Kama wewe ni mwanaume na unajipikilisha, juwa bado hujakua

Kama wewe ni mwanaume na unajipikilisha, juwa bado hujakua

Hahaha. Kwamba unakua unaweza kupiga ugali Ila mboga huwezi mkuu? Katakata tu hizo nyanya pia. Chakula hakijuagi jinsia ya anayekipika.
Ishu sio kutojua. Suala la kupika zile basic skills mbona wengi tu tunajua. Ishu ni kubanwa na ratiba na ile kuona suala la kupika sio muhimu kiasi cha kukupotezea muda
 
Sio kila mtu au kila mwanaume anakula ugali.

Pia ni ujinga na uswahili unapika ugali halafu jitu zima na ndevu zako unatembea na vibobo vya mboga barabarani eti umetoka kununua maharage ya nazi kwa mwanahamisi.
Acha kukulupuka kijana ugali umetolewa mfano tu, na suala la kununua msosi siku hizi kuna delivery sio lazima utoke kwenda mwenyewe kama zamani. Wewe kaa kwenye kibao cha mbuzi kuna nazi zako uunge mboga. Chakula kikiiva mwite mkeo aje kula. Sisi wengine malezi tuliyopewa jikoni sio sehemu ya mwanaume kuonekana
 
Kama wewe ni mwanaume na bado unaingia jikoni kupika au kujipikilisha, juwa bado wewe ni mtoto, bado hujakuwa; ukikuwa utaachana na hayo mambo.

Unatakiwa uambiwe, kaka/baba/babu/mume/shemeji chakula tayari karibu mezani.​
Ulikuwa unataka tu comments. Haya umezipata sasa sijui zitakusaidia nini
 
Dogo endelea kusali kwa mola wako mipango iendelee kujiset, hata yakikukuta uwe na uwezo wa kununua mgahawani kama sio kwa mama ntilie
 
Unaweza ukawa baba mwenye nyumba na bado ukapika sa sjui point yako ni nini

Kupika au kupikiwa sio sababu ya heshima ya mtu kushuka ama kupanda
 
Na alivo na njaa za kutetemeka, ni vizuri kujifunza kupika hata vitu vidogo vidogo sababu sio muda wote utakuwa na access na sehemu za kula/mpishi.
Hawa ni watu waliokulia nyumba zenye uhakika. Yani ukulie nyumba hohehahe, huna dada wa kazi ama madada wa kuwahangaisha kukupikia halafu usijue kupika NEVER

Kwenye group la wanaojua kupika sipo na sio mpenzi wa kupika ila kupika cha kula mwenyewe. Sio issue
 
Hawa ni watu waliokulia nyumba zenye uhakika. Yani ukulie nyumba hohehahe, huna dada wa kazi ama madada wa kuwahangaisha kukupikia halafu usijue kupika NEVER

Kwenye group la wanaojua kupika sipo na sio mpenzi wa kupika ila kupika cha kula mwenyewe. Sio issue
Uko sahihi, Kupika ni basic skill/survival skill kila mtu anapaswa kujua.

Hebu tuone chakula ulichopika cha kula mwenyewe basi 😅😭
 
Back
Top Bottom