!!
 
Magufur tokea aingie madarakan hakununua vifaa vya ulinz hata bastora moja
Nilitaka nione hapa kama kuna silaha mpya. Sasa natumaini awamu ya tano haikununua sana silahasilaha hasa labda hizo Cougar na Super Cougar mbili, moja ilikuwa kwenye maonesho na nyingine iliyowabeba walipoondoka wameninginia sijui ni type gani. Na zenyewe waweza kuta order ilitolewa kabla ya JPM
 
Huwezi kuonesha vyote ulivyo navyo, lakini anaehitaji kujua kwa technolojia ya mawasiliano leo atajua ulivyo navyo hata ulivyo agiza a havijawasili.
Kama amekuelewa atakuwa ana akili sana. Endapo hajakuelewa basi atakuwa mzito kichwani.

Umenena vyema kabisa mkuu.
 
H
Halafu, siyo silaha zinazopigana bali ni watu wenye uchungu wa nchi yao. Sijui wakati wa vita vya Kagera dhidi ya Nduli Idd Amin Dada ULIKUWA WAPI, ila ukweli ni kwamba arsenal ya silaha za kivita aliyokuwa nayo Idd Amin kama angekuwa na wanajeshi wafia nchi, ingekuwa balaa, lakini tukampiga na kumfurusha na hayo masilaha yake yote na mengine tukayateka.
 
Tungekuwa Western Africa uko tungenyanyasika. Ona kama Liberia ilivyoivamia Sierra Leone ikaweka waasi ili iibe almasi kama ambavyo Rwanda na Uganda zinafanya pale DRC
 
Mzee mambo ya watu kupiganisha yalishapitwa na wakati. Sasa hivi ni technology ndio inapigana. Achana na mawazo ya kijima ya Nduli Idd Amin Dadaa.
 
Hizo helicopter zenye landing gear alinunua nani?

Uongo mbaya jamani
Cougar? Embu nenda google usome vizuri.

Kikwete aliwahi kuagiza hizi 6 ila yakatokea mambo mengi saana, JW ikasitisha kuzichukua. Ikasubir mambo yapoe kwanza.

Kuna mambo hatuwez kuzungumza humu ila elewa tupo tunaotambua haya mambo vizuri.

Hope unamtambua Abdurlahman Shimbo, alikuwa mnadhimu wa JW kipindi cha JK.

Hio project ya hizo Cougar ilikuwa toka enzi za JK na walilipa.
 
Zile siraha nzito huwezi zitoa hazarani Ila mtindo huu wa kuonyesha siraha kwenye sherehe ni ushamba waache mara Moja ni kujichora zaidi
 
Ni risk sana kuleta silaha mpya kwenye maonesho ya wazi kama ya leo pale uhuru stadium...
Nakumbushia tu... Komandoo Kagame alikuwepo...

NB: Always play low profile to confuse your enemies...
 
Hivi ulishasikia wapi vita vikaishia angani ubora wa jeshi letu uko ardini mkuu

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Hapo mwisho ungemalizia na tusi ili iletee maana zaidi
 
Kuna uzi mwaka jana nilisema Kenya wana silaha kutuzidi watu wakanijia juu. Mada kama hizi huwa naongea kidogo mengine unapunguza makali, wewe uliona wapi duniani komandoo anabeba magogo mgongoni. Ukiwauliza hawa watakwambia ni kuonyesha ujasiri. Aisee, Israel ina wanajeshi wengine hata ngumi hawajui sasa fyatuka uingie nao vitani.

Last year walituonesha komandoo ana sufuria kabisaa. Leo angalau hawajaleta vituko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…