Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Wengi wao wanaosomesha watoto kwenye hizi shule za bei mbaya wanafanya hivyo kwa ajili ya kupata sifa tu na majigambo. Mimi ninaye jamaa yangu mmoja yeye anasomesha watoto wake shule ya International na analipia ada kiasi cha milioni 16 kwa mwaka kwa watoto wawili. Wakati yeye alisoma shule za kawaida (Kayumba) mpaka akafika chuo Kikuu.
Mbaya zaidi huyu jamaa sasa hivi uchumi wake umeyumba sana lakini bado anang'ang'ania tu kuendelea kusomesha watoto kwenye hiyo shule. Ni mtu ambaye anapenda sana sifa na ufahari na majigambo. Hashauriki hata kidogo na hata ndugu zake wakimshauri yeye anasema wanamwonea wivu. Natamani sana angeuona huu "uzi" labda kuna kitu angejifunza hapa kutokana na jinsi members walivyochangia.
 
H
hahahahaaaaaa hesabu hata iwe kwa lugha ya kiswahili kama akili hazichaji huwezi kufauru.
Hata hiyo mathematics huwezi kuelewa kama lugha haipandi na utakuwa huwezi kujisomea mwenyewe sababu kwenye vitabu kuna maelezo ya kutumia hizo kanuni na kwanini zitumike maelezo ambayo yameandikwa kwa English.

Wasioelewa lugha kamwe hawatoweza kusoma hivyo vitabu hivyo wataishia kukariri kanuni wanazofundishwa bila kujua kwanini then wanasahau baada ya muda.
Tafuta vitabu vyote vya hisabati lazima ukute maelezo ya English na sio namba tupu kama unavyodhani.

Hapo ndipo umuhimu wa English ulipo haikwepeki popote pale.
Bado sana kwa waafrika kuikataa English.
 

You nailed it
 
Wanajifariji tu hawa!
Hakika mkuu.

Wao wanaamini kuwa huko shule za private somo ni moja tu yaani English subject basi.
Hawajui masomo yote yanayofundishwa huko katani pia wanafundishwa ila kwa kiinglish,na ndio maana wanafanya mtihani mmoja Wa necta.

Kuna wamama wajane wanauza mbogamboga ila wanapambana wanapeleka watoto wao private school.

Mleta uzi utakuta ni kada Wa chama tawala,wamejitoa ufahamu.
 
Jamaa anapoint kubwa sana. Ukienda kwenye soko la ajira unakutana wengi st kayumba. Hawa wa shule za English medium wanachoweza na kuongea tu kizungu ila ni kama kuku wa kizungu. Wamezoea kuwa spoon fed.
Soko la ajira wapi huko ndugu ambapo kayumba ndio mmelishika? Eeenhe Mungu tusaidie, wana JF mbona kama uelewa unazidi kushuka siku hadi siku? Au mmekata tamaa na maisha ya jiwe? Soko la ajira hizi za TRA, TPA,TFDA, NIMR etc. Hizi? Naona exposure za humu zinaishia kuona hizi mamlaka/ Taasisi za serikali ndio big deal kiasi kwamba aliyeko huko ndio aliyetoboa katika soko la ajira, SMH! Hivi mnawawaza waliopo kwenye soko la ajira Katika international NGO’s , UN’s, Corporate world akina GGM, ABSA, hapa sisemei tellers 😀

Kuna sehemu ukiwa hukutani na st.kayumba hata mmoja leave alone hizi English medium schools za 3M. Sisi tuendelee kutambiana huku manispaa tu.
 
Tanzania hii soko kubwa la ajira ya uhakika lipo wapi? Unaongelea NGO sijui interrnational kwenye ajira za mkataba muda mfupi? Serikali hata ukiwa mfagia ofisi tyari ni ajira ya uhakika. Sio kampuni binafsi au NGO zinazokufa kila siku. Zungumza reality na sio mere wishfull thinkinga
 

Absa Tanzania nina jamaa zangu wawili, mmoja financial controler anaitwa benard tesha.. shule ya msingi tabata, na mwingine yupo absa pia head of business advisory anaitwa ibrahim nzutu kasoma shule ya msingi mapambano... hawa wote vijana na wamesoma kayumba kipindi ambacho english medium zipo tayari

English medium haikusaidii kupata kazi, bali ni uwezo wako wa kazi hata kama umesoma kayumba unapata kazi popote.. hiyo absa uliyoitaja nimekupa mifano...

Mimi mwenyewe kayumba ila nimeshafanya kazi ubalozi wa taifa moja kubwa sana.. na pia nimefanya kazi kampuni kubwa ya kigeni..
 
Duuuuh! “Ajira ya uhakika”! Ciao....
 

Umeongea pointi. Wengi tunafuata mkumbo baadae mambo yanatulemea. Kuna shule za laki sita tu mtoto unamsimamia vizuri anajua kingereza
 
Hesabu ni a l acha uongo mkuu,
 
Kwa kweli ni tatizo ndugu! Ajira za uhakika za serikali ya CCM za mishahara laki 5 unusu😀😀
 
Kiingereza mkuu😂😂
"Kjana wangu yuko std seven hizo shule, sikifichi anawa challenge hata majamaa waliosoma hizo ma A level za kata"
Kumbe jamaa anamsifia kijana wake kuwashinda ma A level lugha ya kigeni, mimi nilijua mpaka Applied Math, Phy, Bio n.k.
Alisikika mwanaJF mmoja akisema huo ni Utopolo Pro Max.
 
Tatizo ni kwamba tunazani kusomesha ni uwekezaji kumbe ni mchezo wa kubahatisha kama zilivyo kamari za kubet tu sasa ni kuchagua kubet au kukaa tu bila kubet
 
Hesabu ni a
l
acha uongo mkuu,
Mkuu tofautisha uongo, opinions, perspectives na facts.

Sasa nilichoandika sio uongo bali ni facts.
Na haiwezekani kupinga facts bila facts sababu utakuwa unakwenda against reality.

Na tayari umeshindwa kutumia facts kutetea hoja yako.
 
Kizazi chako shule za English medium zilikuwa hazijawa nyingi

Waajiri hawakuwa na options now mambo yamebadilika English medium wanakimbiza vibaya kwenye soko la ajira

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kizazi chako shule za English medium zilikuwa hazijawa nyingi

Waajiri hawakuwa na options now mambo yamebadilika English medium wanakimbiza vibaya kwenye soko la ajira

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app

Wakati Mimi ninasoma msingi, english medium za kipato cha kati level za tusiime zilikuwa kibao.. kama st marys kila wilaya, olimpio, esacs, academic, jk nyerere, taps
 
Duuuu!!! jamaaa umeongea vizuri sana aiseee.
 
Huu ni ujinga sana kuwaza hivi ina maana haujui kama hata KUSOMESHA pia ni UWEKEZAJI kwaajili ya hao unaowasomesha,kwasababu shule nzuri ina vingi vya ziada kwenye Malezi na Makuzi ya mtoto pia Elimu sio lazima mtu aje kuajiliwa au kuwa CEO....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…