Kanusho: Bodaboda na Bajaji hawajapigwa marufuku kuingia katikati ya Jiji kuanzia Alhamisi 21 Aprili, 2022

😁😁 sasa mjinga kama wewe nikujibu nini?

Huo u RC wenyewe hata ungeroga ukoo na kijiji chenu chote huwezi pata
Hahahahahaha Asante, naona pointi imezama kabisa kunako.
 
Bajaji wamejitakia haya wenyewe jamaa sio wastaarabu kabisa hawazingatii alama za barabarani wanalenga kabisa wapita kwa miguu hawawapishi.

Tabia mbaya sana hiyo.
 
Bajaji wamejitakia haya wenyewe jamaa sio wastaarabu kabisa hawazingatii alama za barabarani wanalenga kabisa wapita kwa miguu hawawapishi.

Tabia mbaya sana hiyo.
Zebra crossing hawasimami, red light hawasimami, kuchomekea hovyo hovyo. Ni kero tu hao.
 
Kwani India na China zinatembea wapi na wapi tu, si tuige waliotuletea Ili watuambie na matumizi yake!
 
Habari njema Kwa wazee WA taxi uber na bolt
 
Basi wayaondoe mjini pia maduka ya kuuzia bodaboda na bajaji...

Wenye Ist, vitz nanyie jiandaeni kisaikolojia πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Maduka yoote yanayouza piki piki na vipuri vyake vitolewe mjini , twende sawa maana sio VAT za piki piki wanazitaka lakini hawataki piki piki ziwepo , basi wilaya zinazo tumia piki piki zifaidike na VAT pia
 
Kwanini mnaziachia Guta na Mikocheni? ni aibu kubwa kwa jiji.
 
Mjini tunatakiwa wenye vieite tu.

Kuanzia July mwaka mpya wa fedha IST, Raum, Passo, Vitz na gari za mtindo huo zitapigwa marufuku kukanyaga mjini.

Gari zinazotakiwa kukaganya mjini ni kuanzia angalau Rav 4 tena za kuanzia 2008 na kuendelea.
 
Ni Bora waweke utaratibu Kwa Sasa Bado kero ni kubwa kama umeamua kutembea zako Mjini Kwa miguu! Pia Machinga Bado ni Jipu
 
Hapo utakuta washawaza kutengeneza hela tu hakuna kitu,wanaacha kufanyia kazi report ya cag
 
Hizi marufuku hizi ni kwa wanyonge tu?mara tumesikia gari za nyuma ya mwaka 2010 zisiingie nchini!...nadhani mawazo haya huanzia kwenye kichwa cha mtu mmoja tu ambaye katosheka anapata mamilioni kwa siku chache ,v8 la mkopo tena lenye msamaha wa kodi, mafuta ya bure lita 75 kila wiki...saa ngapi atafikiria walala hoi?
 
Tatizo la watanzania wengi, ni kuendekeza umaskini! Boda boda zimeleta majanga mengi sana hasa hapa Dar. Vifo kwa wingi, vilema kwa wingi, wizi wa kupindikia, ni muhimu kudhibitiwa!
Wengi hawana leseni, wanaendesha wanavyotaka huku trafiki wakijifanya hawawaoni eti "hawawawezi"! Ujinga mtupu!
Kuna njia mbadala za kuwezeaha vijana kujiajiri, siyo boda boda peke yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…