Ok. Binafsi naona elimu ni msingi wa maendeleo ya wanangu. Na elimu hapa ni zaidi ya kufaulu darasani.
Kuna vitu vingi vya ziada shule binafsi (sio zote) zinatoa ambazo hupati shule za serikali.
Mfano, hata kujiamini na kujieleza tu kunaweza kuwa ni mlango wa mafanikio katika baadhi ya maeneo. Au kuwa na mtazamo fulani juu ya maisha na exoosure.
Hiki kitu kwa shule za serikali ni bidhaa adimu. Hapa kata yetu, mwaka huu tu drs la kwanza wameandikishwa wanafunzi elfu 1. Nilikua naongea na ndugu ambaye ni mwakimu hapo, walimu wako overhwelmed. Unakuta stress zote anamalizia kwa watoto.
Kwa kweli kwa kadri hali yangu ya fedha itakavyoruhusu, nawapeleka shule binafsi wanangu.
Hii hainizuii kuplan pia future nzuri kwa ajili yao. Nafikiri, tupambane kiuchumi tuwakwamue watoto.