Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Wengi wao wanaosomesha watoto kwenye hizi shule za bei mbaya wanafanya hivyo kwa ajili ya kupata sifa tu na majigambo. Mimi ninaye jamaa yangu mmoja yeye anasomesha watoto wake shule ya International na analipia ada kiasi cha milioni 16 kwa mwaka kwa watoto wawili. Wakati yeye alisoma shule za kawaida (Kayumba) mpaka akafika chuo Kikuu.Habari wadau..
January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.
Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.
Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.
Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..
Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Mbaya zaidi huyu jamaa sasa hivi uchumi wake umeyumba sana lakini bado anang'ang'ania tu kuendelea kusomesha watoto kwenye hiyo shule. Ni mtu ambaye anapenda sana sifa na ufahari na majigambo. Hashauriki hata kidogo na hata ndugu zake wakimshauri yeye anasema wanamwonea wivu. Natamani sana angeuona huu "uzi" labda kuna kitu angejifunza hapa kutokana na jinsi members walivyochangia.