Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Uongo mtupu !
Nahisi kulikuwa hakuna mawasiliano mazuri kwenye hili, ni kweli kuna wajumbe kutoka chadema walihudhuria hiko kikao cha maadili.
Kama chama hakikubaliani na uamuzi huu basi hawa wajumbe wanapaswa kuchukuliwa hatu kali na chama.
Unawafahamu wajumbe wa chadema waliohudhuria?? Ningeweza kukutajia, shida mna ujuaji sana huku chama hamkijui
 
Tume hii iliyojaa doublestand nani mwenye akili ataiamini?!

Ina maana kwenye hizo form za kugombea wahusika hawajazi ananuani zao?

Na kama hawajazi anuani tofauti na za vyama vyao bali wanajaza za chama,nani alipaswa kuwa addressed kwenye hiyo barua kupitia ananuani ya chama?

Je,si walipaswa kumu-address Lissu kama mgombea kupitia anuani ya chama chake?
Eeeh! Vimenukuliwa vifungu vya sheria vinavyoonga kamati hiyo. Sasa ninyi si niakili kubwa , wapenda haki(lakini hampendi wajibu wa haki hiyo) mnashindwaje kuelewa maelezo ya kamati na tume!?
 
Sometimes ni bora kuacha vitu flani vipite tu ili kuepuka kuwapa watu nafasi adimu ya kukusurubu. Siku 7 sio nyingi sana na bahati nzuri mawakala/wawakilishi wa Lissu wanaweza kumpigia campaign kwa fujo ndani ya hizo 7 days

Kama kanuni zao zinasema hivyo, then Lissu hana ujanja. Huu sio muda sahihi sana wa kuzishambulia kanuni kama zilikuwa wazi tangu mwanzo.

Nadhani ni hoja isiyo na nguvu sana kusema eti wito alipaswa kukabidhiwa mkononi na sio kupitia kwenye Chama
 
Nahisi kulikuwa hakuna mawasiliano mazuri kwenye hili, ni kweli kuna wajumbe kutoka chadema walihudhuria hiko kikao cha maadili.
Kama chama hakikubaliani na uamuzi huu basi hawa wajumbe wanapaswa kuchukuliwa hatu kali na chama.
Unawafahamu wajumbe wa chadema waliohudhuria?? Ningeweza kukutajia, shida mna ujuaji sana huku chama hamkijui
Mawakili wa Lissu sio wajumbe wa Chadema. Na kama ni mawakili walioshiriki basi Chadema haikushiriki.

Amandla...
 
KAMATI YA MAADILI: Baadhi ya watu kutaka kuwaaminisha umma wa watanzania kwamba mgombea huyo ameadhibiwa na tume ya Taifa ya uchaguzi, ukweli ni kwamba bwana Lissu ameadhibiwa na kamati amabayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa kiti cha Rais.

Wajumbe 15 kutoka vyama vya Ada-Tadea, CUF, SAU, UPDP, CHADEMA, CHAUMMA, CCM, NCCR-Mageuzi, DP, UMD, ACT-Wazalendo, NRA, Demokrasia Makini, ADC na AAFP ndio waliotoa adhabu kwa bwana Tundu Lissu.

Kamati pia ina mjumbe kutoka serikalini na mjumbe kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi ambaye ni mwenyekiti wa kamati.

Ifahamike kwamba katika kikao hicho, kulikuwa na mawakili wawili nguli kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) waliosimama kutetea hoja ya bwana Tundu Lissu.

Walisimama mbele ya kamati kujibu hoja zilizokuwepo na kudai kwamba Tundu Lissu na CHADEMA ni vitu viwili tofauti.

Kwa kuzingatia adhabu zilizoainishwa katika kanuni ya 5.11 ya maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 mgombea huyo amepewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa muda wa siku 7 kuanzia leo tarehe tatu Octoba mpaka tarehe tisa Octoba. Hii ina maana kwamba haruhusiwi kufanya kampeni zake yeye mwenyewe wala kwa ajili ya mgombea mwingine awaye yeyote.

Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni atambue kuwa kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5.7L ya maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2020. Ikimbukwe kuwa katika kipindi cha uchaguzi, sheria nyingine za nchi hazijaacha kufanya kazi.

==============

Hivi punde kamati imetoa sababu na imejibu baadhi ya hoja za Lissu kuhusu adhabu hiyo

Kamati inasema
(1)Kwamba kwa mujibu wa kanuni bsrua za wito hupeekrwa katibu mkuu wa chama maana huyo ndo wana anuani zake, na kamati haitunzi anuani za mtu binafsi

(2) Kamati inasema tsrehe 24 September Lissu ashapelekewa malalamiko na chama cha SAU yaliyokuja kwa mtindo huu huu yalivyokuja safari hii na Lissu akayajibu, Kamati inashangaa iweje leo Lissu akosoe utaratibu huu, Kamati imumuita Lissu ni Muongo

(3) Akijibu maswali ya waandishi Ofisa kamati amesema kwa adhabu hii aliyopewa Lissu haruhusiwi kupanda majukwaani na kuwanadi Madiwani au Wabunge maana kitendo cha yeye kupanda majukwaani tu inahesabika kuwa kafanya kampeni

(4)Msomaji wa Taarifa ya kamati asema kuwa adhabu inamhusu Lissu tu, haihusu mawakala wake, kwa hiyo watu wengine wenye dhamana ya kumpigia kampeni wanaruhusiwa kuendelea kumpigia kampeni

Kwa taarifa zaidi tazama video hii hapa:
View attachment 1588923View attachment 1588924View attachment 1588925

Hoja za Lissu kuhusu adhabu hazina mashiko kisheria hata yeye nwenyewe anajua .
Mtu yeyote yule ana physical address yake ambayo ndiyo hutumika pale anapotakiwa kupewa documents. Lissu kama mgombea wa urais kupitia CHADEMA na pia makamu m/ kiti wa chama hicho hawezi dai eti ofisi ya KM wa CHADEMA sio care of (c/f) ya mgombea urais wa CHADEM au Lissu as lon9g as bado ana wadhifa hapo. Vinginevyo aseme physical addresss yake ni ipi maana hakuna mtu mwenye mobile physical address.

Katika nchi yeyote ile kuna mifumo ya kimaamuzi ambayo inawabana wahusika once maamuzi yakitolewa hata kama kuna mtu hakubaliani nayo labda akate rufaa chombo cha juu na uamuzi wa chini utenguliwe.

Lissu alikuwa na nafasi ya kujitetea pengine angeweza kushinda lakini kwa kuburi na kujiona yeye tu ndiye yuko sahihi siku zote na ndiye anayejua akadharau wito; hivyo kesi ikasikilizwa upande mmoja bila maelezo yake ya utetezi.

Hakuna mtu anayeweza kushindana na DOLA katika nchi yeyote hata kama mtu huyo awali alikuwa rais. Lissu hataweza kushindana na dola na hao wanaomdanganya kupitia key board hawatamsaidia lolote.

Dunia kwa sasa ni bipolar haiendeshwi na nchi za magharibi pekee, kuna nchi kama China na Urusi ambazo zimekuwa zukiikabili vilivyo Marekani, hivyo ni kujidanganys eti Tanzania itazipigia magoti nchi za magharibi. Amkumbuke Morgan wa Zimbabwe hadi amekufa alifanikiwa kuing' oa ZANU PF au Mugabe? Syria Venezuela au Iran hali kadhalika?

Uchaguzi utafanyika kihalali na Lissu atashindwa kihalali japo hatakubali matokeo na atawadanganya wafuasi wake aneshinda na ameporwa ushindi lakini haitabadilisha chochote na maisha yatasonga mbele.

Hatuwezi kuwa na nchi kila mmoja ni muamuzi wa kila jambo linalomuhusu, ukifikia hapo unaruhusu anarchy. Lazima pawepo na vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria ili kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu watu. Si lazima wote tukubaliane na maamuzi ya vyombo vilivyowekwa kisheria lakini tuna wajibu wa kutii maamuzi halali yaliyotolewa na vyombo hivyo.

Kuna watu wanamdanganya eti asitii adhabu aendelee na kampeni haya mtumbukizeni shimoni lakini wakati anaangamia atakuwa peke yake.
 
Pamoja na kuwa upande wa lissu, lakini kuna sehemu anakosea.
Sehemu yenyewe ni; Lissu sio mgombea binafsi hivyo barua haiwezi kupelekwa kwake binafsi bali itapitia chama ambacho ndio anakitumia kugombea.
Ingekuwa jambo la ajabu sana kama NEC wangemplekea lissu barua yeye kama yeye badala ya chama
Sasa kuhusu yaliyomo kwenye barua mimi sidhani kama yana mashiko.
Mwisho kabisa, hadi sasa lissu ni kama ashatengeneza mgogoro na NEC, je anategemea kushinda kwenye mazingira gani na je anategemea wagombea wa ubunge na udiwani watashindaje?
Au ndio tutasema kuwa hatutakubali? Hakuna tena jipya chini ya jua, naona kabisa yatatokea yale yaliyotokea uchaguzi wa serikali za mitaa na mwisho wa siku chama ndio kitaathirika

Hivi unaamini NEC watatangaza ushindi wa mtu mwingine tofauti na yule ambae wao wanampigia debe? Mtu mwingine anaweza kutangazwa kama tu patatokea msukumo mkubwa kutoka kwa wapiga kura. Anachokifanya Lissu ni kuamsha hisia wa wapiga kura wake ili waweze kushinikiza wagombea wao ( urais, ubunge na udiwani) watangazwe. Na kama ya uchaguzi wa serikali za mitaa ( ushindi wa asilimia 100) sidhani kama watu watakaa kimya. Nahisi NEC itakuwa makini kuhakikisha kuwa wapinzani wengi zaidi watakaoshinda wanatangazwa ili wapate legitimacy.

Amandla...
 
Lissu anasimamia sheria gani [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]mbavu zangu

Huyu mwana kuropoka
Kama una ushabiki uliopitiliza huwezi kufuatilia mwenendo na kusikiliza ufafanuzi wa sheria, lakini pia kuelewa ni kipaji
 
Hoja za Lissu kuhusu adhabu hazina mashiko kisheria hata yeye nwenyewe anajua .
Mtu yeyote yule ana physical address yake ambayo ndiyo hutumika pale anapotakiwa kupewa documents. Lissu kama mgombea wa urais kupitia CHADEMA na pia makamu m/ kiti wa chama hicho hawezi dai eti ofisi ya KM wa CHADEMA sio care of (c/f) ya mgombea urais wa CHADEM au Lissu as lon9g as bado ana wadhifa hapo. Vinginevyo aseme physical addresss yake ni ipi maana hakuna mtu mwenye mobile physical address.

Katika nchi yeyote ile kuna mifumo ya kimaamuzi ambayo inawabana wahusika once maamuzi yakitolewa hata kama kuna mtu hakubaliani nayo labda akate rufaa chombo cha juu na uamuzi wa chini utenguliwe.

Lissu alikuwa na nafasi ya kujitetea pengine angeweza kushinda lakini kwa kuburi na kujiona yeye tu ndiye yuko sahihi siku zote na ndiye anayejua akadharau wito; hivyo kesi ikasikilizwa upande mmoja bila maelezo yake ya utetezi.

Hakuna mtu anayeweza kushindana na DOLA katika nchi yeyote hata kama mtu huyo awali alikuwa rais. Lissu hataweza kushindana na dola na hao wanaomdanganya kupitia key board hawatamsaidia lolote.

Dunia kwa sasa ni bipolar haiendeshwi na nchi za magharibi pekee, kuna nchi kama China na Urusi ambazo zimekuwa zukiikabili vilivyo Marekani, hivyo ni kujidanganys eti Tanzania itazipigia magoti nchi za magharibi. Amkumbuke Morgan wa Zimbabwe hadi amekufa alifanikiwa kuing' oa ZANU PF au Mugabe? Syria Venezuela au Iran hali kadhalika?

Uchaguzi utafanyika kihalali na Lissu atashindwa kihalali japo hatakubali matokeo na atawadanganya wafuasi wake aneshinda na ameporwa ushindi lakini haitabadilisha chochote na maisha yatasonga mbele.

Hatuwezi kuwa na nchi kila mmoja ni muamuzi wa kila jambo linalomuhusu, ukifikia hapo unaruhusu anarchy. Lazima pawepo na vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria ili kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu watu. Si lazima wote tukubaliane na maamuzi ya vyombo vilivyowekwa kisheria lakini tuna wajibu wa kutii maamuzi halali yaliyotolewa na vyombo hivyo.

Kuna watu wanamdanganya eti asitii adhabu aendelee na kampeni haya mtumbukizeni shimoni lakini wakati anaangamia atakuwa peke yake.
Chama cha PRI cha Mexico kiliongoza kwa miaka 71, kuanzia mwaka 1929 hadi 2000. Bila shaka na chenyewe kilidhani kuwa hakitaweza kushindwa lakini hatimae wananchi walikikataa. Vyama vya KANU, UNIP cha Zambia ambacho mtoto wa Kaunda hajawahi kushinda zaidi ya 1% n.k. navyo viliamini vitakuwepo milele. Kosa ambalo linafanywa ni kudhani kuwa ushindi wa Lissu, Maalim, Chadema na ACT utatokana na kutangazwa na NEC na wabunge na madiwani wao kushinda viti vingi. Hii sio kweli. Hawa kwa kuonyesha mwamko mkubwa wa wananchi kutokubaliana na hali ilivyo ni ushindi tosha na ishara kuwa CCM wasipokuwa waangalifu, kama si leo kesho, watajikuta wanakataliwa kiasi cha kushindwa kulazimisha ushindi. Kwa wale ambao wanakitakia mema, watajua kuwa kuna haja ya kubadilika. Haya tumeanza kuyaona katika matamshi ya viongozi wake na hii ni faida kwa wote. Ukweli ni kuwa mpaka sasa hivi upinzani ambao ulisemwa kuwa umeishakufa umeshinda hata kama hawatapata urais au uongozi wa bunge.

Amandla...
 
YANI VYAMA VILIVYOSHIRIKI KWENYE KAMATI YA MAADILI VINGI VYAO HAVIIPENDI CHADEMA, NA NDIO VILE HATA HAVIJAWAHI KUTOA MBUNGE NA VIKISIKIA TU CHADEMA WANASUSA HIVYO NDIO VINAJITOKEZA KUSHIRIKI.
LEO HII VISHIRIKI KUMUADHIBU MGOMBEA WA CHADEMA UTEGEMEE KABISA VITAMTENDEA HAKI?
NEC WALIKAA KUSUBIRIA POLISI WAMWADHIBU LISU ILA POLISI WAKAMSAMEE, KUMBE MSAMAHA WAO ULIWAUDHI SANA NEC, NA MBAYA ZAIDI NI BAADA YA KUONA CHADEMA WANASHANGILIA,HIVYO WAKAITISHA KIKAO CHA FASTA FASTA KUWAKOMOA.
 
Asante umenisaidia kuongeza ufafanuzi, make huyo bwana anaejiita "bia yetu" "huenda ataekewa" kama "hajalewa"
 
Kama imejaa wateuzi wa Magufuli of which ni CCM.....halafu kamati hiyo hiyo imejaa vyama vya siasa ambavyo ni pinzani...

Hivyo it is in their best interest kuondoa contestant among themselves wabakie wachache waendelee kukiwa na upinzani kidogo among themselves...

Yaani ni elimination game..

Hakuna eti atakaeletwa kwenye kamati asiondolewe kabisa,maana kila mmoja anataka wagombea wapunguzwe isipokua yeye binafsi....

Hivyo hii kamati ni totally flawed kimuundo..ni kama hii kamati ingeundwa na members wasio na affiliation na upande wowote whatsoever!

Tume ya Taifa iliyounda hii kamati ni tatizo,ni mojawapo wa what is very wrong with the brains of our leading class!
 
Chadema walikuwepo pia. Shida nayoiona ni waru kutojua kinachoendelea either kwa makusudi au basi tu
YANI VYAMA VILIVYOSHIRIKI KWENYE KAMATI YA MAADILI VINGI VYAO HAVIIPENDI CHADEMA, NA NDIO VILE HATA HAVIJAWAHI KUTOA MBUNGE NA VIKISIKIA TU CHADEMA WANASUSA HIVYO NDIO VINAJITOKEZA KUSHIRIKI.
LEO HII VISHIRIKI KUMUADHIBU MGOMBEA WA CHADEMA UTEGEMEE KABISA VITAMTENDEA HAKI?
NEC WALIKAA KUSUBIRIA POLISI WAMWADHIBU LISU ILA POLISI WAKAMSAMEE, KUMBE MSAMAHA WAO ULIWAUDHI SANA NEC, NA MBAYA ZAIDI NI BAADA YA KUONA CHADEMA WANASHANGILIA,HIVYO WAKAITISHA KIKAO CHA FASTA FASTA KUWAKOMOA.
 
Mataahira sijui mkoje!!! yaani Lissu anavunja kanuni, anaadhibiwa hamtaki!! sasa ataongozaje nchi kama hataki kufuata Kanuni??
Kampeni zilishawashinda chama mbogamboga kilicho bakia mnatumi mbeleko.Hilo nalo hutaki kukubali.
 
Back
Top Bottom