Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Ok. Binafsi naona elimu ni msingi wa maendeleo ya wanangu. Na elimu hapa ni zaidi ya kufaulu darasani.

Kuna vitu vingi vya ziada shule binafsi (sio zote) zinatoa ambazo hupati shule za serikali.

Mfano, hata kujiamini na kujieleza tu kunaweza kuwa ni mlango wa mafanikio katika baadhi ya maeneo. Au kuwa na mtazamo fulani juu ya maisha na exoosure.

Hiki kitu kwa shule za serikali ni bidhaa adimu. Hapa kata yetu, mwaka huu tu drs la kwanza wameandikishwa wanafunzi elfu 1. Nilikua naongea na ndugu ambaye ni mwakimu hapo, walimu wako overhwelmed. Unakuta stress zote anamalizia kwa watoto.

Kwa kweli kwa kadri hali yangu ya fedha itakavyoruhusu, nawapeleka shule binafsi wanangu.

Hii hainizuii kuplan pia future nzuri kwa ajili yao. Nafikiri, tupambane kiuchumi tuwakwamue watoto.
Hilo halina mjadala mkuu, ila personally siwezi ku toil kwenda kuspend mahela Tusiime wakati kuna shule za serikali nzuri tu ambazo ukimpeleka mtoto ana excel bila shida. Kikubwa ni mtoto awe kichwa tu! Kokote atatoboa.
 
Hivi huu msemo Wa eti watoto wanaosoma shule za academics sijui private school eti wanaishia kujua lughatu,mi natofafautiama na we we mkuu,Kijana wangu yuko std seven hizo shule,sikifichi anawa challenge hata majamaa waliosoma hizo ma A level za kata.na wanamkubali mbaya.
Anawachallenge kwenye nini?
Ebu tuweke wazi kidogo
 
Ok. Binafsi naona elimu ni msingi wa maendeleo ya wanangu. Na elimu hapa ni zaidi ya kufaulu darasani.

Kuna vitu vingi vya ziada shule binafsi (sio zote) zinatoa ambazo hupati shule za serikali.

Mfano, hata kujiamini na kujieleza tu kunaweza kuwa ni mlango wa mafanikio katika baadhi ya maeneo. Au kuwa na mtazamo fulani juu ya maisha na exoosure.

Hiki kitu kwa shule za serikali ni bidhaa adimu. Hapa kata yetu, mwaka huu tu drs la kwanza wameandikishwa wanafunzi elfu 1. Nilikua naongea na ndugu ambaye ni mwakimu hapo, walimu wako overhwelmed. Unakuta stress zote anamalizia kwa watoto.

Kwa kweli kwa kadri hali yangu ya fedha itakavyoruhusu, nawapeleka shule binafsi wanangu.

Hii hainizuii kuplan pia future nzuri kwa ajili yao. Nafikiri, tupambane kiuchumi tuwakwamue watoto.
Kujiamini unamjengea mtoto wewe mwenyewe.

Kujifunza kutafuta maarifa ni zao la malezi hasa nyumbani.. mtoto anatakiwa ajifunze kupata kwa kutafuta.. sio kupewa..

Wengi majobless wanaopaka Poda Sinza wamesoma Medium kwa wengi ni swala jipya.. maana ndio tunashtuka.. ila hazina jipya lolote.. niamini.

Tumesomesha sana huko private na kumalizia Bablo na bado anafika UD anakuta vipanga wamesoma shule ya msingi Yombo, sekondari Gongo la Mboto, high school Benjamini na wananyoosha na in two or three years kingereza nao wanakijua na wanajua kuona fursa na kuzitumia.

Wanamuuzia mwanao T-shirt za kuprint, wanamleta visheti ambavyo yeye hajui hata kupika, wanaleta ubuyu.. yeye anatoka umtafutie na kazi...
 
Anasoma shule ya kawaida, binafsi hizi za laki kadhaa kila baada ya miezi 3, ila nikimuangalia mwanangu, jembe langu, mrithi wangu ninapata amani sana hawezi kuniangusha, kama baba nitahakikisha anapata zaidi ya uwezo wangu kwa sababu naye ni extra ordinary, CEO in the making
 
Acha tu mkuu wtu wanaenda na trending.
Uzuri tumejifunza kitu the hard way, ukikosa pesa huthaminiki! Hili ndio kosa la kwanza kurekebisha kwa watoto wetu ambao ndio generation ijayo. 😂😂😂 Cheti bila pesa ni Utopolo tu! Kijana wangu asije kushindwa kuchakata mama kali bure kwa kigezo hana mawe akae kinyonge staki kabisa huo upumbavu! Elimu atapata ila lazma awe na mzigo pia. Nitahakikisha hilo!
 
Lengo kuu la kwenda shule ni uhakika wa kufaulu?
Kufaulu ni kipimo cha kwamba knowledge iliyokusudiwa ameipata

Wenye kazi nzuri wengi walifaulu. Mzazi anajua watu kibao ambao walifaulu kisha wakapata kazi nzuri.

Kuanzia kwa Benno Ndulu, Kimei,nk
 
Shule ya Kayumba wanayosoma watoto wa viongozi haiwezi kuwa ya kipimbi mzee [emoji16][emoji16][emoji16]!
Huwezi fananisha Bunge Primary na shule ya kata uliosoma wewe.
But both are government schools.
Sitampeleka shule ya gharama kubwa ila nitajitahidi asome angalau shule nzuri kidogo kuliko shule ya kipuuzi niliyosoma mimi inafika hatua ukubwa ukirudi shule ya msingi ulipopitia unahisi kabisa walezi waliamua kukutelekeza na siyo kukusomesha[emoji16]
 
Acha tu mkuu wtu wanaenda na trending.
Uzuri tumejifunza kitu the hard way, ukikosa pesa huthaminiki! Hili ndio kosa la kwanza kurekebisha kwa watoto wetu ambao ndio generation ijayo. 😂😂😂 Cheti bila pesa ni Utopolo tu! Kijana wangu asije kushindwa kuchakata mama kali bure kwa kigezo hana mawe akae kinyonge staki kabisa huo upumbavu! Elimu atapata ila lazma awe na mzigo pia. Nitahakikisha hilo!

Mayweather anasemekana hana shule ila hakuna mpuuzi ambaye anaweza kuonesha aina yeyote ya dharau kwake!
 
Ni kweli 90% ila wazazi wengi ni ngumu kukuelewa wao wanachojua mafanikio lazima shule that's why wana wekeza huko to the extent bila,kujali uwezo wa mtoto na kipaji
Takwimu pia zinaonyesha asimia 90 ya waliosoma hufanikiwa kimaisha ambao huwa hawajasoma na kufanikiwa kimaisha ni asilimia 10 tu hapo ndipo wanaangukia akina Diamond na akina Bakheresa wasiosoma .Somesha
 
Kujiamini unamjengea mtoto wewe mwenyewe.

Kujifunza kutafuta maarifa ni zao la malezi hasa nyumbani.. mtoto anatakiwa ajifunze kupata kwa kutafuta.. sio kupewa..

Wengi majobless wanaopaka Poda sinza wamesoma Medium kwa wengi ni swala jipya.. maana ndio tunashtuka.. ila hazina jipya lolote.. niamini.

Tumesomesha sana huko private na kumalizia Bablo na bado anafika UD anakuta vipanga wamesoma shule ya msingi yombo, sekondari gongo la Mboto, highschool Benjamini na wanamyoosha na in two or three years kingereza nao wanakijua na wanajua kuona fursa na kuzitumia.

Wanamuuzia mwanao T-shirt za kuprint, wanamleta visheti ambavyo yeye hajui hata kupika, wanaleta ubuyu.. yeye anatoka umtafutie na kazi...
Sikatai. Hata mimi nimesoma huko mwanzo mwisho. Na kutokana na background yetu kama famikia, naweza kusema nimetoboa kiasi.

Ila sasa, usitumie hii kumfanya mwanao awe mnyonge baadae. Yes, anaweza kufuata nyayo zako na akatoboa hata kwa Kayumba. Lakini what if he doesn't?

Private sio uhakika wa kutoboa. Lakn walau kuna ziada inapatikana ya kutumia hata asipotoboa.
 
Sitampeleka shule ya gharama kubwa ila nitajitahid asome angalau shule nzuri kidogo kuliko shule ya kipuuzi niliyo soma mm inafika hatua ukubwan ukirud shule ya msingi ulipo pitia unahisi kabsa walezi waliamua kukutelekeza na siyo kukusomesha[emoji16]
wazee walikutelekezea shule sio 😂😂😂
 
Sikatai. Hata mimi nimesoma huko mwanzo mwisho. Na kutokana na background yetu kama famikia, naweza kusema nimetoboa kiasi.

Ila sasa, usitumie hii kumfanya mwanao awe mnyonge baadae. Yes, anaweza kufuata nyayo zako na akatoboa hata kwa Kayumba. Lakini what if he doesn't?

Private sio uhakika wa kutoboa. Lakn walau kuna ziada inapatikana ya kutumia hata asipotoboa.
Ishu ni kujipanga mwanao asiishi kifala kama ambavyo wengi tunapitia! Ile hali ya mtoto kuvaa joho na kuanza kubung'aa bung'aa hana pa kushika ni bonge moja la fedhea in case mzee ulimaliza nguvu zote kulipa ma ada tu!

Wether atasoma private au kata ila hakikisha akitoka kwenye mlango wa chuo ana status yake nzuri tu maishani.
 
takwimu pia zinaonyesha asimia 90 ya walosoma hufanikiwa kimaisha ambao huwa hawajasoma na kufanikiwa kimaisha ni asilimia 10 tu hapi ndipo wanaangukia akina Diamond na akina Bakheresa .

90% ya wasomi wanafanikiwa?? Ebu tupe definition ya kufanikiwa kwanza!! Maana hao wasomi wa kutegemea mshahara na kununua gari na kujenga kwa mkopo,mshahara ukitoka tarehe 28 baada ya siku 10 ushakata ndio mafanikio hayo?
 
takwimu pia zinaonyesha asimia 90 ya walosoma hufanikiwa kimaisha ambao huwa hawajasoma na kufanikiwa kimaisha ni asilimia 10 tu hapo ndipo wanaangukia akina Diamond na akina Bakheresa wasiosoma .Somesha
Ni kweli tunahitaji matajiri wengi zaidi! Ni wakati wa kuelekeza nguvu nyingi huko kwenye utaftaji mali tu 🙏
 
Back
Top Bottom