Karatu imesimama muda huu na habari ni Tundu Lissu
Picha: Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano kupitia CHADEMA akipita Karatu kuelekea wilayani Hai ambapo atakuwa na mkutano wa kampeni kesho. Umati mkubwa wa watu unejitokeza barababrani kumsalimu huku akitarajiwa kurejea Karatu siku za baadaye kwa mkutano wa kampeni.
View attachment 1584481
View attachment 1584489
View attachment 1584502
Uamuzi wa tume ya uchaguzi kuipendelea kwa uwazi CCM, unampa Tundu Lissu kongole za ziada. Safari yake ya kuja ktk kamati ya maadili ya tume, inaonekana kama vile safari halisi ya ukombozi. Wananchi wanatambua ya kwamba maamuzi ya tume yana "double standards" kwa kuwa hayamgusi mgombea wa CCM, ambaye mara kwa mara anakiuka kanuni na maadili na kukaliwa kimya.
Wananchi sasa hawadanganyiki tena. Wameng'amua ya kuwa tume imepewa maelekezo na CCM, na inafanya hivyo ili kujaribu kumtoa mkombozi wao kutoka ktk reli ya safari yake yenye matumaini. Tume na CCM hatambui kanuni za mahesabu za kiroho ambazo zipo ndani ya namba. Ni wao ndiyo waliiweka siku ya Jumatano, ya tarehe 28 ya mwezi wa 10 mwaka 2020 kuwa ndiyo siku ya uchaguzi.
Pande zote kinzani za kiroho, yaani ulimwengu wa nuru na ule wa giza, hutambua mnyumbulisho wa namba hufungwa na jumuisho lenye "single digit number". Kwa siku ya tarehe 28 kwa maana ya 2+8=10, hivyo kwa namba hii 10 hutupa tafsiri ya 1+0=1 kwa maana ya "single digit number".
Kwa hiyo tunaiona tena namba hii 10 ikitokea ktk mwezi wa kumi.
Mwaka 2020 kupitia kanuni hii ya "single digit number" ni 2+0+2+0=4. Na siku ya Jumatano inabaki na namba yake 5, ingawaje ktk ulimwengu wa nuru wa kiroho, siku ya Jumapili ndiyo siku ya kwanza ya juma kwa mantiki hiyo siku ya Jumatano hutambuliwa kama siku ya nne, hivyo huwakilishwa na namba 4.
Kwa kupitia kanuni hii tunapata "single digit number 1" kwa mara mbili, yaani ikiwakilishwa kupitia tarehe 28 na mwezi wa kumi. Vile vile tunapata "single digit number 4" kwa mara mbili, yaani siku ya Jumatano ikisomeka ktk ulimwengu wa nuru kiroho na mwaka 2020 ambao ni wa uchaguzi.
Namba 1 ni namba ya mamlaka ya Mungu mwenyewe, yeye ndiye wa Mwanzo na Mwisho, Alpha na Omega. Kwa hiyo ni kwa vyovyote vile yule ataibuka kuwa mshindi wa kweli kupitia sanduku la kura ndiye atakuwa namba 1 akimwakilisha YEYE ambaye ndiye 1. Katika andilo la kinabii tunaona MENE, MENE, TEKELI & PERESI. Neno MENE likijirudia kwa mara mbili, yaani namba 2.
Katika ulimwengu wa nuru wa kiroho, namba hii 2 inaonyesha maagano mawili ambayo Mungu amefanya na watu wake. Lipo Agano la Kale na pia lipo Agano Jipya. Kwa kupitia tafsiri za uwepo wa namba 1 kwa mara 2 tunaweza tunaweza kuiona "icon" ya Mussa na Yesu Kristo, hali katika uchaguzi wetu wa mwaka huu tunaiona "icon" ya uwakilishi wa Nyerere na Lissu.
Tukigeukia namba 4, ambayo inakibeba siku ya Jumatano na mwaka 2020, kwa maana ile ile ya uwepo wake kwa mara 2. Hii hutupa mshindi kukubalika pande zote za nchi, yaani Kusini na Kaskazini na hata Mashariki na Magharibi. Hii ndiyo ambayo viongozi wa kweli huiona juu ya Tundu Lissu. Huyu amepewa kibali na Mungu, na nyota yake imepata kibali ktk ulimwengu wa nuru wa kiroho.
Hii sasa ndiyo inapokuja uwepo wa namba 5. Hii ktk ulimwengu wa nuru wa kiroho humaanisha upendeleo ambao mja huupata kutoka kwa Bwana wake (rejea Mwanzo 43:31-34; 45:21-24). Namba katika tafsiri ya kiroho haziongopi, tuelekeapo siku ya uchaguzi neno hili na litafikia ukamilifu wake wote.